Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Namshukuru sana mwenyezimungu hatimaye IT leo kaposti pdf yenye jina langu. ( nimelamba asali).

Nawashukuru wataalamu wangu wote kwa sapoti yenu.

Kauli mbiu ni ileile tusikate tamaa bila shaka wadau wa huu uzi wote tutapata placement kwa idhini ya muumba.

Mwenyezimungu Awaongozeni, awabariki na azifurahishe nyoyo zenu.

Hongera sana brother
 
Wadau naomba msaada kwa ajili ya ndugu yangu ambaye majina yake yana dosari kidogo kwa herufi moja.


Chet cha kuzaliwa: Amos Agrey Mathias
Form four: Amos A Mathias
Form six: Amos A Mathias
Chuo: Amos A Mathias
NIDA: Amos Aggrey Mathias

Dosari jina la kati kati la cheti cha kuzaliwa limekosa herufi 'g' moja badala ya kuwa aggrey limeonekana agrey, je hili ni tatizo katika mchakato wa ajira? Na kama ni tatizo aanzie wapi?
Namshauri akachongeshe cheti kipya cha kuzaliwa hapo Rita.
 
Uko sahihi wengi hawawezi kushindana, mimi huwa nasema siku zote kuna taasisi kama NSSF watoa huduma wanaleta sana nyodo ni sababu hawa COMPETE hawajui ni jasho kiasi gani linatoka kufaulu written, Practical na Oral, hawajawahi kulala stand wala kupanda Lori kuhudhuria usaili kwa shuhuda za kina mfwende hapa huwezi tarajia mtu alete nyodo na dharau kazini.

Hawa NSSF and the likes wanatakiwa kufika College of informatics waandike mtihani.
📌🔨 Nakazia mkuu, ndo maana utendaji wao ni 0 Ila kwa waliotoka PSRS wanatoa huduma nzuri Sana Nina ushahidi wakutosha mkuu
 
Namshukuru sana mwenyezimungu hatimaye IT leo kaposti pdf yenye jina langu. ( nimelamba asali).

Nawashukuru wataalamu wangu wote kwa sapoti yenu.

Kauli mbiu ni ileile tusikate tamaa bila shaka wadau wa huu uzi wote tutapata placement kwa idhini ya muumba.

Mwenyezimungu Awaongozeni, awabariki na azifurahishe nyoyo zenu.
huu uzi umebarikiwa hongera sana ndugu yangu, sote tutapata kazi

dbaba hongera pia na wana wotee
sijawasahau kina donvill,marboish electrical wawakumbuke
 
  • kwenye oral unatakiwa ujiamini
  • uwe na angalau knowledge ya maswali unayoulizwa(usiende opposite kabisa na swali), mfano unaweza kuulizwa Utaje components za Financial Statement, anza kwanza kutoka definition ya hicho Kitu (financial statements) halafu uje kwenye components kutoa definition Kuna maksi zake
-
Leo umenipa kitu kikubwa sana
 
Back
Top Bottom