GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,216
- Utaambiwa uongeze Hela.
- Utaambiwa utoe shuka au muda mchache tu Mhudumu atakuja kutoa shuka.
- Utaambiwa hakikisha choo unakiacha katika hali ya usafi.
- Utaulizwa kama una air fresher.
- Utaambiwa hatutaki kusikia makelele.
- Ukishapewa hayo mafuta unapewa pia na Panadol au Diclopa.
- Utasisitizwa kuyafungua madirisha muda wote.
Je wenzangu na nyie mmeshakumbana na hii hali? au Mimi tu labda nina bahati mbaya na hizi gesti / loji ninazoingia? Na huwa wanakuwa na maana gani labda hasa wanapokuambia hayo maneno niliyoyainisha hapo juu?
Hii hali imenikwaza sana hadi sasa nimeamua nikiwa tu nasafiri Mikoani basi kwanza natafuta Rafiki yangu aliyepo huko ili niwe nalala kwake hadi ninapomaliza mizunguko yangu kwani nahisi labda huu ni MPANGO MAALUM wa KIAJENDA kwa wamiliki wote wa nyumba za kulala Wageni gesti na loji.
Mwenye ufahamu zaidi naomba anifafanulie tafadhali! Akhsanteni.