Kwanini Uwanja wa Ndege wa Bukoba ni hatarishi sana kwa marubani kutua na wanapaogopa mno?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,955
109,765
Nasikia kama kuna Kitu ambacho Marubani wengi wa Ndege nchini Tanzania hawakipendi basi ni kupangiwa route ya kwenda Kutua Uwanja wa Ndege wa Bukoba (Kagera) kwa Watani zangu na naambiwa wapo Marubani wengine Hujivunja (Hutoa Sababu za Uwongo) ili tu wakwepe na wapangiwe Wengine.

Pia kuna Mtu kaniambia kuwa pamoja na kwamba katika Uwanja wa Ndege huo kuna Kituo cha Kuongoza Ndege lakini bado hata hawa Marubani hawaamini kwakuwa wanasema Jiografia ya huo Uwanja pamoja na Hali ya Hewa ya Mvua za kila dakika zimewalazimisha Marubani wengi kuupa Jina la Utani huo Uwanja kwa kuuita Pepo ya Haraka na nasikia hata wengi Wao wakitua na kupaa Salama hapo hufanya Maombi ya Kushukuru kuliko hata Malaika wenyewe wa Mbinguni.

Kuna sababu fulani fulani za Kitaalam nimepewa na Mbobezi Mmoja wa masuala haya ya Aviation ila GENTAMYCINE kwa kujua kuwa hapa JamiiForums kuwa Mangwena (Wabobezi) zaidi nimeona hili nililete hapa hivyo nawaombeni wenye Majibu ya Kiufundi na Kiutaalam kariubuni hapa mje mtupe Darasa kwani nimeambiwa hata sababu Kuu ya ile Ndege Kutumbukia Ziwani na Kumuibua Muokoaji Feki na Msanii Majaliwa zinafanana za nilizoambiwa na moja wapo niliyoisema hapa.

Sasa nanyi Watani zangu mnajifanya mmesoma na mna Hela mbona huo Uwanja wenu unawatoeni tu Jasho 24/7?
 
Back
Top Bottom