Kwanini ulipize kisasi eti kisa na wewe ulitendwa?

immasakha

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
489
281
Tulipendanda kwa muda mfupi sana na kila mmoja akafanikiwa kuteka moyo wa mwenzake na tukapeana kila cha kupeana katika mapenzi, chakusikitisha ghafla tu ananitumia sms ya kwamba mimi na yeye basi kimapenzi, kwani kapata mtu amemuhadithia kwamba nilikua na msichana fulani nina date nae.

Nilipojaribu kumuambia tumpigie simu kwa pamoja na tumsikilize huyo msichana kama tupo pamoja au hatupo pamoja yeye kakataa, nilichokuja kugundua ni kwamba kwa vile yeye alitendwa na kataka na mimi niwe mfano kwakwe amelipiza kisasi cha kunitenda.
 
eti tulipendana sana
we ni nani hadi uusemee moyo wa mtu ?

huyo kwako alikua anavuta muda ili ampate ampendaye
 
sasa mkuu linakuumiza kichwa hilo... temana nae maisha ya siku hz rahisi sana sio kama zamani...!
 
Jikaze kiume muache aende tu. Maji yakimfika shingoni atarudi kwako akitambaa kwa magoti. Binafsi kama huwa sina makosa au madhambi yoyote niliyomtendea mwenza wangu, basi huwa sina shaka kabisa najua atakwenda. Lakini atarudi tu na akirudi ndo nampiga chini kabisa!
 
ukiwa kwenye mahusiano usipende kusikiliza maneno ya watu kama huyo mpenzi wako kasikiliza maneno kapanic

bora angekufuma maneno tu alikua hakupendi alikua anatakutafutia sababu tu kidogo achana nae mwache aende
 
Back
Top Bottom