Kwanini Tanzania hatuna biashara zenye mfumo wa chain?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,012
Kwanini hatuna biashara ambayo unaweza ikuta imeenea nchi nzima?
Mfano biashara za wenzetu kama walmart au unakuta kuna pharmacy zimejaa nchi nzima kama Walgreens au CVS.

Unakuta kuna maduka ya electronics, vinywwji. nguo au spare parts yamesambaa nchi nzima. Yanatumia brand moja na quality ya products unakuta ni moja. Kwanini Tanzania hatuna biashara za hivyo.
 
Nchi yenyewe hii uanzishe duka Mwanza uje ufungue huku uweke jina hilo hilo basi hujitakii mema. Figisu figisu. Watu wanakwepa kodi lazima uwe na mbinu za kuikimbia TRA jombaaaa, hii ni sababu mojawapo.

Ipo kampuni naifahamu, Royal Trinity T/A Royal Oven Bakery kwa hapa Dar ipo Tabata, Mlimani, Posta sina hakika na sehemu nyingine. Pia wapo Mwanza na nadhani ndiko makao makuu yalipo.

Chunguza. Mtu analimiki shule za Ujenzi Mkuranga, St Mathew Kongowe ya Mbagala, St Marks ya pale Bakwata Mzinga wanadai na Victory ni ya kwake pia. Kwanini kote huko kaweka majina tofauti? Haya, kamuulize.

Mbona St Marry's zote zina jina moja?
 
Purchasing power ni ndogo mno kuweza kusapoti mfumo kama huo, watu wengi Tanzania hununua mahitaji ya kila siku kama nyanya, chumvi mafuta ya kibaba, mchele wa kupima, unga wa kupima magengeni sasa hiyo chain wataiweza wapi ?
 
Kwanini hatuna biashara ambayo unaweza ikuta imeenea nchi nzima?
Mfano biashara za wenzetu kama walmart au unakuta kuna pharmacy zimejaa nchi nzima kama Walgreens au CVS.

Unakuta kuna maduka ya electronics, vinywwji. nguo au spare parts yamesambaa nchi nzima. Yanatumia brand moja na quality ya products unakuta ni moja. Kwanini Tanzania hatuna biashara za hivyo.
Mkuu ina maana sheli zote za Puma, total, engen nk zilizotapakaa nchi nzima hujawahi kuziona? Benki zote kubwa kama CRDB, NMB, NBC nk si zipo nchi nzima? Huku kanda ya kaskazini kuna mtu anaitwa Panone ametandaza biashara zake za sheli na supermarkets kila mahali na jina ni hilo hilo anatumia. Kabla ya huyo kulikua na Mr Price sijui aliishia wapi. Kuna baadhi ya hotels pia wapo mikoa kadhaa mf Regency na jina wanatumia hilo hilo. Shule pia zipo na kuna biashara ya makanisa ya kiroho ambayo yana branches mikoa karibu mingi.
We sema sio kiviile kama mbele maana wafanyabiashara wetu wengi bado mitaji ni midogo na hawana majina makubwa nje ya sehemu walizoanzia biashara.
 
Mitaji mkuu
 
'Huku kanda ya kaskazini kuna mtu anaitwa Panone ametandaza biashara zake za sheli na supermarkets kila mahali na jina ni hilo hilo anatumia.'

Ila Daah Panone ana hali mbaya sana kwa sasa,mabank yanakimbizana nae kwny mikopo hatari sana.Wanaweza kuja kumfilisi muda si mrefu.
 
Tatizo ni upeo mdogo wa kufikiri na kufanya biashara kimazoea. Financial constraints, risk taking, SME preference and selfishness. Kutanua biashara wanadhani wataibiwa business secrets na hivyo kuleta upinzani in future.
In short, wanaridhika na kuchumia tumbo tu.
 
Mi sijakuelewa! Unamaanisha kwamba biashara zoteziwe Ktk mfumo huo?
Vinginevo hakuna Shida yeyote! Ksbb biashara zote zipo na zinakuwa kutokana na mahitaji ya watu.
 
Back
Top Bottom