Kwanini uuzaji wa Kitimoto hufanyika maeneo ya ufichoni?

Kuna maeneo na maeneo kwamfano huku mtwara hufanyika mafichoni maana wateja wengi ni waislam huwa hawapendi kujulikana, mtwara hihi ukienda ndanda kule kitimoto njenje kule kuna mpaka mabucha kabisa kwasababu kule wakristo ni wengi.
Natumaini hamjambo.
Kama wewe ni mdau kidogo au sana katika maswala ya ulaji ama ununuzi wa nyama ya nguruwe, basi utakua unanielewa zaidi katika uzi huu.

Hivi ni kwanini maeneo karibia yote kwa Dar hata baadhi ya mikoa mengine nyama hii pendwa huuzwa mafichoni kama magendo hivi?
Ni kwanini pia huwa hakuna mabango mazuri ya kuvutia wateja?

Karibuni wazoefu wa mambo mtuelimishe zaidi.
 
KICHAPO HEVI KWA WALA KITIMOTO...KINAKUJA ASEMA BWANA

NI SIKU YA HUKUMU/KIAMA

NYIE MNAODANGANYWA NA KINA GWAJIMA, RWAKATALE, MZEE WA UPAKO, MWAKASEGE, NA KINA PAPA KUWA MLE NGURUWE TU, MAANA WALIKATAZWA WAISRAELI TU, MTAKOMA ASEMA BWANA

ISAYA 66

15 Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.

17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.

18 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.

19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa.

20 Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.
Hembu tusitishane. Wazungu waliotuletea dini ndiyo nyama wanayoila kwa wingi.
 
Watu tunakula mpaka utumbo hiko kichapo kitawapata nyie wasabato
 
Uchunguzi usio rasmi , ni kweli nyama hii au mnyama huyu, analiwa maeneo tulivu, yasiyo na bughudha.

Sababu, mnyama huyu au nyama hii, huliwa sana na Wakristo walio na ndugu, Jirani na marafiki ambao ni Waislamu.

Sifa ya Mkristo ni kumheshimu MTU Wa imani nyingine , ndo maana miaka ya nyuma nyama hii iliitwa MKUU WA MEZA.

Kilichoharibu ni MIHADHARA ya Dini , wale wahadhiri Wa mwanzo Wa Kiislamu walipokuwa wakihubiri waliitaja nyama hii na Ukristo kuwa ni ukafir na haramu.

Wale wahadhiri Wa Kikristo wakijiita BIBLIA NI JIBU wakajibu mapigo na kuwaaminisha WAKRISTO nyama hiyo ni HALALI mkiila kwa kujificha ni sawa na kukubaliana na hoja za Waislamu.

Kula hadharani jivune na imani yako, ndipo ile staha ,ilipoanza kutoweka na kuibuka kwa mabucha na maeneo ya wazi ya kuuza nyama hiyo kiasi neno MKUU WA MEZA likatoweka .

Sasa majina kibao, Mbuzi Katoliki,Noah. Kitimoto, nk

Kuna sehemu barabarani niliona Tangazo " Kula kitimoto safi, mpaka ng'ombe aone wivu"
Mkuu wa meza
 
Babaangu mdogo alikuwa anapasifia mnoo, kuwa kitimoto chao kizuri sana...duuh ndo nikaenda na kampani yangu, kuletwa na kuanza kula tukajiuliza mbona sio kizuri, nyama yenyewe ya nguruwe mzee!....si bora hata pale kumekucha toroka uje!
kudadadek
 
Si unajua wenzetu ukiweka barabarani wanaweza kuvamia biashara eti ni haramu... hukumbuki ishu ya nguruwe Magomeni walipoingilia na kuvunja butcher za nguruwe.. mpaka mwinyi akaingilia kwamba anayekula nguruwe mwache ale!
Ila waislamu wa bongo wanashida kichwani
 
Babaangu mdogo alikuwa anapasifia mnoo, kuwa kitimoto chao kizuri sana...duuh ndo nikaenda na kampani yangu, kuletwa na kuanza kula tukajiuliza mbona sio kizuri, nyama yenyewe ya nguruwe mzee!....si bora hata pale kumekucha toroka uje!
Mpeleke sinza pale Villa hutajuta
 
nguruwe ni nyama haramu kulingana na Quran takatifu na Enjili 'madhubuti' hivyo ni nyama ya wasio na dini na mkoa huu sio wa Kipagani kama Manyara na etc
 
Sina uhakika, nilipita maeneo ya barabara ya kwenda uwanja wa ndege Kigoma mjini, wanauza sehemu ya wazi kabisa mbona.
 
Arusha maeneo ya Kaloleni sarafina inn wanauza sehemu wazi tena na usafi wa hali juu, na inatengenezwa vizuri sana hawa jamaa in wataalamu sana
 
Back
Top Bottom