Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 552
- 1,800
Wengi wetu huamini sisi (Waafrika) ni dhaifu na bila mzungu tungekuwa bado tunavaa majani, binafsi sikubaliana na hili. Labda niwakumbushe, katika zama zote za binadamu wa kale alikuwa akipiga hatua kutoka moja kwenda nyingine, na wakati mkoloni anafika Afrika alitukuta tumeshahama kutoka zama za kuishi porini tukila mizizi na matunda kwenda katika kilimo na ufugaji na mbali zaidi tulikuwa na tawala zetu.
Kitu kingine ni mfumo wa elimu, tumecopy elimu ya kikoloni ambayo zaidi inaelezea mapungufu ya mtu mweusi kuliko maendeleo ya mtu mweusi kabla ya ukoloni. Naamini kabisa hata asingekuja mzungu bado tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana, walichokosea wazee wetu ni kuacha maendeleo yao na kubweteka kusubiri mkoloni akuletee kisha yeye achukue mali zetu. Hii ndio inaendelea hadi ulimwengu wa sasa, tumewekeza kwenye ajira (kama lengo kuu) kuliko kwenye tafiti na uvumbuzi.
Wapo wanaoamini kila kitu amegundua mzungu, tunaamini hivyo kwasababu hatupendi kujifunza kuhusu tulipotoka ila tunaamini kile kilichoandikwa na mzungu zaidi, mf. tuliaminishwa (shuleni) kuwa mtu wa kwanza kuuona mlima Kilimanjaro alikuwa Johannes Rebmann wakati amekuta watu wakiishi na kuwinda hapo. Japokuwa sasaivi wamebadili badala ya kusema “mtu wa kwanza kuvumbua mlima Kilimanjaro” wanasema “mzungu wa kwanza kuvumbua mlima Kilimanjaro”. Hii ni inanikumbusha scnene ya movie ya Malcolm X akijadili dictionary ya kale katika tafsiri ya maneno “white” and “black”
White: (whit), adj. Of the color of pure snow;
reflecting all the rays of the spectrum. The
opposite of black, hence free from spot or
blemish; innocent, pure, without evil intent,
harmless. Honest, square-dealing, honorable.
Black: (blak), adj. Destitute of light, devoid
of color, enveloped in darkness. Hence, utterly
dismal or gloomy, as the future looked black.
Soiled with dirt, foul; sullen, hostile,
forbidding -- as a black day. Foully or
outrageously wicked, as black cruelty.
Indicating disgrace, dishonor or culpability.
Mfumo wetu wa elimu umetuandaa kuona mzungu ni bora kuliko mtu mweusi, ndomana hata leo hii watani zangu wasukuma wanatoa ng’ombe nyingi kwa binti mweupe kuliko yule mweusi, na si ajabu kuona dada zetu wanavyohangaika kujichubua na kuweka dawa nywele zao bila kujali wanadhurika kwa kiasi gani.
Sio kwamba kwasababu natumia simu kutoka ulaya, computer, gari n.k basi ndio nionekane dhaifu, wakati mwingine ni kwasababu tunakosa fursa na si kwamba hatuna akili. Fikiria mwanzoni Amerika mtu mweusi hakuruhusiwa kusoma, kumiliki ardhi hata kushiriki michezo kitaifa na kimataifa lakini bado alipopata fursa hiyo alifanya vizuri sana japokuwa ilibidi uwe na uwezo mara kumi zaidi ya mzungu ili ushinde maana ukiwa na ushindi mwepesi ilikuwa ni rahisi kupindua matokeo. Kuna ambao walisingiziwa kesi za mauaji ili wasichukue ushindi mf. mwana masumbwi Rubin "Hurricane" Carter (1937-2014) alisingiziwa kesi ya mauaji na alikaa jela kwa miaka 20 hadi alipokuja kuachiwa na ikagundulika alionewa.
Kuna wavumbuzi wengi sana wa Kiafrika ambao wengi hatuwajui na inawezekana kuna baadhi ya vitu tunaviona tunaamini vimevumbuliwa na wazungu.
Leo naorodhesha vitu vichache vilivyovumbuliwa na mtu mweusi (Black American):

- Improved Ironing Board, Invented by Sarah Boone in 1892
- Home Security System, Co-Invented by Mary Van Brittan Brown in 1966
- The Three-Light Traffic Light, Invented by Garrett Morgan in 1923
- Refrigerated Trucks, Invented by Frederick McKinley Jones in 1940
- Automatic Elevator Doors, Invented by Alexander Miles in 1887
- Electret Microphone, Co-Invented by James E. West in 1964
- Carbon Light Bulb Filament, Invented by Lewis Latimer in 1881
- Color IBM PC Monitor and Gigahertz Chip, Co-Invented by Mark Dean c. 1980 and 1999