Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,622
- 26,975
CCM hata wakisimamisha sisimizi lazima washinde nafasi ya Urais
kwa comment hii uko box kwa kichwa,jukwaa limevamiwa!!!!
CCM hata wakisimamisha sisimizi lazima washinde nafasi ya Urais
hawa UKAWA hawajiamini na hawana mgombea, wanategemea tu kukopi kwa ccm au yale makapi yaliyochujwa ndio waneemeke nayo. si busara kabisa kupoteza muda na watu wasiojielewa
CCM wamejitokeza wananchi wanawatahmini na wenye mamlaka wanawasikiliza wananchi, UKAWA wanasubiri makapi kama kawaida yao, wataalam wa kushibia masazo ya CCM.
Wakati tukielekea katika Uchaguzi mkuu umoja wa katiba ya wananchi UKAWA unaofanywa na vyama vya upinzani vikiongozwa na vyama vitatu maarufu, (CHADEMA, NCCR na CUF) bado havijaonesha nia ya kuteua safu yao ya wale watakao wawakilisha kwenye uchaguzi katika nafasi ya URAIS.
UKAWA wanafanya haya kwa sababu kuu mbili;
Kwanza wanapima upepo wa yale yanayoendelea katika mchakato wa kutafuta mgombea wa Urais kupitia CCM. Ili wajue wanapambana na nani na nani anaweza kufaa kupambanishwa na mteule wa CCM.
Pili, wanaangalia hatma ya mgombea fulani kupitia CCM kama atapitishwa ama la. Kama mgombea huyo akikosa nafasi kupitia CCM basi wamshawishi kugombea kupitia UKAWA kwani UKAWA wanaamini kua mgombea huyo anakubalika na wengi hata wale wasio CCM lakini kutokana na mwenendo wa swala zima la uteuzi kuna viashiria ambavyo havimpi nafasi mgombea huyo, hivyo kuipa UKAWA kete ya kumshawishi mgombea huyo kugombea kupitia tiketi ya UKAWA kama akikosa nafasi kugombea kupitia chama chake cha CCM.
Sidhani kama kuna sababu nyingine tofauti na hizo ambazo zinaifanya UKAWA kutoteua safu yake ya uongozi katika uchaguzi wa oktoba ukizingatia kwamba wananchi wanayo haki ya kujua mgombea mapema ili kumtathmini kabla ya kupiga kura.
Wenye nia watangaze halafu taratibu zifuatwe..hiyo ndiyo demokrasia taratibu ndio zitachagua mgombea lakini ni muhimu wenye wajitokeze mapema isije baadaye ukatokea mkanganyiko wakati muda ni mfupi.
Aa wapi huko ugogoni na umasaini mnakopata ushindi wa kimbunga wameamka.mjiandae kisaikolojia hata profesa ameshawaambia.CCM hata wakisimamisha sisimizi lazima washinde nafasi ya Urais
Za asubuhi kaka stroke, jana kuna uzi uliletwa hapa kama huu wakwako, tulipoanza kuchangia tu ukatolewa. Hope ni wewe kwa id yako nyingine ama ni humo ofisini mwenu mlikuwa mnataka mpime upepo. Ninachokiona kwa Ukawa hawana muda wa kuiga style za kiccm kutangaza mgombea wao. Nadhani umeona kwa ccm watu wanajitangazania tu nia na kuishia kwenye siasa za kipuuzi kwa kuchafuana hapa mitandaoni. Mara sijui huyu hajui kufunga koti la suti, huyu kapotea na helkopta, mwingine sijui aliiba pesa za Ghadafi na upuuzi mwingine kama huo. Ukawa wao wameamua kuangalia vigezo kwanza kisha watateua watu watakaofikia vigezo ili kuweza kuwapata wagombea bora na sio bora wagombea kama mnavyofanya nyinyi.
Katika kitu kinachowafanya muendelee kufanya siasa zilizopitwa na wakati ni kudhani Ukawa wanasubiri makapi toka ccm ili wawape nafasi. Ukawa wanataka wafanye usaili wa uhakika ili wapate wagombea competent na sio kila mtu kujitangazia nia wakati hata rekodi yake ya utendaji ikiwekwa mezani ni utata mtupu. Nakudhibitishia hili kwa kuangalia hata shaka ya mwenyekiti wenu wa ccm kwenye kilele cha sherehe yenu ya kuzaliwa alisema, waliojitokeza hawafai bali wanaofaa wanahitaji tu kukumbushwa na kushawishiwa. Hiyo nitawashangaa na kuwadharau sana Ukawa kama wataiga mbinu za kichovu za ccm kila mtu kujitokea kutangaza kugombea urais alafu akiulizwa kwanini nchi ni maskini aseme hajui. Huko UKAWA ni lazima ukionyesha nia ujenge hoja pasi na shaka unajua kile unachokisema na uwezo wa kukitekeleza ili ukija kwenye midahalo ujenge hoja zenye mantiki. Nyinyi ccm kwa kuwa mnataka madaraka kwa mazoea na kinachoangaliwa huko kwenu sio uwezo bali ni uwezo wa rushwa, fitina, chuki, majungu na wizi wa kura kila mtu anaweza kujitangaza, na ninashangaa kwanini wewe bado hujatangaza.
Tumeshuhudia mgombea wa ccm akishatangazwa hata kama amepita kwa rushwa na fitina na mbinu zote chafu huwa hamjali kwani huku kwa wananchi ni lazima apite sio kwa kura bali kwa kutumia tume ya uchaguzi isiyo huru, jeshi la polisi lisilojitambua, rushwa na ulaghai. Nadhani wewe ni shahidi kwamba kwenye mikutano yenu ya kampeni kama ni mkutano wa masaa matatu. Masaa mawili ni burudani za kina Diamond, Ze comedy, nusu saa ni ya kusalimia na kutambulisha msafara wa mgombea, robo saa kuelezea ilani na robo saa iliyobaki ni kumwaga ahadi hewa pamoja na kuagana!! Lakini kwa wapinzani ni lazima kwenye mkutano wa masaa matatu nusu saa ni ya kujiandaa na utambulisho, lisaa limoja na nusu ni sera na jinsi ya kutekeleza sera hizo. dakika 45 ni maswali na majibu, dk 15 shukrani na kuaga. Kwenye midahalo wapinzani ndio nyumbani kwao wakati huko kwenu ni amri toka kwa mtendaji mkuu wa chama kwamba ni marufuku kwani anajua hamna hoja bali majungu, chuki, fitina huku mkikiri kwamba hakuna aliye msafi ndani yenu. Siasa za safari hii zimebadilika na watu wamejitambua ngoja wapinzani wawaonyeshe siasa ni nini.
CCM hata wakisimamisha sisimizi lazima washinde nafasi ya Urais
Siku zote kiongozi mzuri ni yule anaefata sheria. Kwani sheria zinasema ni lini wagombea wa nafasi mbalumbali wanatakiwa kujitokeza na kuchaguliwa kuwakilisha vyama vyao? UKAWA wako makini na sheria acha watafuta madaraka wa sisiemu waendelee kuvunja sheria kwa kutangaza kila kukicha. stroke vipi milungula ya juzi na jana Dodoma uliambulia hata kidogo au hawajakukumbuka niwakumbushe.
Hapo sasa ndo unadhihirisha utaahira wako! kama watu hawaeleweki na hawajiamini shida ipo wapi hapo kwa ccm! si muanze sherehe ya ushindi basi mapema! ila nina wasiwasi umekunywa supu ya magimbi wewe Saburi lina washa kinomahawa UKAWA hawajiamini na hawana mgombea, wanategemea tu kukopi kwa ccm au yale makapi yaliyochujwa ndio waneemeke nayo. si busara kabisa kupoteza muda na watu wasiojielewa

wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu umoja wa katiba ya wananchi ukawa unaofanywa na vyama vya upinzani vikiongozwa na vyama vitatu maarufu, (chadema, nccr na cuf) bado havijaonesha nia ya kuteua safu yao ya wale watakao wawakilisha kwenye uchaguzi katika nafasi ya urais.
Ukawa wanafanya haya kwa sababu kuu mbili;
kwanza wanapima upepo wa yale yanayoendelea katika mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kupitia ccm. Ili wajue wanapambana na nani na nani anaweza kufaa kupambanishwa na mteule wa ccm.
Pili, wanaangalia hatma ya mgombea fulani kupitia ccm kama atapitishwa ama la. Kama mgombea huyo akikosa nafasi kupitia ccm basi wamshawishi kugombea kupitia ukawa kwani ukawa wanaamini kua mgombea huyo anakubalika na wengi hata wale wasio ccm lakini kutokana na mwenendo wa swala zima la uteuzi kuna viashiria ambavyo havimpi nafasi mgombea huyo, hivyo kuipa ukawa kete ya kumshawishi mgombea huyo kugombea kupitia tiketi ya ukawa kama akikosa nafasi kugombea kupitia chama chake cha ccm.
Sidhani kama kuna sababu nyingine tofauti na hizo ambazo zinaifanya ukawa kutoteua safu yake ya uongozi katika uchaguzi wa oktoba ukizingatia kwamba wananchi wanayo haki ya kujua mgombea mapema ili kumtathmini kabla ya kupiga kura.