Kwanini Wahalifu wengine waitwe Magaidi na wengine waitwe Waasi?

mockers

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
12,806
35,220
Dunia na Mikanganyiko yake!

Hayo makundi yote yanafanya uhalifu sawa sawa katika nchi zao, makundi mengi hayazitambui serikali za nchi zao. Nini sababu kubwa ya makundi hayo kwenye nchi za waislamu kuitwa magaidi na sheria kali kutungwa dhidi yao, kwa mfano Somalia, Yemen, CAR, Mali na Msumbiji, halafu uhalifu kwenye nchi za wakristo wengi kama Haiti, Uturuki, Mexico, DR Congo, Uganda wahalifu hao waitwe waasi na hakuna sheria za kidunia za kupambana na waasi wakati hao wote hufanya uhalifu unaofanana?

Haiwezi kuwa janja za kijasusi kuchafua dini za watu wengine au inakuaje? Maana hao wahalifu kazi zao zinafanana kabisa na hawana tofauti Kwa uhalifu wao.

Tuangalie kwa uhuru, nini kinakua nyuma ya hilo suala?

Houth, Hamas ni magaidi lakini M23 na wale wa haiti ni waasi, Boko Haram ni magaidi lakini Tamil Tigers wao ni waasi! Kuna nini hapo kwenye hiyo mikanganyiko?

Kama Dunia iko fair basi wote wawe treated sawa kabisa, tena watungiwe sheria sawia ili kuwabana wote na uhalifu wao.
 
Magaidi wengi wamejipambanua kwa imani yao na huainisha kupigania kusimamisha dola ya kiislam mahali wanapotaka. Hao waasi sioni wakijitanabaisha wako mrengo gani kidini, waasi hua na mrengo tofauti na serikali (kisiasa).

Muasi ni mwananchi wa nchi husika, ila kaamua kua upande tofauti na serikali yake(ameasi). Gaidi si lazima awe wa nchi husika huweza kutokea ng'ambo. Na gaidi hana nchi yeye ni popote analipua tu.

Kwahiyo ukiitwa gaidi basi wewe ni adui wa dunia, ila muasi unaweza kimbia na kwenda kupata hifadhi nchi nyingine na ukaishi huko bila wasi.
 
Uasi na ugaidi haya yote ni mambo yakiharifu kwahiyo sioni haja yoyote yawewe kulialia kana kwamba kuna anaebebwa maana si gaidi si muasi wapuuzi wote hawa wanaua raia,wanaharibu miundo mbinu n.k.

Na hii shida yawewe kuona hivyo nikwasababu unaufinyu wa fikra!,nyie viumbe wa namna hii mnakera sana hamjui tu!.. mmekumbatia mambo ya dini tena dini zenyewe hata sio za mababu zenu!.

Ungekuwa unaupeo ungekuja na hoja yakuikomboa Africa itokane na haya mambo yakipuuzi yanayoendelea ila umelewa udini fikra zako zinanjaa tupu!, mi watu wa dini nawashangaa sana hiyo miungu yenu kama ingekuwa inawapenda basi ingewapa amani na furaha lkn ni karaha tupu tu!.

Kuna kila haja yakutibu fikra zenu kabla yakusema mnatibu matatizo yanayowakabili maana matatizo ni hizo fikra zenu butu.
 
unaufahamu mfinyu sana!,uasi na ugaidi haya yote ni mambo yakiharifu kwahiyo sioni haja yoyote yawewe kulialia kana kwamba kuna anaebebwa maana si gaidi si muasi wapuuzi wote hawa wanaua raia,wanaharibu miundo mbinu n.k...
Nitake radhi unatakiwa ujibu Kwa kuelewesha vizuri, mimi ni mkatoliki lakini tujaribu kuwaza tofauti na Kwa legend kama wewe sikutarajia ujibu hivo sema nakuheshimu tu
 
Nitake radhi unatakiwa ujibu Kwa kuelewesha vizuri, mimi ni mkatoliki lakini tujaribu kuwaza tofauti na Kwa legend kama wewe sikutarajia ujibu hivo sema nakuheshimu tu
Unaona unavyozidi kuyaboronga! kwani katoliki sio dini..? mi nazungumzia hizo dini sidhani hata kama umenielewa! kaa ufikiri vizuri hatupaswi kufikiria hii mi dini si kitu kwetu hayana pakutupeleka yanadumaza fikra tu! fungukeni waafrika hizo dini zinawafanya muwe watumwa tu kila kukicha!.
 
Back
Top Bottom