Kwanini upande wa utetezi kesi ya ugaidi wa Mbowe na wenzake wame - object maelezo ya Kingai na mshitakiwa Adamu kupokelewa kama vielelezo halali?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535

1. Upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu leo umepinga kupokelewa kwa maelezo ya shahidi namba 2 wa jamhuri Afande Ramadhani Kingai na maelezo ya mshitakiwa Adamu Kusekwa kwa sababu kuu mbili;

. Yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria

. Yalichukuliwa kwa kuwatesa watuhumiwa kama njia ya kuwashurutisha kukubali tuhuma hizo!

2. Kwa sababu hiyo, ikasabanisha kesi ya msingi kusimama kuendelea kusikilizwa ili hili shauri dogo lisikilizwe na kutolewa maamuzi (trial within trial) kwa upande wa mashitaka kuthibitisha kuwa walifuata utaratibu wa kisheria au upande wa utetezi waoneshe kuwa utaratibu wa kisheria haukufuatwa.

Lengo la objection hii ni upande wa utetezi kutaka kuimaliza kesi mapema kwa kuendelea kuanika uongo wa mashitaka haya na hivyo kuithibitishia mahakama kuwa mashtaka haya ni ya HILA, UONGO na ya KUTUNGA.

Sikiliza ufafanuzi wa Mwanasheria akiliweka hili vizuri katika voice video
hiyo hapo juu...

UPDATES:
Tundu Lissu naye auchambua ushahidi wa Afande Ramadhani Kingai
 
Mambo moto, kesi imefikia patamu na hivi ni usikilizajwi wa kesi kwa mfululizo bila kusitishwa, basi mengi yataibuka labda upande wa mashtaka / jamhuri ukiamua kutupa taulo ktk ulingo wa mpambano wa kisheria la kuomba pambano lifutwe kabisa kwa manufaa mapana ya umma.
Wakitupa taulo tutakataa , ngoma iendelee hadi mwisho tuendelee kuwaanika hadharani .

KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE
 
Hii kesi imeenda kuufungua utawala wa Tanzania uonekane duniani jinsi unavyoingilia vyombo vya ulinzi na usalama kwa manufaa ya chama tawala.

Hawa jamaa wanaopewa hizi kazi za utetezi wanapata tabu sana kupanga uongo wao ufanane na ukweli, wakati nasoma maelezo ya Kingai ikanijia picha inawezekana alikuwa hajui chochote akakurupushwa tu na mkubwa wake wa kazi aende kutoa ushahidi.

Najiuliza kama kweli jamhuri walikuwa na interest na hii kesi, kwanini walisubiri mpaka Mbowe alipoanza kuidai Katiba Mpya ndio wamkamate na kumshikilia mahabusu? kwanini wasingemkamata baada ya upelelezi wao kukamilikia wampeleke mahakamani?

Kumbe jamhuri nao inawezekana wana tabia ya kuwaficha "wahalifu", mpaka pale wanapogusa maslahi yao kisiasa ndio wanaanza kuwashughulikia kwa lengo la kuwafunga mdomo, hii serikali ya namna hii haitufai, itatuangamiza kama taifa.
 
CCM na mawakala wao polisi hawatoboi kwenye hii kesi! The light at the end of the tunnel is obvious! Wamtegemeao Bwana ni kama mlima Sayuni!
ujinga ni kudhani haki ya mbowe inatazamiwa kupatikana mahakamani.

hizi hizi mahakama msizoziamini!!!
 
Hii kesi imeenda kuufungua utawala wa Tanzania uonekane duniani jinsi unavyoingilia vyombo vya ulinzi na usalama kwa manufaa ya chama tawala.

Hawa jamaa wanaopewa hizi kazi za utetezi wanapata tabu sana kupanga uongo wao ufanane na ukweli, wakati nasoma maelezo ya Kingai ikanijia picha inawezekana alikuwa hajui chochote akakurupushwa tu na mkubwa wake wa kazi aende kutoa ushahidi.

Najiuliza kama kweli jamhuri walikuwa na interest na hii kesi, kwanini walisubiri mpaka Mbowe alipoanza kuidai Katiba Mpya ndio wamkamate na kumshikilia mahabusu? kwanini wasingemkamata baada ya upelelezi wao kukamilikia wampeleke mahakamani?

Kumbe jamhuri nao inawezekana wana tabia ya kuwaficha "wahalifu", mpaka pale wanapogusa maslahi yao kisiasa ndio wanaanza kuwashughulikia kwa lengo la kuwafunga mdomo, hii serikali ya namna hii haitufai, itatuangamiza kama taifa.
Na hapa bado wanahangaika na washitakiwa wale watatu peke yao hata hawajamfikia mshtakiwa wa nne ambaye ndiye mwamsha dude hili, yaani Freeman Mbowe...

To cut it short, ni kuwa hili shauri linabebwa na makosa ambayo hayapo, hayakuwahi kutendwa na mshitakiwa yeyote....

Hapa hakuna kesi!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom