Kwanini Tanzanian Writers, Wasiandike Movie Scripts | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Tanzanian Writers, Wasiandike Movie Scripts

Discussion in 'Entertainment' started by sun wu, Sep 16, 2012.

 1. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuchoka kuangalia ma-Cadillac, na AK-47 na Movie ambazo hazina uhalisia na Bongo, na kuwakumbuka watunzi mashuhuri kama Agoro Anduru (Temptations, Bed of Roses na This is Living..) na watu wenye style ya kuandika ya ki-Tanzania kama Chesi Mpilipili.. alafu nikarudi tena kuangalia movie za kibongo ambavyo hazina substance nikajiuliza......

  Wabongo hawapendi kusoma.., ila kuna watu wana talent ya kuandika na kupangalia stories na dialogue, hivyo kwanini kina Chesi et al badala ya kuandika vitu ambavyo vinaishia kufungiwa maandazi na kupata vumbi kwenye bookshelves.., wasiandike movie scripts maybe just maybe movies za Kibongo zitakuwa more watch-able, na badala ya kuangalia movies za sijui CIA kafanya nini na Terrorist wa wapi.., tutaona movies za vipi machinga anasomesha watoto na kuwalea wazazi wake huku anapigana chenga na mama mwenye nyumba, au maybe Mkwawa itakuwa a blockbuster kama ilivyokuwa Shaka Zulu
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Good idea....
   
 3. Pianist

  Pianist JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe kuwa filamu nyingi za kitanzania hazina substance na haziko watchable. Lakini inabidi ujue ili movie kuwa nzuri si tu script pekee inayotakiwa kuwa bora bali kuna vitu vingi zaidi. Nyingi ya hizi ukiangalia unajua kabisa hapa kuna mtu anaigiza yaani uigizaji hovyo, dialogue hovyo, sauti, mavazi, upigaji picha, uongozaji na uandaaji. Movie nyingi ni za kulipualipua, unakuta mtu kwa mwaka anaandaa movie 12 na zote yeye ni mhusika mkuu na producer na muongozaji.
  Lakini lengo la kuigiza ni kufanya biashara na movie itakayotoka hapo iweze kuuzika isiwe hasara, hivyo ndo maana tunaona movies nyingi za 4weeks na 20m budget. Hakuna utaratibu mzuri uliowekwa na serikali wa kusimamia usambazaji wa filamu hivyo si rahisi kuinvest 2years and a big budget for one movie.
   
 4. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna ukweli unachokisema ila unaweza ukatumia a small budget na bado movie ikawa bora, alafu pia inabidi kuangalia buying power ya wabongo peke yake na sababu ya piracy ni vigumu kutegemea hili soko ili uweze ku-return investment yako, wenzetu nje hawategemei soko la video tu.., bali matangazo, sponsorship, kuuzia tv networks na kuuzia majumba ya cinema.

  Hivi swali linakuja..., hawa TBC, ITV, Star TV huwa wanalipia zile tamthiliya kama prison break, 24, Egoli, na zile za Asia..? kama wanalipa huoni kwamba maybe soko kubwa zaidi sio kumtegemea mtu wa mwisho kununua DVD yako ili upate pesa bali pesa ya nchi nchi ni kuuzia some rights kwa hizi TV.., ?
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Waandishi na waigizaji wa filamu tulio nao sasa ni njaa kali. Hakuta vipaji ujuzi wala kujituma zaidi ya umaarufu wa shilingi mbili. Wazo lako bomba ingawa nina shaka kama watanzania watazipenda kutokana na tabia ya kupenda udaku. Sometimes hawa watunzi wanaangalia upuuzi wanaopenda wateja wao. Leo hii magazeti ya udaku kuanzia wa nyumbani hata kwenye majengo ya ibada vimetawala. Angalia magazeti hayo ya udaku wa kidini na kifamilia yalivyoshamiri.
   
 6. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu usemayo lakini hata kama ni udaku hivi kweli wabongo wanashindwa kujipanga na kutengeneza series kama Isidingo ya kibongo, ambayo itakuwa inacheza kila siku kwenye TV fulani ?, na hapa kama itakuwa ni bora nina uhakika TV (ITV, TBC, n.k.) watagombana ili kuipata sababu na wenyewe watapata matangazo na sponsorship.., kwahio hata kama ni huo udaku utengenezwe realistic na uwe na connection na maisha ya bongo ambayo mtanzania anaweza ku-associate.., kwanini prime time kwenye tv badala ya watu kuangalia isidingo kunakuwa na series ya maana ya kibongo, na sisi maybe tuweze hata ku-export hata Kenya na Uganda (more money for wasanii), watu kama wale Bishanga, Jangala na Kina mzee Jongo (yaani pure utanzania ambao watu wanaweza ku-associate)
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu ni kutopenda kusoma vitabu na kuchangamsha akili,...how could we think and do differently
   
 8. P

  Paul S.S Verified User

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Waandishi wa vitabu na waandishi wa scripts za movies ni watu wawili tofauti kabisa

  Movies zinatengenezwa kutokana na vyanzo mbalimbali vya story(matukio), inaweza ikawa kutokana na tukio la kweli, au matukio ya kubuni au kutoka kwenye vitabu vya hadithi

  Sasa kilichopo bongo ni kwamba waandaaji na watengenezaji wa film zetu ndio hawataki kutumia stori za kwenye vitabu

  Mfano James Hadley Chase katika vitabu vyake zaidi ya tisini vitabu hamsini vimetengenezewa movies na watu wa film
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  wapo watu
  tatizo tunawadharau

  kulikuwa na tamthilia tbc zamani
  3 days kwa wiki ilikuwa inaitwa Jumba la dhahabu..
  ilikuwa a very good starting point
  watu wa FEMINA pia wana utaalamu wa series na film
  hawatumiki....
   
 10. P

  Paul S.S Verified User

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Waandishi wa vitabu na waandishi wa movie scripts ni watu wawili tofauti kabisa

  Tatizo ni kwamba waandaaji wa films za kibongo hawataki kutumia vitabu vya kibongo kama vyanzo vya stori zao, wamekazana na zakutunga wenyewe
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama wakiandika Isidingo, take it from me, watanukuu na kutafsiri Isidingo kiasi cha kukera na kutia kinyaa na hapa ndipo utakapojua kuwa nchi yetu imo msambweni kiakili na kisomi.
   
 12. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu kitabu ni tofauti na movie script.. (sababu movie script inabidi ielezee kila kitu kinachotokea, mazingira dialogue n.k., kwahio inakuwa more elaborative) sasa sababu movie za kibongo haziendi kitaalamu kwanini waandishi ambao nina uhakika wanaweza kuandaa dialogues bora zaidi wasitumike ?

  Ukizingatia kwenye kuandika kwao income stream sio kubwa kivile kwanini wasitumie hii outlet nyingine ya kuandika scripts.., Pia kuchukua story ya mtu kama kitabu n.k. kuna issue za kugawana % ambazo huenda ndio maana actors wanaogopa, sasa kwanini mfano mtu mwenye kitabu chake tayari yeye mwenyewe asibadilishe kwenye movie script ya maana na kuwaita wasanii na kufanya nao kazi in collaboration alafu wakagawana mapato mwisho wa siku ? Binafsi naona input ya waandishi kwenye hii tasnia italeta tija zaidi, ninao uhakika mtu anayeandika kitabu hawezi kushindwa kukaa na wasanii na kuwasaidia kuandika script kuliko sasa hivi ambavyo msanii anabeba mizigo yote
   
 13. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,485
  Likes Received: 5,961
  Trophy Points: 280
  kuna baadhi ya movie wameandaa watu wa chuo cha sanaa bagamoyo zinamaongezi yenye akili sana na story inampangilio mzuri,tatizo la wabongo kujidai kujua kilakitu
   
Loading...