Kwanini wa zanzibar wana jeuri dhidi ya bara?

Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
180
Wadau najaribu kujiuliza sipati jibu kwanini wazenji wana jeuri na kiburi sana mbele ya serikali ya bara?kwanini wanajiamini kuliko sisi wa bara?kila wanachotaka wao wanapewa?
 
Zanzibar ni nchi, na katiba yao inaanza hivyo, hapa awali ilikuwa inaanza Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini katika kumkomesha Pinda alipodhubutu kusema Zanzibar si nchi basi neno Tanzania wakaliondoa katika presentetion ta mwanzo kwenye katiba yao, si unaona Pinda hajatia mguu Zenji? anaogopa, Mwenzake Lowassa yeye mkali alikuwa anaenda kila mwezi kuwaonyesha kuwa na huko ana mamlaka akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, kwa hiyo uwoga wa viongozi wa Tanganyika ndio chanzo cha Zanzibar kuifanya Tanganyika Shamba la Bibi, angalia Mawaziri wao bara wanafanya nini? adanganywe nani? Serikali nzima ya nchi ya Zanzibar yenye Majeshi kamili na tiifu tu kwa Rais wa Zanzibar, tunajidanganya, Zanzibar ndio mabosi wa Bara.
Rais wa Zanzibar yupo Uturuki na serikali yake kufunga mikataba ya siri, hata mara moja hajaitaja Tanzania, anasema Zanzibar iko mashariki ya bara la Africa. Zanzibar watawanyonya Tanganyika kisha waitupa wao wakiwa kama Dubai na Haiko mbali, mahoteli yaliyoko beach za Zanzibar hamna hata Kenya, hiyo ni kwa kazi wanaifanya Mabalozi wazanzibari nje waliotumwa na Wizara ya Muungano, wao wanaitangaza Zanzibar tu
 
halafu wawekezaji wakifika Zanzibar hata kusikia kama kuna kitu kinaitwa Tanzania hawasikii, na wamepata wawekezaji wa kila aina, ndege kubwa za Ulaya zinatua Zanzibar kila siku na watalii watupu, sio hizi za Dar za kubeba mahujaji toka mekka na wahindi toka Delhi.
Beach za Dar kuna vijikampuni vya kienyeji, nenda Beach za Zanzibar, Watalii walioko kwa Hoteli moja Zanzibar ni sawa na wanoingua Bara kwa mwaka. usicheze wamepiga hatua, sasa bara ni mzigo tu kwao, na mnaogopa kuwaambia lolote, sasa wao wanawachezea kwa vidole....
 
Zanzibar si nchi,hakuna nchi kama hiyo Duniani, kwenye orodha ya umoja wa mataifa na Rais wa Zanzibar hajawahi kuhudhuria vikao vya UN hivyo waache wajifariji
 
Wakuu.
Kwa kipindi kirefu tumedanganywa na kudanganyika kuwa Tanzania ni nchi moja. Na sasa tunajidangaya kuamini kuwa tutaweza kuleta serikali moja.
"Baba wa taifa",Muasisi na mlindaji mkuu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania), Nyerere anasema hivi,

"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili." Uk 11

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Tujiulize, je jumuiya ya Afrika Mashariki imeundwa upya?
Je tunategemea kuwa na Shirikisho la Afrika Mashariki? Umesikia fast track process?

Soma uk 109.
http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27

Eastern African Centre for Constitutional Development - Document Details | Aii.Shirikisho Ndani ya Shirikisho:Uzoefu wa Muungano wa Tanzania by F. Jjuuko & G. Muriuki. Swahili
 
Serikali inatambua kuna baadhi ya vitu inavifanya kinyume na mkataba wa muungano,na ndiyo maana ianakaa kimya sana ila kwa ujeuri hawana ujeuri wowote hawa ni mbwembwe tuu.
 
Wadau najaribu kujiuliza sipati jibu kwanini wazenji wana jeuri na kiburi sana mbele ya serikali ya bara?kwanini wanajiamini kuliko sisi wa bara?kila wanachotaka wao wanapewa?

Mke kakalia mume kichwani hehehe, ndo mnashutuka bana?
 
zanziba ni nchi wacha na tanganyika iwe nchi, kisha tuingie kwenye EA
 
Ufahamu kuna kitu kimoja, sisi ndo tunaonekana tunautaka sana Muungano kulliko wenzetu, sasa matokeo yake ndo haya, kwamnba kila watakachukuwa wanakitaka wanapewa ili wasichomoke.Sawa na mke ambae umeonyesha unampenda sana kiasi kwamba anakudengulia kila kukicha, mara nataka hiki mara kile ili mradi tu akuone utakavyoreact.Ki ukweli mimi binafsi natamani sana Tanganyika yetu, nchi kubwa imemezwa na visiwa ndugu zangu kiasi kwamba hatuhemi kabisa,wenzetu wanajiunga na makundi mbalimbali sisi tumebaki kama kuku wa mdondo, we hav to work up and cry for our TANGANYIKA kwenye mchakato wa katiba mpya la sivyo hawa jamaa watatupelekesha ile mbaya.
 
Napita tu hapa kama njia!nachofahamu zenji cyo nchi,bali kisiwa kilichoko Tz
 
Napita tu hapa kama njia!nachofahamu zenji cyo nchi,bali kisiwa kilichoko Tz

Kisiwa chenu ni Ukerewe na Mafia n.k, Zanzibar ni nchi,

Katiba ya Zanzibar ya 1984 inasema;

(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …

(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:

(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.

(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.

(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…

(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…

Upoo mkuu?
 
Wadau najaribu kujiuliza sipati jibu kwanini wazenji wana jeuri na kiburi sana mbele ya serikali ya bara?kwanini wanajiamini kuliko sisi wa bara?kila wanachotaka wao wanapewa?

Kama unataka kufahamu kwanini vyote wanavyoviomba wanapewa ni kwa sababu Zanzibar ni nchi inayoweza kujitegemea sana bila Muungano. Hivyo serikali ya Muungano lazima itimize matakwa yao kwani yote wanayoomba wanaweza kuyapata nje ya Muungano. Kwa maana ukiwacha watafute wenyewe maana yake ni Muungano utakua kwishne.
 
Zanzibar si nchi,hakuna nchi kama hiyo Duniani, kwenye orodha ya umoja wa mataifa na Rais wa Zanzibar hajawahi kuhudhuria vikao vya UN hivyo waache wajifariji

Naomba unisaidie ufahamu zaidi hivi nchi zote duniani ni wanachma wa UN?
 
Lakini mi naona kuwa Zanzibar ndio inayoongoza Serikali ya kwa asilimia 100, na inaiongoza Tanganyika kwa asilimia 50, sasa watake nini? watulie wakunje kwanza ilihali mabibi wa Tanganyika wamelala fofofo! kwani Mawaziri wa Kizanzibari waliopo katika serikali ya Muungano unafikiri wapo kwa maslahi ya Tanganyika? hebu chunguza halafu niambie, pia mabalozi wa Tanzania wanaotokea Znz nje, na ndio wanaomwaga wawekezaji wa Kizungu zanzibar, kuna kipindi watalii ni wengi kuliko raia Zenji. Tanganyika ilijaribishwa kidole ikazama, sasa muda wowote Zanzibar itafanya kweli, kwanza wameshatajirika sana.... pole watanganyika!
 
sasa tuanzeni rasmi harakati za kudai taifa letu, tudai historia yetu, tudai jina letu na tunadai uhuru wetu
 
Lakini mi naona kuwa Zanzibar ndio inayoongoza Serikali ya kwa asilimia 100, na inaiongoza Tanganyika kwa asilimia 50, sasa watake nini? watulie wakunje kwanza ilihali mabibi wa Tanganyika wamelala fofofo! kwani Mawaziri wa Kizanzibari waliopo katika serikali ya Muungano unafikiri wapo kwa maslahi ya Tanganyika? hebu chunguza halafu niambie, pia mabalozi wa Tanzania wanaotokea Znz nje, na ndio wanaomwaga wawekezaji wa Kizungu zanzibar, kuna kipindi watalii ni wengi kuliko raia Zenji. Tanganyika ilijaribishwa kidole ikazama, sasa muda wowote Zanzibar itafanya kweli, kwanza wameshatajirika sana.... pole watanganyika!

Hapo kwenye red bado sijaelewa. Wametajirika sana akina nani? Waitaliano wenye mahoteli au wazanzibari wapagazi? hahahahahah
 
Back
Top Bottom