Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,017
- 51,157
Wakati tukielekea katika Uchaguzi mkuu umoja wa katiba ya wananchi UKAWA unaofanywa na vyama vya upinzani vikiongozwa na vyama vitatu maarufu, (CHADEMA, NCCR na CUF) bado havijaonesha nia ya kuteua safu yao ya wale watakao wawakilisha kwenye uchaguzi katika nafasi ya URAIS.
UKAWA wanafanya haya kwa sababu kuu mbili;
Kwanza wanapima upepo wa yale yanayoendelea katika mchakato wa kutafuta mgombea wa Urais kupitia CCM. Ili wajue wanapambana na nani na nani anaweza kufaa kupambanishwa na mteule wa CCM.
Pili, wanaangalia hatma ya mgombea fulani kupitia CCM kama atapitishwa ama la. Kama mgombea huyo akikosa nafasi kupitia CCM basi wamshawishi kugombea kupitia UKAWA kwani UKAWA wanaamini kua mgombea huyo anakubalika na wengi hata wale wasio CCM lakini kutokana na mwenendo wa swala zima la uteuzi kuna viashiria ambavyo havimpi nafasi mgombea huyo, hivyo kuipa UKAWA kete ya kumshawishi mgombea huyo kugombea kupitia tiketi ya UKAWA kama akikosa nafasi kugombea kupitia chama chake cha CCM.
Sidhani kama kuna sababu nyingine tofauti na hizo ambazo zinaifanya UKAWA kutoteua safu yake ya uongozi katika uchaguzi wa oktoba ukizingatia kwamba wananchi wanayo haki ya kujua mgombea mapema ili kumtathmini kabla ya kupiga kura.