Kwanini tunapeleka wanajeshi wetu badala ya Mwenge?

Kwanini tunapeleka wanajeshi wetu badala ya Mwenge?

Wanajeshi kwenda kulinda amani ni miradi ya mataifa makubwa na lengo huwa sio kumaliza machafuko nafikiri mkuu una uelewa mdogo juu ya maigizo ya wanasiasa. Vilevile kwenda kulinda amani ni dili kubwa sana kwa wanajeshi na vikosi vingine,kupata chansi ni mpaka uonge,au kuna mkubwa anakujua hivyo akushike mkono,ukijua maslahi wanayoyapata hata na wewe ungetamani sana kwenda kule. In short kule hawaendi kupigana kama unavyofikiria.
Pesa na uhai kipi bora.
 
Si CCM wanasema tusipokimbiza mwenge machafuko Na Vita vya wenyewe kwa wenyewe itatokea!!!
Basi ao ccm wanaosema uo ujinga ni wajinga lakini wale wanaoambiwa uo ujinga nakukubali wa watakuwa wajinga zaidi.
 
Panapo tokea machafuko nchi mbalimbali Duniani, Tanzania imekuwa mstari wa mbele kupeleka wanajeshi wake wakalinde Na kuboresha amani.
Mazingira hayo Siyo rafiki. Ni nusu Vita kama sio Vita kamili.
Kwenye mission mbalimbali tumepoteza askari wetu ambao ni tegemeo kwa Taifa Na familia zao.
Tunao Mwenge wa Uhuru. Na Tunaambiwa amani Na utulivu vilivyopo nchini ni matokeo ya kuukimbiza mwenge nchi nzima.
Kwanini tusiukimbize mwenge kwenye nchi zenye machafuko kama Sudan Kusini, Congo etc ili wawe Na amani Na hivyo kuwaokoa askari wetu Na hata wenyeji wa hizo nchi?
Maoni Na majibu yenu ni muhimu.
swissme, BAK, mshana jr, Pascal Mayalla, Nyani Ngabu, Mzee Mwanakijiji, GuDume, CCM, CHADEMA
Mwenge nadhani ni dhana mficho ya Taifa.! "sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro ili ulete tumaini........"..
Nukuzi kutoka katika Maneno ya Mwl Jk nyerere.

Natumai kila Taifa lina dhana yake mficho kwa ulinzi wa ama imani au Utaifa wao.! ukiaenda usie husika ukajaribu kufikiri waweza ona ni kama upuuzi tu.
mathalani kifimbo cha malkia kwenye olimpiki kina sabbu gani yakuzungushwa kwenye Nchi za madola?
au kile kinachoitwa mwenge wa olimpiki
ni dhana yake?

Ukienda China kuna jambo wanaliamini katika dragon toka kizazi kimoja kwenda kingine ukienda mgeni je dragon lao lina jambo lolote muhimu kwako?

Ukiangalia kwa mtazamo wa pesa utaona ni hasara lakini ukiangalia kwa Dhani ya Uhai wa Imani ya Kizalendo kwa Taifa ni kubwa sana.! Kwa kizazi kijacho labda tu ukiwa sio Mtanzania wa kweli jambo hilo linaweza kukusumbua.

Amani katika mataifa yenye machafuko. Huenda ni jambo la kisiasa zaidi ya kimani. Mathalani kulikuwa na haja gani ya Libya kuingia kwenye machafuko ?
Je UN hawakujua madhara ya Libya kwa siku za Mbele?
au Machafuko ya Syria UN hawajui sabbu za machafuko hayo?
the same DRC congo je UN hawajui..?

La hasha ni miradi yao wanayoitengeneza kwa manufaa yao wenyewe so sio uimara wa jeshi unaohitimisha migogoro katika Nchi zenye machafuko ila ni dhana. Iliyopandwa ndani ya fikra zao.!
ambayo yaweza kupandwa kwa kuaminishwa kuwa hawa wanapendelewa kuliko hawa na wale wananyanyaswa kuliko wale.
Wakishaanza kushambuliana walio wachonganisha wanapata wanachokitaka.!

Hivyo dhana ya Mwenge wa uhuru ni kuwakumbusha watanzania umoja wao na usawa wao ambao waweza kuondolewa na baadhi ya watu kwa kisingizio cha kisiasa.! Ambacho ukichunguza chanzo chake halisi sio ndani Ya Taifa letu..

"Kuwasha Mwenge na kuuweka Juu ya mlima kilimanjaro"

RIP.. Jk Nyerere..
RIP ... Nyirenda..

Kizazi kijacho kinachotafuta ukweli kitagundua siri hii.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wanajeshi kwenda kulinda amani ni miradi ya mataifa makubwa na lengo huwa sio kumaliza machafuko nafikiri mkuu una uelewa mdogo juu ya maigizo ya wanasiasa. Vilevile kwenda kulinda amani ni dili kubwa sana kwa wanajeshi na vikosi vingine,kupata chansi ni mpaka uonge,au kuna mkubwa anakujua hivyo akushike mkono,ukijua maslahi wanayoyapata hata na wewe ungetamani sana kwenda kule. In short kule hawaendi kupigana kama unavyofikiria.
Mwaka mzima unahatarisha maisa yako kwa mil 40.
 
Mkuu umewaza mbali sana, mi ninachokishuhudia kwenye kukimbiza huo mwenge ni ngono na ulevi tu na sidhani kama unaleta amani kamwe!
 
Hukunitag km hao wengine. So I will not comment here though is a good qn
 
😀😀😀😀
naunga mkono hoja!
 
Back
Top Bottom