Kwanini Wadada wanapenda Wanaume wasafi/smart?

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Nakumbuka 2010 pale Sinza kwa Remmy nilitokea kukutana na binti mrembo aliitwa Nusra. Aisee alikuwa mzuri haswa. Nilijikuta tu napata ujasiri wa kumkaribia na kumsalimu;

"Dada mambo vipi? Naitwa Jumong, wewe waitwa nani?" Akanijibu naitwa Nusra. Tuliongea mawili matatu akaondoka tukaplan kukutana after siku 3. Yes, niliamua kujipanga. Nikatungua suruali yangu ya kitambaa, pana kama kitambaa cha mashine huku nimevaa shati aina ya dogidogi, mikono kama kengere ya bomani. Chini nilivaa tafubuti za Fubu.

Siku ya tukio binti alipendeza haswaa ila hakukaa japo nusu saa na hata soda moja hakumaliza! Nilijitahidi kutia story nzuri ila wapi! Duh, niliumia sana! Siku nilipomtafuta kwa simu na kumuuliza why alinijibu kifupi tu, "nenda kajifunze namna ya kuvaa kwa wasabato wa mjini." hewala, kumbe siku ile mavazi ndo yalizingua?

Aisee, nakumbuka nilitumia karibu 70% ya mshahara kubadili style ya mavazi next month.

Brothers!
Mavazi nadhifu ni dawa ya mengi. Kuvaa nadhifu huficha umasikini na hukoleza mahusiano. I feel so comfortable katika uvaaji wangu nadhifu sasa! Hata kama unakipato kidogo, nunua mtumba, nenda kwa fundi wa mjini akutengenezee vazi la kisasa.

Sina hakika na sikumbuki nini kilitokea baada ya mabadiliko yangu kwa Nusra.

Popote ulipo Nusra, you were the cause of my looking smart!
a5ee6cb3120a5267bb46296ee24c75af.jpg
736feff4b8f1fa4faf67265107a85ccf.jpg
d11179e278d5ae67f6fa841bc39d6109.jpg
52ca073606b05afa9c14125c21e9d8cf.jpg
79791bf06f78b631a78ee87d18795526.jpg
 
Hahahahaha............ hii maneno "nimevaa shati aina ya dogidogi, mikono kama kengere ya bomani. Chini nilivaa tafubuti za Fubu" Nusura nionekane kichaa kwa kucheka mwenyewe
 
Tatizo kuwa smart ni gharama na inafuatana nna mazingira unayoishi...kama wew mda wote unashika oil itakuchosha
 
duh, ongesa na utumiaji wa lugha vizuri hilo ndo la muhimu sana..
 
You always have to look smart brother.

Always look good, feel good.

Unadhifu huwavutia wanawake wengi kama sio wote.

Hakuna mwqnamke anataka kua na mtu mchafu mchafu na asie jijali.
 
Kuna mtu anapenda uchafu kweli!!!
Macho ndio huanza kuvutika then mengine ufuata. Awe smart kimuonekano na kumkichwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom