GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Tende ni kati ya matunda ninayoyapendelea sana. Nilianza kuyatumia kwa kuvutiwa na ladha yake, sikujali sana faida zake kiafya, na wala sikuwa nikizifahamu.
Ni hivi karibuni, tena kupitia nyuzi za humu Jamii Forum, nilifahamu kuwa tende si tunda lenye ladha nzuri tu, bali pia lina faida lukuki kiafya.
Lakini kuna taarifa zilizonishangaza! Kuna watu wanachukulia tende kama chakula cha Waislamu, tena cha wakati wa mfungo wa Ramadhani. Kwa nini watu wamekuwa na mtazamo huo?
Mimi nafahamu, kama sikosei, kuwa Waislamu hupendelea pia kula wali, mihogo, viazi vitamu, n.k. kipindi cha Mfungo. Itakuwa ni sahihi kusema kuwa mihogo na viazi ni chakula cha Waislamu?
Nimeangalia mtandaoni. Tende zinalimwa nchi kadhaa za Asia na zisizo za Asia. Kote huko zinalimwa kwa ajili ya Waislamu?
Hizi ni baadhi ya nchi zinazolima tende: SAUDI ARABIA, IRAN, MOROCCO, MISRI, ISRAEL, CHINA, MAREKANI, QATAR, NIGER, PALESTINA, ALGERIA, OMAN, UNITED ARAB EMIRATES, ALBANIA, MEXICO, SPAIN, UNITED STATES OF AMERICA, CAMEROON, KENYA, BENIN, COLOMBIA, n.k.
Sijaona popote palipoandikwa kuwa tende ni kwa ajili ya Waislamu!
Watu wanaovumisha kuwa tende ni chakula cha Waislamu wana nia gani? Wanataka kuwakosesha wasio Waislamu virutibisho vinavyopatikana kwenye tende?