Kwanini tusiunganishe nguvu kama lengo ni moja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tusiunganishe nguvu kama lengo ni moja!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by karim wade, Sep 12, 2012.

 1. k

  karim wade Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF! Napata wakati mgumu sana kuelewa, kama walio wengi lengo letu ni kubadilisha mfumo uliopo sasa ambao kwa wengi wetu tunaamini umefail to deliver the promise for the past 50 years. Kwa nini CDM, CUF na vyama vingine visiunganishe nguvu na kuondoa mfumo uliopo sasa.

  Navyoona CCM wana take advantages ya utitiri wa vyama vingi visivyokuwa na mashiko and then its easier to defeat them when comes to election. Rai yangu lets have dialogue on this kama kweli lengo letu sote ni kuleta madiliko ya kweli kwa mtanzania ili aweze kuishi kwa TANZANIA YA NDOTO YAKE!
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Si rahisi mjomba CCM lazima watie mkono ili viparaganyike.
   
 3. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Lengo ni moja mkuu Karim Wade, ila sera/itikadi za vyama zinatofautiana..unakumbuka mwaka 2002 NARC ya kule Kenya ilivyokuwa? walijitahidi kuficha ubaya, uovu na tofauti zao angalau "kwa muda" na kuiondosha KANU, sasa hivi, ni historia..maslahi ya Taifa kwanza.

  So, nadhani itawezekana ila shida inakuja kwetu wananchi watu wanawaza nani awe Rais, Makamu, W/Mkuu, Mawaziri n.k kwa hisia fulani tu kuwa Chama fulani kina washabiki/wafuasi/wanachama wengi!!!

  Kama, tukificha tofauti zetu tukasimama pamoja, haijalishi nani atakuwa nani, vinginevyo wote watabaki kugombania nafasi ile ambako Hayati Mwl JK Nyerere alisema, "Ikulu si mahali pa kukimbilia"..na hakuna atakayeweza kupafikia, Not in this life time.

  BTW, i liked the Thread title mkuu.
   
 4. m

  mamajack JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  vyama vingi ni vya mamruki,kama kina mbatia na cheyo na wenzao,
  wapinzani waliokuwa wa ukweli walikuwa CUF amabap walifunga ndoa na ccm 2010.
  kwa hiyo kuunganisha hivi vyama ni bomu na hatutafanikiwa.
  only with CDM TUTAIKOMBOA NCHI HII MIKONON MWA WANYANG'ANYI
   
 5. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hoja nzuri km hii mazuzu wanakua kimyaaaaaaa
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tatizo hapa ni udini tu, hiyo inaitwa live bila chenga. CUF%+CHADEMA%=Perfect (100%). watu hawajajua tu hilo. ni rahisi kwa huku bara NCCR-manunuzi kuingia madarakani kuliko chadema au CUF as an individual. conclusion, acha Magamba waendelee kupeta mpaka tutakapojua jibu nililotaja hapo juu.
   
 7. K

  KINUKAMORI Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mada ni nzuri, ingependeza na kwa vyovyote nguvu ingeimarikwa kweli kweli kung'oa chama tawala, tatzo mwana jf mwanzangu kila mtu anataka awe rais, hapo ndo pagumu
   
 8. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  uko right sana
  cuf-majority ni waislam
  cdm-majority ni wagalatia
  mchezo ndio uko hapo.otherwise ingewezekana na wangefanikiwa.
   
 9. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani jf ni mali ya upinzani????? Kwani upinzani ni kupinga bila hoja????? Hivi aliyepo ameshindwa nini, na ajaye ataleta nini??? Naamini, mabadiliko yangewezekana kama 2015, tungekuwa na katiba mpya, yenye kuwa na ufumbuzi wa tume ya uchaguzi. Kama hilo lingewezekana, naamini 2015 tungepata utawala mpya, tukaona lipi jipya ambalo lingewaletea watanganyika maisha tofauti na haya.
  Kwa bahati mbaya, 2014 katiba mpya itapigiwa kura, na wengi wataikataa, na hivyo tutaingia kwenye uchaguzi wa 2015 na katiba ile ile ya siku zote, na tume ya uchaguzi ile ile, watakao penda kuandamana kupinga, tutawapa hati miliki ya maandamano, ili waandamane hadi jangwani.
   
 10. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Huwa napata shida sana na hoja hizi za kidini kuzielewa, hivi waislam wengi wapo CUF kwasababu ya sera za CUF zimekaa Kiisalam zaidi au kwasababu viongozi wake wengi ni Waislam? Mwenye jibu la hili tafadhari, before 2000, CUF ilikuwa ndio Mbadala wa NCCR manunuzi, hata Wakristo wengi pia walikuwa wagombea kwenye chama hiki, huwa sielewi nini kilichomtokea Rwakatale kwenye ule mkutano mkuu pale Morogoro na pia napata hofu sana na hatima ya Julius Mtatiro kama Waislam wengi waamini kuwa hiki ni chama chao.
   
 11. A

  Alhabaad Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cdm hawa waendesha madisco na kuiba wake za watu???au chadema ipi!
   
 12. k

  karim wade Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF: Lets be analytical in our thinking, huu unaosemwa UDINI ni mtaji tu wa wanasiasa lakini ukiangalia kwa sisi wananchi wa kawaida religion has not divided us as politician they are trying to publicise it. Nakumbuka 2010 wakati mkuu analiitubia bunge aliongelea nyufa ya UDINI after 2010 election, but sincerely sijui huo udini kwetu sisi wananchi wa kawaida upo wapi wanaouongelea.

  Tatizo ni palepale its just a game ya kututoa kwenye hoja ya msingi ya ile Tanzanian dream tunayoitaka sisi ambayo for 50 years has not been accomplished. Lets discuss as Tanzanian kwamba tunaitaji direction mpya no matter who your. Ili watoto wetu na wajukuu wetu watukumbuke kwa maamuzi magumu ambayo this generation naamini tunaweza kuyafanya "LETS JOIN THE FORCE AND TOGETHER WE CAN"
   
 13. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hata mimi leo nikawa najisemea hizi mada za udini zinaletwa humu kutuparaganyisha tu. In actual fact hatuna uhasama wa udini
   
 14. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,335
  Likes Received: 10,416
  Trophy Points: 280
  Mimi ninavyojiuliza hapa. Ikitokea wakaungana nani atakuwa rais? Bungeni tu! kwenye kambi ya upinzani hawaelewani je wakiungana itakuwaje?
  Nani atakuwa raisi kati ya hawa?
  1. Mbowe
  2. Lipumba
  3. Mrema
  Hawa jamaa wako na uchu wa madaraka
  Liniwahi kumsikia Lipumba akisema yeye hataki nyazifa ndogo ndogo
  Hebu tufikirie.
   
 15. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Katiba mpya huenda ikaja na utaratibu mpya wa kumpata mshindi kwenye uchaguzi ujao 2015. Kwa mfano, vyama vinaweza kushindana na ikibidi kuungana katika uchaguzi ili kupata kura za kutosha baada ya kushindikana kwenye raundi ya kwanza - kama ilivyotokea Uingereza ktk uchaguzi uliopita.

  CCM ingependa kukiona CUF kinaimarika kwani siku ya siku ikibidi kuunganisha nguvu wao ni wenzao. Kwa mantiki hii, sijui CDM kikitakiwa kuunganisha nguvu na chama kingine itakuwaje.....maana wao kwa sasa wamevimba vichwa na kujiona kuwa wameshafika Magogoni.

  Ukweli unabaki kuwa, pamoja na M4C, Operesheni Sangara, Bla-blaa,...... si rahisi CDM kuwashinda CCM + CUF.
   
 16. K

  KINUKAMORI Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi jamani mwana jf nashindwa kuweka kikatuni changu kwenye avatar napenda sana vinavyo apear mwenye ujuzi jamani anielimishe
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ubinafsi na umimi umetawala Tanzania.
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Sikubaliani na mleta hoja kwamba vyama viungane kwa sababu lengo ni kuiondoa CCM. Kuwa upinzani siyo sababu ya kuamini kwamba wapinzani wako wote mna malengo sawa! Rudi shule ujisomee zaidi mambo sirahisi hivyo,achana na propaganda za kizamani za CCM.
   
 19. m

  mamajack JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kwani wewe unajua cdm ip????na wewe iba hao wake za watu tukuone.cdm ni chama cha watanzania wote,sasa hao wapiga madisco ulitegemea wakaibe ili wajipatie kipato,kanawe uto tope machoni.
   
 20. A

  Alhabaad Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema hawawezi kubali cz wana agenda ya kuendeleza mfumo kristo ulioasisiwa na baba yao wa taifa!!
   
Loading...