Burundi unapata GB 30 'Usiku pack' chini ya dola moja

Burundi unapata GB 30 'Usiku pack' chini ya dola moja

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,770
Reaction score
4,395
Kwenye harakat za 'Kusaka tonge' Nikajikuta nimedondokea nchini Burundi..Hapa nchini burundi mambo ni rahisi sana sasa napata EXPERIENCE ya ile kauli ya Waziri kuhusu kuhamia burundi kama maisha TZ yamekushinda.

Mtandao pendwa ni Lumitel na Ecotel na mingineyo..Sasa katika harakati za kutafuta bundle ndo nikakutana na hii "Usiku pack" ya burundi ni kufru!!

Kwa 4K ya huko(Faranga)ambayo ni kama buku 2 ya TZ ambayo ni chini ya dola moja za kimarekani (USD) unapata GB30 saa 6 usiku mpaka 12 asubuhi.

Screenshot_20230508-082255_1.jpg

kasi ni nzuri maeneo ya mji mkuu bujumbura(buja)kwa mujibu wa (fast.com) usiku inapepea hata (7 mbps).Najuta kwanini sikuja na PC nitoboe usiku mzima kushusha madude.!!!.Kwa wazee wa game,Movies hii inawafaa sana.

Screenshot_20230508-082242_1.jpg

Ikumbukwe Mitandao ya TZ ilisanuka na kututolea vifurushi vya GB 10 usiku pack..wanakwama sana washenzi wale.Kwasasa tabu nayopata ni kustream mpira kwa HD unaangalia mpira huku unapresha ya kufungwaa.. huku presha ya bando kuisha..Aisee kazi ipo

"Ili nalo mkalitazame"

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom