Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Na hapo ukihoji, utasikia eti usiwaseme vibaya watumishi wa Mungu.
Yaani kuna mmoja ninamfahamu, amezaa na bidada flani hapa mtaani na anamuhudumi kama kawaida na anaenda pale kama mume kabisa.
Kuna mwingine yeye tunakatanae maji baa kila jioni.
Kuna mwingine yeye alipata ajali na gari la kanisa, akilwa na mhudumu wa bar ambae akafariki papohapo.
Kwakweli minaenda kanisani ili nikamuabudu Mungu wangu tu, mengine huwa sitaki hata kuyafikiria
 
Unakuta Msanii ambae Ni KIOO Cha jamii,

Mlevi wa sigara na pombe wa kupindukia, anaimba matusi kibao kwenye nyimbo zake, anachezesha wanawake uchi kwny video zake.

anatuharibia VIJANA wetu.

Akishapata pesa kutoka kwenye iyo kazi yake haramu, Anaituma mkoani kujengea nyumba ya ibada.

Siku moja kabla uzinduzi,
Anapanda usafiri wa Umma, anawalipia nauli watu wote na pombe za bure.

Alfajiri,
Watu wanafika wamelewa mpk wamejinyea.

Saa 3 asbuhi,
anaenda kuzindua nyumba ya ibada.
Viongoz wa dini wanampokea na kumlaki Kama shujaa.

Saa 8 mchana,
Anapiga show kwenye uwanja wa mpira, wamama,wababa, VIJANA, na watoto wanalewa pombe,wanacheza nyimbo za ngono.

Viongozi wa dini wako kimya
 
Yaan boss kwa hali ya Sasa huko kanisani kusema unaenda kumuabudu Mungu huwenda ukajidanganya aisee labda kusema tunaenda kujumuika tu na jamii.

Mimi binafsi sina shida na matendo ya kiongozi wangu wa kiroho, kujulika anataembea na fulani au ana mahusiano na mtu mfulani au anakunywa sana pombe kwangu sio shida! Ni bahati mbaya tuu imejulikana ila kila mmoja ana matendo yake mimi na we na nafsi zetu sina tuhukumu.

Kilicho nisikitisha kwa upande wangu Ni ile wakiwa katika ibada waliacha kulihubiri kwa usahihi Neno la Mungu kwa kiasi walichojaliwa badala yake wamegeukia mipasho na umbea! Mpaka maungamo ya watu wanayasema ila tu hawataji jina, na tunakoelekea watakuja kutaja tu fulani jana aliungama hivi na vile.

Wao kwa wengi wao mahubiri yanayolenga michango na matoleo ndio yaelezwa kwa usahihi na kwa muda mrefu sana.
Nayo haya ndio sababu ya vijana wengi kutoenda kanisani, achilimbali matabaka wanayoweka ya wenye nacho na wasio nacho.
 
Naendaga mara mojamoja kumwabudu Mungu wangu mengine nayajua mengi sana ambayo hata mimi nayafanya na ninafanya nao ila nikiwaza sote ni binadamu na nikikumbuka bila unafki maisha hayaendi nawaza ukuu wa Mungu ndani yangu licha ya maovu yangu natakiwa kushukuru.

Leo nimenda kanisani but last time kwenda ilikua usiku wa pasaka kidogo niaibike kumbe kwenye kutakiana amani waumini wana-wave mimi nilikua nataka kushika mtu mkono[emoji28][emoji28]

Anyway nasubiri mvua ikate niende home.
Have a blessed Sunday [emoji120][emoji3589]
 
Niliacha kwa sababu ya wale dada zetu wanao tuvalia nguo za kutamanisha kanisani.

Niliona wazi na jiongezea dhambi tu ndani ya kanisa kwa kuwa taman
Hapo ninatilia mashaka na afya yako ya mwili au akili.

Hakuna mwanaume 'timamu' anayelaani kuangalia mwanamke mzuri hapa duniani.

Kuangalia urembo wa asili walioumbwa nao wanawake si dhambi pia ni dawa inayotibu msongo wa mawazo.

Nimeshangaa sana kukutana na comment kama hii itokayo kwa mtu mwanaume anayedai kulaani kuangalia wanawake wazuri wazuri!
 
Viongozi wa kanisa langu kubaki kimya kipindi serikali inatesa, kuua na kubambikia kesi wapinzani.

Siendi church labda nje ya nchi au nijiridhishe nyendo za anayeongoza kanisa kuhusu itikadi zake.
 
Mimi mapdri wangu wamekua kituko,kila shetani akienda kusali wanampa nafasi ya kuropoka madhabahuni...kanisa limekua jukwaa la kumsifu shetani
 
Baada ya kugundua pasi shaka kuwa Yesu kristo wa Nazareth ni Mwafrika Mweusi. Baaasi nikaona kweli niliingizwa chaka mbaya!!!! siku hizi wanaongea nawatazamaaa juuu halafu nawashushaaa then napumuaaa!!!

Halafu kama wananusaga hivi, siku hizi hawanishobokei km zamani!
 
Missada lazima inatoka vatican hawataki msiende
 
Dah mimi hata sielewii nilijikuta tu sipendi kwenda kanisani tu
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Ongeza
Ujenzi wa Ukuta
Ujenzi wa Duka la Kanisa
Ujenzi wa Ukumbi
Chakula cha Seminary

Ili hali ukipeleka mtoto shule hawakupi discount wala kwenye ukumbi.


Michango ya Jumuiya na vyama vya kanisa kibao, kufuatana hadi nyumbani hii ndio huwa siipendi
 
VIWAWA, KAPU LA MAMA, KAPU LA PAROKO, KAPU LA MAKATEKISTA, KAPU LA MASISTA, KAPU LA REDIO MARIA, UJENZI WA KANISA, SADAKA, SHUKURANI, KUMSHIKA MKONO BABA PAROKO, KAPU LA BABA ASKOFU, alafu wao tunavyolalamika maisha magumu mambo hayaendi wao wamekalia kusifia na kujipendekeza kwa Mzee wa Chato
 
Hao sio Waislamu
Islam ni Aman.. Uislam unamtaka Muislamu kumpa haki asie na Muislamu..
Uislamu unamkataza Muislamu kuto mlazimisha yeyote katika dini isipokuwa kumlingania akipenda..
The p in islam stands for 'peace'
 
Ninyi endeleeni tu kutokwenda kanisani kwa amani, hakuna anayewahukumu, japokuwa naamini hapa yenyewe nafsi zenu zinawasuta ndiyo maana mnajifanya kutafuta justification tu ya matendo yenu hamna lolote..!
Halafu we mdada nimeanza kukupenda bure...
 
Tunasubiri kutimiza aliyotuahidi wana Kawe Sasa. Hapo ndipo mtego ulipo na huduma yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…