mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Kumekuwa na utata mwingi kuhusu utaifa wa Rais wa Gabon wa sasa Ali Bongo Ondimba. Hapo awali wanasiasa nchini mwake walimtaka Rais huyo kuwasilisha kipimo cha DNA ili kuthibitisha kuwa kweli yeye ni mtoto wa marehemu Rais wa nchi hiyo Omar Bongo Ondimba. Inadaiwa Rais Ali Bongo Ondimba alikataa kufanya vipimo hivyo.
Madai haya yalikuja baada ya mwandishi wa insha Mfaransa na mtaalamu wa Gabon, Pierre Pean kuandika katika kitabu chake kiitwacho "New African Affairs" kwamba rais wa Gabon ana asili ya Nigeria.
Mwandishi huyo anadai kuwa babake rais, Rais wa zamani Omar Bongo alimleta Ali Bongo kutoka Biafra wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria.
Kuna picha imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Rais Ali Bongo Ondimba akiwa katika mazingira duni na afya duni akionekana kuwa na utapiamlo.
Picha/Maelezo: Anayedaiwa kuwa Rais Ali Bongo aliyezungushiwa kiduara akiwa kwenye kituo cha watoto yatima kabla ya kuasiliwa na Hayati Omar Bongo