Kwanini unaogopa kifo?

Kwanini unaogopa kifo?

Kifo mi nakiogopa kusema ukweli,kwasababu napenda kula starehe za dunia mwanzo mwisho mpaka pale nitakapo zeeka sana,ila mambo ya kufa bado kijana sitaki hata kusikia.
Kufa si tatizo tatizo huko uendapo Salama?
 
Wiki iliyopita nilikuwa pale mochuari muhimbili, loh watu tunakufa jaman. Gani moyo wangu ulikuwa na ganzi kwa muda woote nilikuwa pale.
Kifo kinatisha, kinaogopesha kweli ni ukumbusho kuwa Mungu yupo.
 
Binafsi nikifikiria kifo napata hofu. Nawaza je hicho kifo kitasababishwa na nini? Je kitakuwa kifo cha maumuvi au itakuwa katika usingizi nisijue lolote? Kiukweli kifo kinatutatiza wengi. Hata pale tunaposema hatuopogi kifo bado tunakuwa na hofu kidogo tukiwazia kifo na namna kitakavyo tukia.

Nawaza pia namna wapendwa wangu watahuzunishwa na kifo changu. Wakikumbuka mambo mengi mazuri niliyofanya watajisikia vizuri sana lakini watajisikia huzuni kunikosa moja kwa moja. Mawazo yangu, fikra zangu, kazi zangu zitaishi lakini mwili wangu, vile nilivyokuwa nasemezana na wapendwa wangu, kusafiri pamoja, kula pamoja, kufanya kazi pamoja......hayo yote yananifanya niwaze mengi kuhusu kifo. Najua kifo kipo tu na kitatokea siku moja.....lakini hii haiondoi hofu yangu juu ya kifo.

Natamani sana kuishi milele.
 
Siogopi kufa sbbu nakuwa sielewi nn kitatokea huko niendapo.ninachoogopa ni Ile kufukiwa na kuliwa na wadudu.
 
Humu kila mtu amewahi kulala usingizi na kuota ndoto!!! Mwili unakala ila roho ilio ndani hailali!! Km roho hailali na mwili unalala na ukiwa usingizini hutambui nn kinaendelea katikaa dunia hii mpaka uamke!! Huo ni mfano wa kifo katika mwili!! Swali ni kwamba roho itakuwa wapi???? Na inafanya nn??
 
Kwa hiyo kama ukijirekebisha maisha yaendelee milele baada ya kurudi mara ya pili???
Hapana, kuna watu bado wanamashhaka na uwepo wa pepo na moto.kwahiyo kama ukifa na ukikuta vitu hivyo vipo"unapewa nafasi yakurudi duniani nakuchagua aina ya maisha yakuishi baada ya kifo.

Wengi hatuogopi kufa,tunaogopa kutangulia na aina ya kifo.na hatujui tutafikia wapi.
 
Au kuwe na levels mbalimbali.
Ukifa dunia hii, unazaliwa dunia nyingine kama hii katika hali hii.
Hii process inaendelea milele.
Mkuu Dunia nyingine tena? Dunia si ni hi hii moja tu.duniani😀😀😀😀...
 
Mwenye matendo mazuri mbele ya mwenyez Mungu hawez ogopa kifo,,,,,,uoga wa kifo nipale unapojua kabisa kuna mahali nimeteleza kwakuvunja maelekezo tulopewa na mwenyez mungu lazm ukiogope tu na daima hakizoeleki
 
Naogopa kufa jamani,neno lenyewe tu nikiliwaza mwili unapata ganzi apo bado kitendo.Laiti kama kungekuwa na kitu cha kufanya ili niishi milele ningekifanya duu naogopa sana kifo
 
Utakuwa mpuuziii.wa kutupwa.kama utaogopa kifo afu huku...unapenda kwenda kuzka @napta
 
Siogopi kifo sababu ni njia yetu. Ila naomba nife nikiwa nimefanya mazuri yote ninayoyataka kwa familia na jamii. Bado vitu 3sijatimiza kifo naomba nivumilie nitimize.
 
Back
Top Bottom