Kwanini UKAWA itashinda kesi ya umeya Kinondoni

Hiyo mahakama kama ni ya hapa Tz CCM watashinda pia kibabe hivyo sidhani kama itawezekana kuwatoa CCM kwa kura au mahakama.
CCM itaondoka madarakani siku tukifanikiwa kupigania kupata KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Malisa GJ;

Hawa CCM chini ya Magufuli ni shida na balaa tupu.

Hawa wataitisha hata bunge la maCCM watupu usiku kwa usiku ili kubadili sheria in favor of them!

Wakishindwa hilo, trust me.......Magufuli ana uwezo wa kuwapa majaji na mahakimu wote wa mahakama zote likizo za malipo manono kwa miaka yote minne iliyobaki ili mradi tu kesi hiyo ikae na kujiozea hapo Kisutu!!

Na wakishindwa yote hayo mawili hapo juu, basi hakimu ama jaji yeyote atakayesimamia kesi aweza kusikiliza kesi na kufikia maamuzi kwa kusoma hukumu iliyoandaliwa magogoni chini ya mtutu wa bunduki in favor of the CCM, the ruling party!!
 
View attachment 423635 KWANINI UKAWA ITASHINDA KESI YA UMEYA K'NDONI.

By Malisa GJ,

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]: Akidi ya kikao haikutimia. Sheria inataka 2/3 ya wajumbe wote kuhudhuria na kusaini mahudhurio ndipo mkutano upate uhalali wa kufanyika. Wajumbe HALALI wa mkutano huo ni 34, kwa hiyo 2/3 ni wajumbe 23. CCM ilikua na wajumbe 18 (kati yao walikuwepo wasio halali). Hata hivyo iadi ya wajumbe 18 wa CCM haikutimiza akidi, kwa sababu wajumbe wa UKAWA hawakusaini mahudhurio. Kwahiyo mkutano wa jana ni batili. Mahakamani CCM hawawezi kujitetea ktk hili. #Moja_bila.!

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]: Kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo ya serikali za mitaa, taatifa ya mkutano mkuu wa uchaguzi inapaswa kutolewa angalau masaa 72 kabla ya uchaguzi (i.e siku 3 kabla). Lakini barua za mkutano wa uchaguzi zilitumwa tar.22 zikielekeza kuwa mkutano mkuu ni tar.23. Notification ilikua chini ya masaa 24 kinyume na sheria inavyotaka. Mahakamani DED hawezi kujitetea kwenye hili. #Mbili_bila.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: Sheria ya marekebisho ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 2006 (Local Government Laws - Miscellaneous Amendments), Sheria No.13 ya mwaka 2016 kifungu cha 17 (d) inasema, Mbunge yeyote atakayeteuliwa na Rais atakuwa mjumbe katika Halmashauri anayoishi (Any member of Parliament appointed by President shall be a member to a Council in which that member ordinarily resides).

Lakini Dr.Tulia Akson amepiga kura Halmashauri ya Kinondoni wakati yeye ni mkazi wa Kibamba na Halmashauri yake ni Ubungo. Kwahiyo Tulia si mjumbe halali wa Kinondoni kwa mujibu wa sheria. Mahakamani Tulia hawezi kujitetea ktk hili. #Tatu_bila.!

[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]: Sheria ya marekebisho ya sheria za serikali za mitaa ya mwaka 2006 (Local Government Laws - Miscellaneous Amendments), Sheria No.13 ya mwaka 2016 kifungu cha 17 (e) inasema wabunge ambao ni wateule wa Rais wakizidi watatu kwenye Halmashauri moja, wale waliozidi wanaweza kuhamishiwa Halmashauri za jirani provided Waziri ataujulisha umma kupitia gazeti

(Provided that where members of the Parliament appointed by the President are more than three, the Minister shall by order published in the Gazette direct that the rest of the Members of Parliament in excess of the three to become members of the neighbouring council as if they were ordinarily resident in those councils).

Kwa mujibu wa kifungu hiki cha sheria, hapa kuna mambo mawili. Jambo la kwanza ni kwamba wabunge wa kuteuliwa na Rais wawe zaidi ya watatu kwenye Halmashauri moja, pili Waziri atoe tangazo kwenye gazeti la serikali kuwahamisha waliozidi.

Sasa Ndalichako na Mahiga kuhamishiwa Kinondoni kutokea Ilala, je Ilala walizidi watatu? Jibu ni Hapana, hawakuzidi watatu. Sheria inasema wakishazidi watatu ndio wahamishiwe kwenye halmashauri ya jirani. Lakini Wabunge wa kuteuliwa na Rais kwa Ilala walikua wawili tu (Ndalichako, na Mahiga). Kwa hiyo uhamisho wao kwenda Kinondoni ni BATILI kwa mujibu wa kifungu hicho cha sheria. Si Mahiga wala Ndalichako anayeweza kujitetea mbele ya mahakama. #Nne_bila.!

Pia sheria inasema kabla hawajahamishwa Waziri husika lazima atoe taarifa gazetini kuelezea sababu za uhamisho wao. Waziri wa TAMISEMI Ndg.George Simbachawene hajawahi kutoa tangazo lolote gazetini kuhusu kuwahamisha Ndakichako na Mahiga kutoka Ilala kwenda Kinondoni. #Tano_bila.!

[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]: Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa pamoja vinataja suala la serikali za mitaa kuwa SIO SUALA LA MUUNGANO. Kwahiyo Mbunge wa Z'bar haruhusiwi kuwa mjumbe kwenye halmashauri za Tanzania Bara, na Mbunge wa bara haruhusiwi kuwa mjumbe wa halmashauri yoyote upande wa Zanzibar. Kwahiyo kitendo cha Prof.Mbarawa kupiga kura Kinondoni sio tu ni kinyume cha sheria bali pia ni kinyume cha Katiba ya nchi ambayo ni sheria mama.

Kwahiyo haihitaji degree kujua kwamba uwakilishi wa Profesa Mbarawa ni batili na hata Kura yake ni batili pia. Prof.Mbarawa hawezi kujitetea mbele ya Mahakama kuhusu. #Sita_bila.!

Kwa kifupi ni kwamba Wabunge wote walioteuliwa na Rais walioshiriki kupiga kura Kinondoni jana ni wajumbe batili. Wawili (Ndalichako na Mahiga) ni wa Ilala, Tulia ni wa Ubungo na Mbarawa ni wa Zanzibar. Wote wanne hawana uhalali wa kushiriki vikao vya Halmashauri ya Kinondoni.

Kwahiyo nategemea Mahakama itangaze uchaguzi wa jana kuwa batili, na kuitisha upya uchaguzi halali, (in absence ya wajumbe wanne feki ambao ni wateule wa Rais). Kwahiyo kati ya wajumbe 18 wa CCM toa wanne (feki), wanabaki 14.

Mahakama pia nategemea itawaruhusu wajumbe halali wa Halmashauri ya Kinondoni walioondolewa bila sababu zozote za msingi waweze kushiriki vikao vya Halmashauri hiyo. Wajumbe hao ni wabunge wawili wa UKAWA (viti maalum) na madiwani wawili (viti maalumu).

Kwahiyo ktk uchaguzi wa marudio, utakaofanyika baada ya Mahakama kutoa hukumu, nategemea UKAWA itakua na wajumbe 20, na CCM wajumbe 14. Jumla 34. Hawa ndio wajumbe halali wa mkutano mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

The good thing about Law ni kuwa "Sheria haipendagi ujinga". Lissu alisema tutawashinda Mahakamani na tutawasinda nje ya Mahakama", kwa ujinga wao wa kupenda namba wakati hawajui hesabu. #Sita_bila, kama mmesimama vile.!


Malisa GJ.
Majina ya akina Sitta yana mkosi sana ! Leo unaambiwa wewe ni Meya , kesho unavuliwa kwa kudhalilishwa na Mahakama !
 
Tuombe iwe hivyo!! Maana Mahakama nayo inaweza kuvishwa. Majoho ya madiwani kumi wa ccm! Hapo badala ya 18 wakafikia 28! Mbona mbunge wa tanga alipiga kura Arusha? Tuombe tu ccm wasiamue kumtumia mwenyekiti wao!! Maana kwa mujibu wa statement yake pale kinyerezi 1 wapinzani ni wow!woh woh,d-o-g-s
 
Majina ya akina Sitta yana mkosi sana ! Leo unaambiwa wewe ni Meya , kesho unavuliwa kwa kudhalilishwa na Mahakama !
kweli kabisa mkuu nimemkumbuka sana Samweli Sitta alivyoharibu rasimu ya Warioba kwenye bunge la katiba leo ameshasaulika kwenye siasa.
 
Hiyo kesi itasikilizwa miaka mitano. Huo upuuzi una dalili za baraka kutoka juu.
 
Hii kesi itapigwa danadana sana.
Ushauri kwa Chadema,umeya wa kinondoni apewe diwani kutoka CUF.
Wataangalia upande gani utakuwa na madiwani watakubaliana [HASHTAG]#UKAWA[/HASHTAG] ni familia pamoja akishinda diwani wa CUF ushindi kwa Chadema akishinda wa CUF ni ushindi kwa Chadema.
 
Jamani mimi nimeishia la 3B naombeni nikawe wakili wa Ukawa kwenye kesi hii na ninaomba Wakili wa serikali awe na PhD nikamtoe mkuku mahakamani ,naomba msimsumbue Tundu Lisu kwa kesi hii
Na msiniletee Tulia Ackson mwenye PhD maana huyo hajui hata FFU ni kitengo katika jeshi la polisi
 
Prof Lipumba ameshasema ukawa wameshindwa umeya sababu ya ubinafsi wa chadema.

Lawama zote zipelekwe kwa wabadili gia za angani chadema
uwe unaficha upumbavu wako kwa uhuni ambao mlifanya jana ni mpuuzi anayeweza kuwaunga mkono
 
Prof Lipumba ameshasema ukawa wameshindwa umeya sababu ya ubinafsi wa chadema.

Lawama zote zipelekwe kwa wabadili gia za angani chadema
Ukiona mtu anatumia mtazamo wa mtu aliye filisika kisiasa kujenga hoja zake ujue yeye kafilisika akili.
 
Mkuu hayo yote ccm wanayajuwa. Mbona mikutano ya kisiasa pia ipo kikatiba, je ukawa wanafanya?
 
Back
Top Bottom