mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Juzi Taifa limepata msiba kwa kupotelewa na mkuu wa Freemason Tanzania kama sio EA mzee Chande. Mkuu wa Taasisi/Club/Dhehebu ambalo Mkuu wake anafahamika lakini waumini au members zake hatuwajui. Duniani kote kuanzia miaka ya 2000 mashambulizi misikitini,makanisani,kwa waganga, Wasanii wafuatiliaji wa mambo wamekuwa wakiishutumu Taasisi hii kama ni ya kichawi, hatari,haifai, Yenye nguvu isiyozuilika.
Sasa leo tunagundua kumbe kiongozi wa taasisi hii pingwa, ni Mtu mzuri, anamchango mkubwa kwenye jamii, hajawahi kukutwa hata na chembe ya shutuma, hata wanaomfahamu wakimuelezea kurasa hata 1000 hutachoka kumaliza wasifu mzito wa mtu huyu mashuhuri.
Wajuaji wa mambo mtusaidie, Tuchukue Freemason Ipi, Ile Inayopodwa mitaani,Mitandaoni,makanisani,Misikitini,waganga, Uswahilini hofu ya freemasonry ndio usiseme, Humu JF, au Hii ya Mzee Chande ambayo imewaunganisha wanasiasa wa upinzani, watawala na watawaliwa kumlilia. Hii ambayo viongozi wetu wote toka nyerere walikuwa wakimpenda na kuwa karibu na kiongozi wetu...
Ninaandika nikiwa na OMBWE la maharifa juu ya hii taasisi lakini ninauhakika wa Hofu(wenda ya kweli au ya kutengenezwa na wajanja wachache mitaani kwa manufaa yao) juu ya taasisi inayosadikiwa kuwa tata na ya siri iliyotapakaa Dunia nzima na inayosemekana ilianza miaka 1600BC kwa mujibu wa Uzi wa mkuu wetu wa JF Melo Freemasons Inside - Out: Who are they? How they operate? How to join them?
karibuni wadau mtutoe tongotongo sisi wa vijijini...
cc: Magazeti ya leo
Kanumba ahusishwa na mambo ya freemasonry kutokana kupishana siku moja na mkuu wake katika kifo (Gazeti la UDaku)
Mwananchi:Zitto amlilia kiongozi wa Free mason kuzikwa J4.
Mtanzania, Siri kifo cha kiongozi wa freemason
na mengine mengi yakionyesha masikitiko yake juu ya kupotelewa na mtu huyu mashuhuri nchini.