Kwanini Viongozi wengi hawajibu jumbe za watu?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,252
Reaction score
2,001
Habari Wakuu.

Nauliza kwa nia njema, kwa heshima na kwa kutambua ugumu wa majukumu ya uongozi,
Kwanini viongozi wengi hawajibu SMS za watu?

Sijafika kulalamika, bali nataka kuelewa. Mara kadhaa nimejaribu kutuma ujumbe kwa kiongozi fulani sio wa matusi, sio wa kutaka fadhila, bali ujumbe wa ushauri au hata kuuliza jambo la msingi kuhusu jamii yetu. Hakujibu. Nilipojaribu tena kwa mwingine jibu lilikuwa kimya kingine.

Naelewa ratiba ni nyingi, changamoto ni nyingi, na wingi wa ujumbe unaweza kuwa mkubwa sana. Lakini huu ukimya unawasaidia au unawazidishia umbali na wananchi? Je, wapo wanaopokea ujumbe kwa niaba yao? Au tumaini letu linapotelea hewani bila kufikishwa?

Najua viongozi wetu ni watu wa maono makubwa wenye dhamira njema ya kuliona taifa likisonga mbele. Lakini je, kuna nafasi ya kuwa na njia rasmi ya kupokea na kuchambua ujumbe wa wananchi? Maana wakati mwingine ujumbe mmoja unaweza kuwa kilio cha watu mia na kujibu mmoja tu kunaweza kuwa faraja kwa wengi.

Nauliza kwa sababu naamini kuwa kusikiliza ni sehemu ya uongozi. Kujibu si lazima iwe kila mmoja, kila wakati ila kuwe na mfumo kuwe na ishara kwamba sauti zetu zinasikika. Hata kama hatupati jibu moja kwa moja.

Ninaamini tunaweza kuwa na Afrika ya viongozi wanaosikiliza, wanaojibu, na wanaowajali watu wao hata kupitia ujumbe mdogo tu wa maandishi.

Ni tafakari tu,
Kutoka kwa mwananchi wa kawaida anayeamini kuwa mawasiliano ni msingi wa maendeleo.

Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Wako bize, wanaandaa mikakati ya kushinda tena majimbo yao.
 
Hawana shida na wewe.
 
Elewa viongozi wetu hawapo kwa ajili ya kuongoza taifa kwenye maendeleo, viongozi wetu wapo kwa ajili ya manufaa yao ndio maana hawahangaiki na kizalala kama wewe, sababu itakavyokuwa huwapunguzii kitu.
 
Mwandikie kuwa kuna watu wanapitapita jimboni kwake na pesa huku wakimsagia kunguni.

Asipokupigia utakuwa umekosea namba.
 
Habari Wakuu.

Nauliza kwa nia njema, kwa heshima na kwa kutambua ugumu wa majukumu ya uongozi,
Kwanini viongozi wengi hawajibu SMS za watu?

Sijafika kulalamika, bali nataka kuelewa. Mara kadhaa nimejaribu kutuma ujumbe kwa kiongozi fulani sio wa matusi, sio wa kutaka fadhila, bali ujumbe wa ushauri au hata kuuliza jambo la msingi kuhusu jamii yetu. Hakujibu. Nilipojaribu tena kwa mwingine jibu lilikuwa kimya kingine.

Naelewa ratiba ni nyingi, changamoto ni nyingi, na wingi wa ujumbe unaweza kuwa mkubwa sana. Lakini huu ukimya unawasaidia au unawazidishia umbali na wananchi? Je, wapo wanaopokea ujumbe kwa niaba yao? Au tumaini letu linapotelea hewani bila kufikishwa?

Najua viongozi wetu ni watu wa maono makubwa wenye dhamira njema ya kuliona taifa likisonga mbele. Lakini je, kuna nafasi ya kuwa na njia rasmi ya kupokea na kuchambua ujumbe wa wananchi? Maana wakati mwingine ujumbe mmoja unaweza kuwa kilio cha watu mia na kujibu mmoja tu kunaweza kuwa faraja kwa wengi.

Nauliza kwa sababu naamini kuwa kusikiliza ni sehemu ya uongozi. Kujibu si lazima iwe kila mmoja, kila wakati ila kuwe na mfumo kuwe na ishara kwamba sauti zetu zinasikika. Hata kama hatupati jibu moja kwa moja.

Ninaamini tunaweza kuwa na Afrika ya viongozi wanaosikiliza, wanaojibu, na wanaowajali watu wao hata kupitia ujumbe mdogo tu wa maandishi.

Ni tafakari tu,
Kutoka kwa mwananchi wa kawaida anayeamini kuwa mawasiliano ni msingi wa maendeleo.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Ni ego tu. Kuna kajamaa kamoja kabla hakajapata shavu la unaibu waziri aliwahi kuwa mkuu wa idara sehemu fulani nikifanya kazi chini yake sasa basi kipindi fulani nikapata shida ambayo ilikuwa ni uonevu na swala lilikuwa katika wizara yake ebana nikiamini huyu mtu anaweza nisaidia nikamtumia ujumbe kawaida na wasap pia. Nikamtumia na kwa email yake ya kazi nikiambatanisha na vielelezo. Ila ajabu kwenye wasap ali blue tick tu akakaa kimya.

Ikanibidi nitafute mawasiliano ya juu zaidi nikapata mawasiliano ya waziri, aisee yule mama Mungu ambariki sana alichelewa kunijibu hadi jioni yake na baada ya hapo hazikupita siku mbili nikapata haki yangu.

Kwaiyo hilo swala huwa ni ego tu za mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom