Kwanini Tanzania inapokea watalii milioni 2 tu?

Kwanini Tanzania inapokea watalii milioni 2 tu?

Kwa hapa Africa nchi gani? Maana Tanzania ni ya 6 kwa watalii, just next after Kenya
Hata huko Asia kuna nchi hazifikii Tanzania kwa vivutio vya utalii lakini wanapokea watalii wengi kuliko sisi
Jeshi la Tanzania una amini lipo kwenye top Ten ya majeshi duniani na africa ?
 
Jeshi la Tanzania una amini lipo kwenye top Ten ya majeshi duniani na africa ?
Hapana, siamini. Maana sijaona vitu vya kufanya jeshi la Tanzania lifikie hizo nafasi
Lakini kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vinaonekama na vinastahili watalii wengi zaidi
 
Watalii wanaangalia vitu vingi, moja ya vitu wanavyoangalia ni mbuga za wanyama. Vivutio ni vingi
Na Tanzania ina offer more than mbuga za wanyama.
Achana na mataifa kama France ambayo yanapokea hadi 90M tourists. Kwa vivutio vya Tz ilipaswa tupokee watalii hata milioni 10

60% ya watalii wanaokuja tanzagiza wanaenda beach zanzibar, kwa maana nyingine wanakuja kwa sababu ya beachnzuri zanzibar ...
 
ili tufahamu tunakwama wapi,napendekeza maeneo ya vivutio na viwanja vya ndege waweke 'BOX LA MAONI',lazima watalii watasema Tanzania tunakwama wapi.
 
Sasa Tanzania miji yetu ina nini cha ku offer surely?
TZ bado haijafunguka logistically.

Watalii wenginm tunaopokea ni NICHE tiurists, wanaokuja kwa SAFARI au kupanda Mlima Kilimanjaro.
 
Kijakazi acha kupotosha watu wewe
Hifadhi mbili tu za taifa zinapokea takribani watalii milioni 1.4.
Hizo ni 2 peak, bado hujaongelea hifadhi nyingine
Haya ya 60% kwenda Zanzibar umeyatoa wapi
Zanzibar ina receive watalii wengi, na maeneo mengine yanapokea watu wengi pia
Screenshot_20260327-231110.png
Screenshot_20260327-230933.png
 
Utalii ni zaidi ya kuona wanyama.Ulo Pattaya Thailand watalii wanamiminika kama maji.
Utalii ni vitu vingi, including kuona wanyama
Duniani wapenzi wa nature ni wengi sana, saaana. Tena tu nature za kawaida kama misitu na maporomoko ya maji watu wanapenda, sembuse mbuga za wanyama?
Halafu Tanzania ni more than mbuga za wanyama. Kama hujui vivutio vya Tanzania sema nikuorodheshee list.
 
Gharama za utalii Tanzania zipo juu sana wanaenda sehemu gharama zipo nafuu ya hapa..
 
Umeuliza swali lakini umejijibu.
Kwanza hatufanyi promotion ya kutosha.
Pili gharama zipo juu tumelenga watalii matajiri wakati unakuta kuna mtu kadunduliza pesa aje atalii lakini anakuta gharama kubwa sana.
Miundo mbinu mibovu hasa barabara za kwenda mbugani mfano kipindi cha mvua ni ngumu kwenda Ruaha National park.
Kuna mgeni wangu alikuwa anakuja toka Poland akawa anataka atembelee visiwa vilivyoko maeneo ya Dar au karibu yake. Nikawa natafuta mtandaoni nilichokuwa naona ni vichekesho unakuta mtu anazungumzia kisiwa cha Mbudya hasemi wapi unapata usafiri wa kwenda Mbudya, gharama ni kiasi gani kwenda huko sanasana utasikia oyaa hapa mbudya , tuko na washikaji zile basic information wanashindwa kutoa.
Kisiwa kingine nafikiri Lagoon gharama ya siku $130 ni nyingi kwa mtalii wa kawaida. Kuna mchina mmoja alikuja toka Hongkong akawa anatuambia kwanini tusiende huko ilikuwa mambo ya biashara alifikia Holiday Inn akatuambia Holidain ya kule ni gharamaa nafuu kuliko Holiday Inn ya hapa.
Kama tungetangaza vivutio vyetu tukaachana na siasa za Royal tour, tukaweka gharama rafiki tungepata watalii wengi ingewezekana tungekuwa tunaongoza Afrika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom