Kwanini tunashusha bendera yetu ya Taifa?

Nimekaa nikajiuliza hivi kuna sababu gani bendera ya taifa letu la Tanzania kupandishwa asubuhi ya SAA kumi na mbili na kushushwa jioni ya SAA kumi na mbili?
**Hoja hapa inamaanisha ikifika hiyo SAA kumi na mbili nchi ya Tanzania inakuwa haipo?

**Utambulisho wetu muda huo mpaka kesho yake asubuhi unakuwa ni nini?

**Wenzetu nchi kama ya Marekani hawashushi bendera yao siku zote za wiki,mwezi wala mwaka,bendera yao inapepea siku zote 365 usiku na mchana.

**Sioni haja ya kuishusha bendera yetu ya Taifa katika maeneo yote inapokuwapo.
Duh!
 
PIa iwepo amri ni marufuku kupandisha au kushusha bendera ya Nchi ukiwa umevaa ndala! BALI ya ccm wanaweza shusha au kupandisha na ndala.
 
Swali la Nyongeza:-

Iweje basi kwenye mkesha wa Mwenge bendera hiyo hiyo ya Taifa haishushwi? Pale hupepezwa usiku kucha. Why?

Maswali haya yangejibiwa vizuri na watu wa Itifaki.
 
Is it semantical to use historical instead of history?
Hata mimi nililiona kosa hilo lakini ilibidi nipite tu nikizingatia aliyepost yupo kwenye umoja wa kupinga kila kitu. They never appreciate even when corrected in their common mistakes.
 
Mimi binafsi japokuwa sio mtaalam wa protokali nafikiria kuna simple logic ya kuishusha bendera kila siku badala ya kuipandisha milele.

Ni kwamba, kile ni kitambaa. Kinapeperuka kutokana na upepo. Upo uwezekano wa kitambaa hicho kuchanwa na upepo mkali. Na pia upo uwezekano wa kitambaa hicho kuchoka tu na kuanza kuchanika kidogo kidogo. Sasa badala ya kuiacha ichanike hadi ianze kuning'inia ovyo ovyo vipande vipande, jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kuwa ni uchovu wa nchi, basi ndio maana kuna kuishusha kila siku. Ni katika kuishusha huko ndiko wahusika wanapata nafasi ya kuitazama kama ina kasoro zozote na kuzirekebisha mara moja. Ikiwa itashindikana kurekebishwa basi kesho yake alfajiri hupandishwa nyingine isiyo na kasoro.

Ni mtazamo wangu huu wa kienyeji kabisa na wala sio mtaalam wa itifaki mimi.
 
440px-Flag_of_Zanzibar.svg.png
 
Haahahahahaaaa, yaani ni shida sana maana hata kiswahili hatujui. Mimi kuna mzungu alinitoa nishai wakati tunagonga kiswahili hadi aibu.
Kiswahili hatujui, kiingereza tunacholazimisha ni Mungu tuhurumie basi ni taabu tupu
 
Hivi ukiwa na bendera yako tofauti na ya Taifa na isiyo ya kisiasa kwa Tanzania na yenyewe unatakiwa uishushe usiku?

Au bongo hairuhusiwi kuwa na bendera binafsi kama ya kampuni kwa mfano?
 
Hivi ukiwa na bendera yako tofauti na ya Taifa na isiyo ya kisiasa kwa Tanzania na yenyewe unatakiwa uishushe usiku?

Au bongo hairuhusiwi kuwa na bendera binafsi kama ya kampuni kwa mfano?
Hakuna pingamizi la kumiliki bendera binafsi.
 
Mtoa mada
Kwanza nikupe historia fupi kuhusu bendera.
Matumizi ya bendera yalianza miaka mingi huko nyuma hasa kwenye mapambano na mapigano ya kivita.
Nchi nyingi zilianza kutumia bendera katika karne ya kumi na nane.
Aina ya bendera,namna ya kuipandisha na kuihifadhi inaongozwa ni swala la kiprotokali zaidi.
Zipo protokali ambazo nchi zote zinafuata.
1. Bendera kuwa na umbo la mstatiri
2. Nguzo ya bendera kuwa wima
3. Heshima na matumizi stahiki ya bendera

Kuna mengi ila kwa sababu ya muda nitamalizia mengine nikifika ofisini.
Tuje kwenye swali
Bendera Za taifa zina mambo makubwa mawili
1. kuonyesha uhuru wa nchi na utambulisho wake.Ukiwa UN hutakuta bendera ya Zanzibar kwa kuwa UN haiitambui Zanzibar kama nchi.
2. kuonyesha mamlaka
Kupandisha bendera asubuhi na kuishusha jioni inafanywa hivi kwa mazoea ambayo nchi nyingi imekuwa nazo.
Bendera kwa kuwa ni alama inapaswa kuwekwa mahali ambapo itaoneka na muda ambao itaonekana.
Hivyo nchi nyingi hazipeperushi bendera usiku kwa sababu ya giza. Mfano India pia wanashusha bendera usiku.
Mfano Marekani wao kama bendera inapepea usiku basi hilo eneo lazima liwe na mwanga wa kuifanya bendera hiyo ionekane la sivyo lazima ishushwe. Kwa waliofika Marekani watakubaliana na mimi hapa.


Note. BENDERA kushushwa usiku haina uhusiano wowote na mamlaka ya Rais wala Jeshi la Ulinzi ni utaratibu wa kiprotokali usioathiri nguvu wala majukumu ya Rais ama taasisi yoyote ya Serikali.

Nitarudi baadaye.
naamini jibu sahihi ni hili hapa, ila mkuu swalo nyongeza kuna hoja humu kuwa bendera za jeshi hipandishwa jioni nankushushwa asubuhi, unaweza fahamu kwani inakuwa hivyo
 
Kuanzia saa 12 asubuhi, mpaka saa 12 jioni nchi inakuwa kwenye himaya ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndiyo maana ikifika muda huo siyo bendera ya Taifa tu, bali hata ile ya Rais huwa inashushwa kuashiria kuwa sasa TPDF Tanzania people defence foces nchi ipo kwenye himaya yao na bendera ya mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi inapandishwa mara moja.
Hili jibu linajitosheleza kabisaaaa...
 
Kuanzia saa 12 asubuhi, mpaka saa 12 jioni nchi inakuwa kwenye himaya ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndiyo maana ikifika muda huo siyo bendera ya Taifa tu, bali hata ile ya Rais huwa inashushwa kuashiria kuwa sasa TPDF Tanzania people defence foces nchi ipo kwenye himaya yao na bendera ya mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi inapandishwa mara moja.
Hili jibu linajitosheleza kabisaaaa...
 
Na yenyewe bendera binafsi inatakiwa kushushwa na kupandishwa mawio na machweo?


Kushusha au kupandisha bendera binafsi ni uamuzi wako tu ukitaka hata wakati wa kula shusha nusu mlingoti na ukienda chooni shusha kabisa ni wewe tu. kumbuka hiyo unayoiita kuwa bendera binafsi kwa wengine ni daso kama yalivyo madaso mengi tu hakina maana yeyote.
 
Back
Top Bottom