Kwanini vijana wa SUA hawana ajira?

Kwanini vijana wa SUA hawana ajira?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,475
Reaction score
33,038
Hello JF...

Leo nauliza kwa nini wanafunzi wa SUA hawana ajira.???

Wenzetu mtu mwenye degree ni mtu mwenye uhakika na ajira...

Kwa nini serikali isijenge vyuo vingi vya Kilimo watu wasome...

Watu kuanzia waliomaliza darasa la saba mpakla form six waliofeli waingie kwenye hivyo vyuo wasome kilimo...

Watu waliograduate SUA ndio wafundishe kwenye hivyo vyuo after teacher training...

At least wanajua nadharia na vitendo...

Sijui cohort iliyopelekwa israel kusoma kilimo ilikuwa ni watu wa characteristics gani...

ila mimi ningependa kuona watu waliograduate SUA ndio waende huko...

Wenyewe ndio wako capable kusoma...kumchukua kijana out of bush kusoma ni kumuonea....they are not mentally ready...

Vijana wa SUA sio waende mashambani huko kusoma vitu ambavyo havitusaidi wakasome Agriculture trending courses kama the use of technolohgy to improve agricultrure proccess, data analytics in agriculture, Agribusiness management

Labda mtasema tutakuwa saturated na wakulima, ila kukiwa na researchers wa kubaini tulime nini tuuze wapi sijui kama kutakuwa na tatizo....

Nasema hivi sababu kuuza resources zetu kama bandari while tuna large untapped resource (Land) ni Plain stupidity!

onLY 33%of our arable land has been used, tuki optimize matumizi yake lazima tutamove foward...

Halafu serikali iwe inatoa credibility kama inatoa mawazo huku sio kulaumu tu

Haya wana JF nimepuyanga au?
 
Licha ya umuhimu wake, kilimo kinadharaulika na kuchukuliwa poa na watu waliowengi huwaona wakulima kama watu waliofeli maisha!

SUA Kozi zake zinaushindani sana, wanaozisoma ni wengi kulinganisha na ajira zilizopo.

BSc Veterinary Medicine
BSc Biotech & Lab science
BSc Aquaculture
BSc Forestry
BSc Agri'engineering
BSc Agribusiness

Wanasoma wengi nafasi za ajira chache!

1. Serikali ifanye namna viwanda hasa vinavyoendana na kilimo viongezeke, itapanua wigo wa ajira kwa wahitimu, pia itaongeza soko kwa wakulima/wahitimu waliojiajiri katika kilimo.

2. Ihamasishe uwekezaji katika kilimo-biashara, hasa wawekezaji wa ndani.

3. Sekta ya uvuvi iendelezwe, ni kama imekufa kabisa. Tanzania kuna primitive fishing. Wahitimu wa aquaculture wanaishia kuwa bodaboda.
 
Wazo zuri saana ni uboreshwaji wa wazo ndiyo unatakiwa tu.

Mfano: Baadhi ya nchi hasa za Asia, Africa zipo chache ukiingia kwenye kilimo unaomba mkopo kama business plan yako ikipita unapewa mkopo na unatafutiwa aridhi. Marudisho unarudisha tu asilimia 50.

Kwa biashara na wakandarasi hivyo hivyo. Wakandarasi wanapewa mikopo rafiki na usimamizi wa kitaalam.

Tuseme kama tumewapa wakandarasi 100 wa kitanzania 40 wakaanguka 60 wakanyanyuka hatujapoteza kitu. Bado pesa zinazunguka Tanzania.

Hatuna utamaduni wa kuwezeshana. Wanasiasa na wananchi tupo busy kujadili petty issues.

Binafsi ningeulizwa kipaumbele chetu kingekuwa nini ningesema kupigia kelele wanasiasa wawawezeshe wananchi hasa kwenye uzalishaji na uchakataji wa bidhaa.

Tumwage pesa kwa wananchi wenye uthubutu..tusisubiri waanguke kisha tuwalaumu...tuwape mitaji na wataalamu wa kufanya nao kazi.

Wachina walianza hivi... wengi walio na miaka 15 hadi 20 Africa ukiwauliza wanakuambia serikali ilifadhili kiwanda cha nguo kisha zilipozalishwa nyingi wakakusanya wajasiriamali wakawapa mitumba na pesa kidogo wakawaleta Africa kwa jina la wawekezaji.

Leo hawa Wachina wamejazana kuanzia Nigeria hadi South Africa na ndiyo wametawala kwenye maduka ya nguo.
 
Hao vijana walio pelekwa israel unajua walipo ? Ngoja nikwambie walipo hamna mwenye ajira baadhi wali pelekwa kwenye mradi wa BBT (wa bashe) ambao ume telekezwa una jifia tu uko dodoma maana likua ni project ya kupiga pesa tu na wahuni washa piga tayari.

Wengine wako mtaani baada ya kuhaidiwa wataitwa hadi leo bila bila ,kumbuka wali hakikishiwa ajira serikalini moja kwa moja wakirudi
 
Nimependa contribution yako mkuu, watu wakipewa ardhi kwa mrejesho wa 50% itawa encourage kuchukua ardhi, na wakipewa mentorship kwenye hii miradi kufeli kutakuwa kidogo...
 
Kijanaa nimeamua kulima eka Tano za bamiaa ,nakujaa sokoni nakuta wananunua sado mia mbili,wakati mwezi uliopita sado ulikuwa buku

Haki kilimo nipata poteaa,nimerudii zangu mjini kuendelea kuchomelea vyumaa na bamiaa nimesusaa shamban🙌
Pole mkuu, hakuna uwajibikaji kwa serikali ndio tatizo...kwa mfano kungekuwa na wataalamu wanasema limeni hiki kwa sasa, usingelima bamia na kuangukia pua mkuu....sijui ukweli tatizo liko wapi mkuu...
 
Hao vijana walio pelekwa israel unajua walipo ? Ngoja nikwambie walipo hamna mwenye ajira baadhi wali pelekwa kwenye mradi wa BBT (wa bashe) ambao ume telekezwa una jifia tu uko dodoma maana likua ni project ya kupiga pesa tu na wahuni washa piga tayari.

Wengine wako mtaani baada ya kuhaidiwa wataitwa hadi leo bila bila ,kumbuka wali hakikishiwa ajira serikalini moja kwa moja wakirudi
Ufisadi ni janga ambalo linawa affect vijana na nguvu kazi ya kesho, nichagueni mimi kuwa Rais nifanye reforms LOL
 
Kijanaa nimeamua kulima eka Tano za bamiaa ,nakujaa sokoni nakuta wananunua sado mia mbili,wakati mwezi uliopita sado ulikuwa buku

Haki kilimo nipata poteaa,nimerudii zangu mjini kuendelea kuchomelea vyumaa na bamiaa nimesusaa shamban🙌
Poor mindset.

You have not failed you have learned ways of doing it.

Mi ni mkulima mzuri sana wa mazao ya bustani [Nyanya, Karoti, Hoho, Bamia, Pilipili, Mbogamboga, Miche ya matunda].

Mwanzo nilikitana na changamoto kubwa kuzidi hata hizo, Afadhali ulivuna - unakijua kinyaushi au unamfahamu kantangaze?

Vijana wengi hukata tamaa mapema bila kuangalia walikosea wapi, Wanataka wakifanya kitu mara moja tu kiwatoe.

Get up brother.
 
Unakumbuka lile samo la sayansi kilimo Enzi zile, lilitusaidia sana sisi vijana wa Enzi zetu.
Kama lile somo litarudi na SUA wakija wanaweza saidia pakubwa sana.
 
Back
Top Bottom