Kwanini Viongozi wetu wa Kisiasa hawaombi msamaha wanapokosea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Viongozi wetu wa Kisiasa hawaombi msamaha wanapokosea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Jun 26, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Katika Nchi yetu Viongozi wetu wa kisiasa wamekuwa wagumu sana kuomba msamaha wanapokosea,sababu ni nini?Mfano tu,Waziri anajibu swali la mbunge kwa kusema "na wewe tafuta hoja nyingine",kuna vitisho mbalimbali katika uchaguzi n.k. wana JF mnafahamu zingine,Je ni mazingira ya siasa za Tanzania ndio imewalea hivyo au tatizo ni sheria zilizopo?
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa ni wakati muafaka wa kuweka utaratibu wa kuwafanya wanasiasa wetu wawaheshimu waliowaweka kwenye nafasi walizonazo.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nani kakwambia wanakosea? Kuomba msamaha inabidi ukubali kwamba umekosea kwanza.

  Amani karume alishasema hatuna utamaduni wa kukosoana na kukubali kukosea.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..kwasababu wa-Tanzania tunapenda viongozi waongo-waongo.

  ..wakituambia ukweli kwa kukiri makosa na mapungufu yao wanaweza kukosa kura.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna viongozi wa kisiasa na Viongozi wa Serikali ,kiongozi wa kisiasa ni lazima awe mbishi au mwenye kupinga na kujua mbinu za kuzima na kutuliza ila kiongozi wa serikali anatakiwa kuwa mkweli na mwenye kuwajibika na uwongo kwake ni mwiko halikazalika kukwepa kujibu ni kushindwa katika fani ya cheo alichonacho katika serikali na anakuwa hafai.
  Hivyo ukiona kuna viongozi wa aina hiyo ya kuzima na kukwepa basi inatakiwa kwa haraka umuelewe kuwa huyo si kiongozi bali ni kihio tena mbabaishaji tu hafai kuwepo madarakani katika serikali.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa Kikwete ni kiongozi wa kisiasa au kiserikali? Na kuongoza serikali ni nini kama sio siasa?
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kuna wakati nimewahi kufikiri kwamba viongozi wetu wamewahi kutumia 'bange' au mihadarati fulani ujanani mwao!

  Mtu anaposema:
  -HIVYO NI VIJISENTI TU

  -NCHI IKIKAA GIZANI TUSILAUMIANE

  -BORA WANANCHI WALE HATA NYASI ,LAKINI NDEGE YA RAIS LAZIMA INUNULIWE

  lol!
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hili ni tusi kwa watumiaji makini.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  drugs hazina watu makini!unaweza kuwa 'mmakini wa kwanza' utatumia sana lakin YOU MUST SUFFER THE CONSEQUENCES
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  labda walikunywa bange maana mambo yao ni kinyume kabisa na wavuta bange!!! tuwape muda kabla ya 2010 wataanza kutunga nyimbo za reggae sijui za kwao tutaziita nini au za kibange bange.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  You did not get the pun, my bad.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kama alivyosema Bluray.. hakuna kiongozi hata mmoja anayekubali KUFANYA makosa hasa ktk kaluli zake..Ni hulka na tabia mabyo tunayo sisi wote Watanzania..Mtanzania hawezi kuomba samahani hadi wewe mtuhumu uweze kumwonyesha USHAHIDIO wa makosa yake..na hata kama utaweza kuupata huo ushahidi bado atatafutwa Mchawi..
  Ni malezi tuliyokuwa nayo toka utototni, mtoto akiichukua kitu ndani ya nyumba bila ruksa mara zote hukataa katakata hata kama anajua kafanya hivyo kwa sababu kwanza kuna fimbo,pili familia itaondoa imani kwake..Na hata kama mtoto huyo atakamatwa na ushahidi basi atasema kapewa na mtoto fulani jirani, mdogo wake asiyejua kinachoendelea ama amekiokota..
  Tunakuwa na tabia hizi hata kama unapanda hadi darini -Phd...Ni ustaarabu wa Mdanganyika!
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni dalili ya kutostaarabika na kabla sijatupiwa kombora
  anayepingana na dai hili anathibitisha tu usahihi wake
  - watanzania si wastaarabu.
  Mstaarabu hukubali anapokosea na kuwajibika
  pindi akikosolewa na hivyo kurekebisha tabia yake.
  Kwa nini tunakosa ustaarabu?
  Asiye na ustaarabu ama huchagua lililo bovu
  au kutenda lisilokubalika - ni malezi ya CCM ?
  hakika hatuna ustaarabu.


   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu, wala hujasema Uongo..
  Ndivyo Tulivyo ina viambatanisho vingi sana..
   
 15. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Viongozi wetu hawawezi kuomba radhi hata wakikosea kwa sababu hawajui kama wanakosea au hawakosei. Wanafanya vitu kwa mazoea tu na hawana muda wa kutafakari wanayosema au kutenda. Au kama wana huo muda na wanajua wanalosema au kutenda basi unafiki umewajaa!

  Ndiyo maana kiongozi anaweza kusema kitu cha ajabu sana na watu wakakikosoa halafu baadaye akajidanganya kwa kusema wananchi hawakumwelewa na kwa ujanjaujanja akarekebisha kauli yake ili ionekane kama ndivyo alivyosema. Hili ndilo tatizo la viongozi wetu wa leo.

  Waziri Mkuu Pinda jana wakati anajaribu kumtetea Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kuhusu ufisadi alisema hapa Tanzania hapajawahi kutokea kiongozi kwa ngazi ya Rais awe fisadi!

  Yaani, alitaka kumaanisha kuwa ni watu wa kawaida tu wanaoweza kuwa mafisadi na siyo viongozi wa ngazi za juu. Lakini anasahau kuwa serikali ambazo zinajenga demokrasia ya kweli na zinazowajibika vizuri kwa wananchi wao zimekuwa mstari wa mbele hata kuwafikisha viongozi wao kwenye vyombo vya sheria kama uongozi wao ulikuwa na walakini. Yeye anataka kutuaminisha kuwa hata Tanzania hilo halipo au haliwezekani.

  Mimi nadhani mfumo wetu wa siasa ndio unaowafanya viongozi wetu wawe vipofu wa kupindukia. Wabunge wana wajibu wa kuwahoji mawaziri juu ya utendaji wao na mawaziri wanaonekana kuogopa kuhojiwa na wabunge na wakiona wanakosa majibu wanatumia lugha ya kukejeli au wanapuuza tu hoja iliyotolewa.

  Sasa wameanzisha dhana ya kuwa kila mbunge ni 'potential minister or deputy minister' ili wasikosolewe sana kwa vile hao wanaowakosoa nao wanaweza kujikuta wanashika nyadhifa hizo. Sasa mawazo kama hayo kweli yanatoka kwa watu wanaotafakari wanayosema? Mwanafalsafa mmoja alisema (nadhani ni Socrates) aliwahi kusema kuwa UNREFLECTED LIFE IS NOT WORTH LIVING!
   
 16. O

  Omseza Mkulu Member

  #16
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii ni kawaida, hata wewe au hao walio madarakani wakitoka watakuwa wepesi kulalamika na kyaona kama uonavyo.

  Ndg MWIBA amejaribu kutoa tofauti kubwa kati ya viongozi wa kisiasa na Serilali kwa hiyo hata majibu yao yanabidi yawe na utofauti.
  Kama unasawsikia baadhi ya wabunge wanao lalamika baadahi yao waliwahi kuwa viongozi lakini hawakakuyaona mabaya.
  Mf ni mbunge mzooefu kutoka RUKWA: alijulikana kwa hoja ambazo zilipelekea mawaziri miaka ya nyuma kuachia madaraka, lakini kwa sasa anaonekana kufanya yale yale kwa sababu yupo katika kundi liliofaidika na ufisadi ktk sekta mbali2!
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hakuna kiongozi au serikali inayo kubali makosa moja kwa moja. Siku ukisikia mwanasiasa akisema directly nimekosa ujue kabanwa mbavu sana lakini mara nyingi wata jaribu kuspin mambo. Mara nyingi kiongozi akikubali makosa it's political suicide because he/she goes on record saying kitu fulani nilikosema na mimi mwenyewe nakubali. Na hivi ndivyo ilivyo kwa wanasiasa wote si wa Tanzania tu.
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawa Viongozi wanaonekana kama vile Miungu watu vile, Na pia Katiba yetu ndio inachangia kufanya kiburi chao. Dawa yao kuchagua watu wengine na sio Viongozi wabovu kama Hawa waliopo leo katika Madaraka ya utawala huu. na ndio maana wanakuwa na
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inaonekana una matatizo ya kuelewa kina cha maelezo ,kwa ilivyo unapokuwa Raisi wa Nchi unakuwa ni kiongozi wa watu wote ,Hivyo huwezi kutumia cheo hicho kisiasa ndipo pale unaposikia watu wakihoji Ziara ya Kikwete kule Pemba na Unguja ilikuwa ya serikali au Chama ,kwa kuwa alishindwa kutenganisha Cheo chake kama Raisi wa watu wote na kujivalisha koti la UCCM ndipo alipoonekana kuwa amefanya ziara kama Mwanachama wa CCM,na alipojibiwa matusi yake ya kuwaita wapinzani kuwa ni walevi wa gongo alijibiwa kama ni mwanachama wa CCM na sio Raisi wa Nchi.Kama utapitia majibu ya Maalim Seif Sharif Hamadi utaona ni jinsi gani Kikwete alivyowekwa sawa.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ili mtu aombe msamaha kwanza ni lazima atambue kosa na kuwa amelitenda kosa hilo. Watawala wetu hawajui wapi wamefanya makosa na hivyo hawako tayari kuomba msamaha kwa vitu ambavyo hawajui ni makosa; lakini zaidi, nani amesema wanakosea?
   
Loading...