Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kwa utambulisho Biafra ni jina la eneo ambalo lilitaka kujitenga na nchi ya Nigeria, ambapo kwenye miaka ya 60' lilianzisha (Biafra) jaribio kubwa lililopelekea vita kubwa kutokea kati yake (Biafra) na nchi ya Nigeria ambapo mwishowe nchi ya Nigeria ilifanikiwa kuishinda Jamhuri ya Biafra na kuiunganisha tena na nchi ya Nigeria!
Lakini kilichonifanya niandike Mada hii ni ushiriki wetu kwenye ile vita ambapo sisi kama nchi tulichukuwa upande wa Biafra na nchi yetu ilikuwa ni moja kati ya nchi chache zilizoitambua Jamhuri ya Biafra kama Dola kamili, sasa ni kwa nini? Kuna anayefahamu sababu za nchi yetu kuitambua Jamhuri ya Biafra au kuwa upande wa Biafra na siyo upande wa Nigeria?
Kwa maana nifahamuvyo ni kwamba sisi chini ya Mlm.Nyerere sisi tulikuwa ndiyo wapiga debe wa Muungano wa Afrika (Pan -Africanism) sasa iweje tuwe upande wa watu wanaotaka kujitenga (Biafra) na siyo upande wa wanaotaka kuungana (Nchi ya Nigeria)?