Kwanini wachawi hawana maendeleo?

Kwanini wachawi hawana maendeleo?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,671
Hawana pesa, Mali, wala vitu vya thamani.
Utasikia fulani ana misukulie inamlimia, lakini hutomuona huyo mchawi akipata mavuno ya ziada ya kuweza kuuza na kuongeza kipato.
Watoto wa wachawi hawana afya, na maendeleo yao shuleni huwa yako chini sana.
Je ni nini faida ya kuwa mchawi?
FaizaFoxy
MziziMkavu, Mtu mzito, mshana jr, na jichawi mnipe majibu
 
Maendeleo yanapatikana kwa kushirikiana na watu kuwa karibu na watu kunafanya upate mawazo na dili mbali mbali ukiwa mchawi huwezi kufanya hayo kwasababu ya roho mbaya na sahau kuhusu kupata maendeleo
 
Hapa nategemea jibu zuri zaidi toka kwa watafiti na wachawi wenyewe.
 
Kama umekusudia wachawi wa afrika na nchi za kimaskini sawa. Lakini nchi za Ulaya wapo na wana hela sana. Mfano muigizani comedy wa kiafrika huvaa matambara. Lakini wa first world wao huvaa vizuri tu. Sababu wachawi wa afrika wengi hufanya kwa kudhuru watu. Na ulaya hufanya kwa kuangalia nyota yako tu.[emoji111]



Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Uchawi maana yake ni UJIMA, (Rejea Kamusi ya kiswahili kupata maana)

Huwezi kuuliza swali, ni kwa nini mtoto Mchanga hatembei...!!

Wachawi ni watu wa kwanza na wa pekee, wanao zingatia MIIKO ya Kazi/Fani yao..

Usitake MCHAWI afanane na kuwa na maisha sawa na Mfanyakazi au Wafanya biashara Mafisadi..!
 
mbona nasikia wakinga wametajirika na huo huo uchawi? au kuna aina zake?
 
mbona nasikia wakinga wametajirika na huo huo uchawi? au kuna aina zake?
Usije ikawa unamfananisha MGANGA ama yule anae kwenda kupata TIBA kwa Mganga na Mchawi.

Yaani huwezi Kuongelea mafanikio ya Daktari, ukazungumzia Mafanikio ya Mbu kwa kumsababishia Mgonjwa Maleria, kisha ukazungumzia mafanikio ya dawa ilivyo mpona Mgonjwa..! DMS (doesn't make sense)
 
Back
Top Bottom