Kwanini vifurushi vingi na vya bei nafuu vipo usiku

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Habarini,mimi huwa najiuliza maswali mengi sana hivi kwanini mitandao yetu yote hapa Tanzania vifurushi vizuri na vya bei nafuu vyote vipo kuanzia usiku yaani Sa sita usiku hadi sa 12 asubuhi au kuanzia sa tano usiku hadi sa 12 asubuhi hasa hasa vifuri vya internet.

Je kuna swala lolote la kiufundi kwamba usiku MB zinazo tumika ni Chache au huwa wanafanya kwa Lengo gani?

Mfano tigo wa Hii ya kustream video youtube bure,na mitandao mingine ndo wanaofa nzuri usiku,na usiku mtu anakuwa ametulia ana mda mzuri wa kutumia internet kuliko mchana

KwaninI Jamani
 
Mimi hizi ofa za mitandao ya simu huwa zinanifurahishaga sana. Eti ongea bure kuanzia saa sita usiku. Hahahahaha
 
speed za mitandao ya simu ni shared yaani mnagawana watumiaji, hivyo wakiacha mchana watu watumie sana ujue mtandao utakuwa slow hata msg ya whatsapp kutuma inakuwa kazi.
 
Wana JF wenzangu tupeane Info kwa siku za hv karibuni ni mtandano gani unatoa ile Ofa ya Vifurushi vya Night Pack,Airtel walikuwa na Usiku Pack tsh 1500/= Kwa Gb 15 siku hizi hakuna.TTCL walikuwa na TOBOA night pack Tsh 1000/= kwa GB 15
images.jpg
 
Hao wajinga wameona tunafaidi sana..

Alaf sijui kwanini hakuna vifurushi vya unlimited, waweke tu hata kama vitakuwa bei.
 
Back
Top Bottom