Wakuu habari za majukumu,
Kuna huu utafiti mdogo niliofanya na baada ya kuongea na baadhi ya watu,
Nimegundua kipindi kile cha kampeni ilikuwa ukimuuliza mtu wewe ni chama gani anakwambia wazi kuwa mimi UKAWA na kama ni CCM wengi wao walikuwa wanasema hawana chama kwa kuogopa kuzomewa au kuchekwa.
Lakini naona baada ya uchaguzi na kutokana na hii kasi ya Rais JPM kufanya mambo mengi yaliyo kwenye katiba ya UKAWA, kibao kimewageukia kabisa UKAWA kwa sasa watu hawapo huru kujitambulisha hadharani kuwa ni wana UKAWA. Hawapo kifua mbele na UKAWA kama mwanzoni tena.
Nimegundua siasa ni kama soka kuna kushambulia na kushambuliwa.
Ningependa kufahamu ni mtazamo wangu mwenyewe au hata nyie mmegundua hili?
Nawasilisha.