The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
1. Upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu leo umepinga kupokelewa kwa maelezo ya shahidi namba 2 wa jamhuri Afande Ramadhani Kingai na maelezo ya mshitakiwa Adamu Kusekwa kwa sababu kuu mbili;
. Yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria
. Yalichukuliwa kwa kuwatesa watuhumiwa kama njia ya kuwashurutisha kukubali tuhuma hizo!
2. Kwa sababu hiyo, ikasabanisha kesi ya msingi kusimama kuendelea kusikilizwa ili hili shauri dogo lisikilizwe na kutolewa maamuzi (trial within trial) kwa upande wa mashitaka kuthibitisha kuwa walifuata utaratibu wa kisheria au upande wa utetezi waoneshe kuwa utaratibu wa kisheria haukufuatwa.
Lengo la objection hii ni upande wa utetezi kutaka kuimaliza kesi mapema kwa kuendelea kuanika uongo wa mashitaka haya na hivyo kuithibitishia mahakama kuwa mashtaka haya ni ya HILA, UONGO na ya KUTUNGA.
Sikiliza ufafanuzi wa Mwanasheria akiliweka hili vizuri katika voice video
hiyo hapo juu...
UPDATES:
Tundu Lissu naye auchambua ushahidi wa Afande Ramadhani Kingai