Kwanini unaogopa kukagua simu ya mke/mpenzi wako?

Kwanini unaogopa kukagua simu ya mke/mpenzi wako?

Red black

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
18,567
Reaction score
60,042
Usiogope kukagua simu ya mke/mpenzi wako kuna baadhi ya details za muhimu sana utazipata na utajishukuru sana.
Screenshot_20260705-191432~2.jpg
 
Sio kwamba hawataki la hasha bali nafsi zao zinaogopoa kukutana na kile wanachohisi kuwa kinawezekana kikawepo........

Wanaogopa kwa kuwa nyoyo zao hazipo huru juu ya maamuzi yanayohitaji akili zao pale ambapo macho yao mawili yatapowaonyeshea ukweli ulio bayana......

Hawataki kwa kuwa wamechagua kuwa wafungwa huru kwenye gereza la mapenzi baada kuzikabidhi nyoyo zao kwa waso kuwa na imani nao.....

Hawawezi kwa kuwa wamechagua kuishi na mwiba kwenye mguu kwa kuogopa maumivu ya kuutoa mwiba ili apate uponyaji wa kudumu!!!

Kwa kifupi vijana wameridhia kuishi na machangudoa na waasherati huku wakipuuzia madhara yatayoletwa na hayo matendo kwa kuwa wao wanaamini hakuna mwanamke au mwanaume wa peke yako!!!......
 
Kwanini ufanye hivo na hukumkuta BIKRA
Hukumkuta bikra sawa, lakini mnapoingia mkataba wa ndoa, si mnakula kiapo cha uaminifu lakini?

Hilo unalisemeaje?

Kutokufungua ama kuogopa kufungua simu ya mwenza ni kuogopa kukumbana na ukweli wa maisha yake halisi.

Yaani hutaki kuyajua ya sirini kwa mtu unayelala naye kitanda kimoja ambaye ndiye msiri wako!

Mbona ni mitihani mizito mnajitwisha?
 
Kiapo tena??
 
Back
Top Bottom