Kwanini tangu D29 ushabiki wa mpira wa Simba na Yanga umepungua sana?

Kwanini tangu D29 ushabiki wa mpira wa Simba na Yanga umepungua sana?

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,555
Reaction score
40,749
Hapa tunapoishi jilani siku ya jmosi kama leo kuna vijiwe asubuhi kama leo ndo vinakuamsha kwa mabishano ya mpira wa simba na Yanga, nilikua nawachunguliaga dirishani nikiwa louge, sasa hivyo vikao katika vijue vitatu jirani havipo tena.

Vijana waligundua kwamba wanapoteza sana muda kwa mambo yasio ya msingi wakati wana ya msingi yanao wakabili?

Vijana na watu wazima walihama mtaa au walikufa?
Political awareness imepatikana katika jamii ya kitanzania tangu 29 Oct.
Au hofu ya kukamatwa kwa uhalifu uliofanyika?
 
Timu za kariakoo ndo zinazotumika ku'push agenda za serikali dhalimu na pongezi nyingi kwa mama yao ilhali mashabiki wao wanapitia hali ngumu ya kukandamizwa na hao wanaopongezwa.
Kuna mashabiki wengi waliofariki siku na baada ya dec 29 wakiwa hadi wamevalia jezi za timu hizo lakini hakuna aliyetoka hadharani kutoa hata pole, walijikausha kama vile hawapo.
Girishoni kutumia matamasha yao kumpigia na kutafuta engagement ya samuya ni kama walipoteza kabisa ladha ya mpira wao mazima
 
Kumekua na mfululizo wa matukio mengi ambao umefanya masuala ya simba na yanga yasipewe uzito na raia.

1. Jezi mbovu. Timu zote mbili msimu huu zimetoa jezi mbaya

2. Masuala ya kisiasa. Msimu unaanza ndio kipindi cha kampeni kwaiyo habari za siasa ndizo zitafatiliwa zaidi. Likaja sakata la MO29 yaliyotokea bado yanaongelewa mpaka leo.

3. AFCON. Baada ya hapo imekuja afcon.ikiisha afcon tunarudi epl baada ya hapo world cup.

Huu msimu umaarufu wa simba na yanga umeshuka, bila shaka watakua wamepata hasara ya jezi. Kama faida ipo basi ni ndogo sana ukilinganisha na misimu ya nyuma

Hersi na mangungo wahesabu msimu wamepoteza, wajipange msimu ujao
 
Kumekua na mfululizo wa matukio mengi ambao umefanya masuala ya simba na yanga yasipewe uzito na raia.

Msimu unaanza ndio kipindi cha kampeni kwaiyo habari za siasa ndizo zitafatiliwa zaidi.

Likaja sakata la MO29 yaliyotokea bado yanaongelewa mpaka leo.

Baada ya hapo imekuja afcon.

Ikiisha afcon tunarudi epl baada ya hapo world cup.

Huu msimu umaarufu wa simba na yanga umeshuka, bila shaka watakua wamepata hasara ya jezi. Kama faida ipo basi ni ndogo sana ukilinganisha na misimu ya nyums

Hersi na mangungo wahesabu msimu wamepoteza, wajipange msimu ujao
Hata matukio yote kila msimu yapo ila bado ushabiki wa S&Y unapewe kipao mbele, ila mara hi watu kama wamezira huo ushabiki wa hizo timu, upo ila sio kama siku za nyuma.
 
Hata matukio yote kila msimu yapo ila bado ushabiki wa S&Y unapewe kipao mbele, ila mara hi watu kama wamezira huo ushabiki wa hizo timu, upo ila sio kama siku za nyuma.
Kwamba uchaguzi mkuu na massacre iliyofanyika huwa inatokea kila msimu na habari za simba yanga zinaendelea kutrend?
 
Kwamba uchaguzi mkuu na massacre iliyofanyika huwa inatokea kila msimu na habari za simba yanga zinaendelea kutrend?
Naona hujanipata mkuu naongelea afcon epl siasa na uchaguzi ni wa misimu kila mda fulani massacre ni matokeo ya uchaguzi, naomba unielewe
 
Mwenyewe ni mmoja niliokacha kabisa stor za simba na yanga.

Mimi ni simba ila sasa hivi nimeshasema acha wafungwe kadiri inavyowezekana.

Kama mpira epl, la liga, bundes, serieA zinatosha sana.

Hizi timu za wahuni acha zibakie na wajinga.
 
Waliokuwa wanachagiza hizo mbanga ni pamoja na hao wakina Madelu ambao watu hawataki kuwasikia kabisa.
 
Mimi ni mfano asee,juzi simba na azam wamecheza hata Sina habari sifahamu kama Kuna game.
Hivi vitu vimetuchelewesha sana
 
Ushindani halisi wa Simba na Yanga umepotea kutokana na Simba kutokuwa na mwendelezo mzuri mbele ya timu mbalimbali ikiwemo Yanga na Azam. Mashabiki wake wamepoa na kukosa nguvu ya kubishana na Yanga hivyo ladha halisi ya Simba na Yanga kupotea.
 
Pia matajiri waliokua wanahonga media kuonge ukenge wa club zao wamesepa halimbaya
 
Hapa tunapoishi jilani siku ya jmosi kama leo kuna vijiwe asubuhi kama leo ndo vinakuamsha kwa mabishano ya mpira wa simba na Yanga, nilikua nawachunguliaga dirishani nikiwa louge, sasa hivyo vikao katika vijue vitatu jirani havipo tena.

Vijana waligundua kwamba wanapoteza sana muda kwa mambo yasio ya msingi wakati wana ya msingi yanao wakabili?

Vijana na watu wazima walihama mtaa au walikufa?
Political awareness imepatikana katika jamii ya kitanzania tangu 29 Oct.
Au hofu ya kukamatwa kwa uhalifu uliofanyika?
Nilishasema ushabiki unakufa kabisa ni suala la mda japo wanalazimisha
 
Back
Top Bottom