Kwanini unaogopa kuangalia maiti?

Kwanini unaogopa kuangalia maiti?

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Mimi ni muoga sana wa kuangalia maiti, yaani hata kama tulikuwa marafiki vipi ukishakufa sio rafiki yangu tena.

Najua si mimi tu, wapo wengi tu ambao hata uje na wanajeshi wenye vifaru na mabomu hawawezi kuangalia maiti.

Hivi kwanini tunaogopa maiti jamani? tunaogopa maiti itatutokea usiku au tunaogopa kuchelewa kupotea kwa picha ya maiti kichwani?

KWANINI TUNAOGOPA KUANGALIA MAITI??

MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Last edited by a moderator:
umenikopi na kupesti nlivyo ... sijawahi kuaga maiti hata siku moja... hatariiiii
 
Mnakuwa ni watu wa dunia mbili tofauti, pia maitiiaisa. Sababu zikonyingi. Mimi kama maiti inanihusu siogopi, ila kama ya pembeni woga unakuwepo
 
Sio wote twaogopa maiti. Samahani kwa kusema hili, ila labda wewe bado dogo. Kama si dogo basi woga wako ni wa kidinadamu tu. Maisha (pumzi) ni kitu cha thamani sana kwa hiyo unapoona mwili wa binadamu aliyekufa (hauna maisha au hauna pumzi) huwa kunaingiwa na uwoga au hofu kubwa kwa mtu ambaye hajazoea kuangalia maiti. Kwani wewe huwa huendi kuhudhuria mazishi kwa watu? Pole, usihofu. Ila sio wote waogopao maiti.
 
ni kweli mkuu sio wote wanaogopa maiti maana hata mochwari zinaibiwa sana!
 
Sio wote twaogopa maiti. Samahani kwa kusema hili, ila labda wewe bado dogo. Kama si dogo basi woga wako ni wa kidinadamu tu. Maisha (pumzi) ni kitu cha thamani sana kwa hiyo unapoona mwili wa binadamu aliyekufa (hauna maisha au hauna pumzi) huwa kunaingiwa na uwoga au hofu kubwa kwa mtu ambaye hajazoea kuangalia maiti. Kwani wewe huwa huendi kuhudhuria mazishi kwa watu? Pole, usihofu. Ila sio wote waogopao maiti.

kweli kabisaaa. uko sawa mkuu
 
Samahani ila nahisi bado haujapatwa na msiba wa karibu kabisa,mimi nilikua na tatizo kama lako ila nikapata msiba wa mdogo wangu pale TMK hosp huwezi amini tulichaguliwa watu 3 kwenda kumuandaa marehemu(mimi,babu na mdogo wangu wa mwisho)uwoga uliniisha nilipoingia chumba cha maiti maana niliulizwa uyu si mdogo wako?mmekua wote?aya muogeshe sasa kama alivyokua mdogo amini nakuambia sikutoa chozi mpaka usiku nikiwa pekee angu wakati huo dogo tumeshamzika jioni,mpaka leo sina tatizo na maiti kabisa.
 
Maiti zinaogopesha labda zile za ajali na zikiwa zimeharibika vibaya,lakini hizi mbazo maiti kafa anarembua macho na lipstick hazina shida.
 
Maiti zinaogopesha labda zile za ajali na zikiwa zimeharibika vibaya,lakini hizi mbazo maiti kafa anarembua macho na lipstick hazina shida.

Astaq'firullah!!!!Makamee unamaneno wewe,ila mi siogopi pia.
 
Ashakum si matusi! Niwie radhi mkuu, hiyo hatua wote tumeipitia ama tutaipitia, tamaduni zetu zinatutaka tuwaandae maiti za jamaa zetu wa krb, mf bb, mm, yf, husb, mto wako etc! Its a matter of tym, wng wasioogopa washafikwa mkuu!
Ila mkuu hii mada ngumu, muwe mnaeka warn ktk title
 
Hofu ilikuwa kubwa nilipo mdogo,nikisikia jirani kafariki/mtu nnae mfaham,aisee nilikuwa naogopa kuingia ndani nikiwa peke yangu,yaan hata chumba nilikuwa nakiogopa,hata nikiingia kulala nilikua sipati usingizi niliouzoea,
waswahili wanasema kifo ukiskie kwa mwenzako,kikiwa kwako bwana weee heee.
Mzee alifariki nikiwa kijana,kwanza kuhs hof sikuwanayo kabisa,nilpo pokea taarifa nilikuwa kama zuzu,kulia silii kucheka sicheki,sina huzuni,sina furaha.baadae sasa..,,aisee kooni nilibanwa na uchngu,hta nikinywa maji hayapiti vyema,wala hayafuti maumivu kooni, ulichukua muda kutoweka,tumbo liliuma si la taifodi wala njaa,wala hamu ya kula sikupata.
Aisee kweli kufiwa usikie kwa mwenzako.Chaa ajabu hofu ya maiti wala sikua nayo,kama ambavyo zamani nilikuwa nikiogopa,
Kaburi nilisimamia mpaka likakamilika hata hamu ya kumbeba na kumpleka mazikon nilitaka nishiriki kubeba lkn nilishindwa kwa kufaham sitapata fursa kwa namna moja ama nyngne,
Yaani hapo sasa ndo nilijua umuhimu wa Baba.
Mpaka sasa hofu huwa sina,na usngzi nauchapa kama kawa hata kama nikiona maiti iliyokatika kichwa kule..utumbo palee,,ubongo kulee,walaaaaaa.
 
Niliogopa maiti baada ya kuiona moja ilikuwa haijafunga macho then yale macho yakawa kama yamepoteza ile fluid yake (yamebonyea). Ile maiti ilichukua miaka kupotea akilini

Niliacha uoga baada ya kukutana na mikasa ambayo ilibidi nishiriki mwanzo mwisho!

Moja) kuna jamaa alifia gheto kwetu na sie tukiwamo! Aisee...!! Tukaanza kuambiwa sijui mfunge macho na mambo mengi mengi mpaka tulipompeleka mochwari ikawa nafuu.

Pili) mtoto wa dada wa kazi tulikuwa tunakaa nae alikufa ghafla usiku na mwanaume nilikuwa ni mimi pekee na mtaa ulikuwa na makauzu balaa! Piga kelele usiku hawaamki, nikajitoa fahamu kiume mamamaeeee! Duuuh! Nilikuja kutetemeka baada ya maziko

Tatu) mke wa staff mwenzetu alikufa kwa ajali na wakati huo mimi na jamaa tuko tunapata ulaji tukimsubiri my wife wake tumpokee!! Simu ilipopiga ilibidi mimi ndiyo nisimame kwa nguvu zote pembeni ya jamaa mpaka eneo la tukio, aliumia zaidi kichwa na mgongo!! Daah! Nakumbuka tulifika eneo la tukio jamaa hajiwezi so nikalazimika kuwa stering, unambeba mtu unayemfahamu ubongo unamwagika, taya ipo vipande vipande! Nililia baada ya wiki nzima na sikuamini kilichotoke

Mpaka leo, siogopi sana ingawa kama hainihusu sipendi kuisogelea sana
 
Daaah sitaki ata kusikia habari za maiti... hapa nyumbani kwetu alifariki anti yetu,ule mwili wa marehem anti ukawekwa chumbani kwangu kitandani daaah nilitumwa na mama niende nikafunge chumba sasa wakati wa kufunga mlango nikasema ngoja nikafungue jeneza nione daaah nilijikuta niko chini ya mti nimemwagiwa maji napepewa..na tangu siku hyo nilikuwa naweweseka sana bt nilivyokuja kuombewa ile hali ikatulia. mpka leo sina hamu ya kuaga maiti wala kuiona naogopa sana
 
aisee.. pole mkuu maiti mbona ni mtu wa kawaida tu.. mi nadhani we ulishajiwekea moyoni kwamba maiti ni dubwasha,au jini kitu ambacho si kweli, kila mtu atakua maiti hapa duniani bora uzizoee tu hahaha
 
Daaah sitaki ata kusikia habari za maiti... hapa nyumbani kwetu alifariki anti yetu,ule mwili wa marehem anti ukawekwa chumbani kwangu kitandani daaah nilitumwa na mama niende nikafunge chumba sasa wakati wa kufunga mlango nikasema ngoja nikafungue jeneza nione daaah nilijikuta niko chini ya mti nimemwagiwa maji napepewa..na tangu siku hyo nilikuwa naweweseka sana bt nilivyokuja kuombewa ile hali ikatulia. mpka leo sina hamu ya kuaga maiti wala kuiona naogopa sana

Dah...
Samahani nimecheka kama mazuri vile.
Huo utundu wako balaa.
Yalishapita
 
Ukifiwa Sana hutaogopa maiti,japo zingine hutishaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom