HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mimi ni mzazi na ninaelewa sana! Nikiwa mtumishi nililazimika kuingia kwenye mikopo ya bandika bandua ili wanangu waweze kusoma chuo. Kuna ambao hawakutoboa vizuri form 4 ikabidi niwapeleke private F5 & 6. Kwa kuwa walisoma private hawakupata mkopo loan board. Ikabidi niendelee kuwalipia kwa kuendeleza mikopo!! Wamehitimu lakini ndo hivyo tunaendelea kubanana hapa nyumbani tukikagombania hako ka-pensheni kangu!! Wawili walifanikiwa kupenya PSRS na kulamba asali! Wawili ndo bado tunabanana nao hapa nyumbani. Wawili walipata mkopo hao ikanipa unafuu. Walio[penya mmoja alipata mkopo na mmoja nilimlipia!! Waliopo nyumbani pia mmoja alikuwa na mkopo mmoja nilimlipia!!

Ila nimewaandalia plan B: Nina heka 10 huko kijijini niliwaandalia!! ikibidi wakalime hata kwa mkono kwa kuanzia!! Ila ukiwaambia habari ya kwenda kulima kijijini ni kama unawaambia habari ya kwenda jela!!
Huu uzi. umenipa moyo san, hakuna kukata tamaa
 
Back
Top Bottom