Kwanini suala la kuunganisha mitaji ni gumu sana? Nini kifanyike?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,499
Moja ya Changamoto inayo wakabili watu wengi ni suala zima la Mitaji ya kufanyia Biashara, Mitaji ni Kilio cha kila mtu, hasa watu ambao hawana uwezo wa kwensa kukopa Benki na pia hata kama uwezo wa kukopa Benki ungekuwepo ila bado mitaji haitoshi.

Wachina niliwahi soma andiko lao moja kwamba unakuta kampuni moja ina share holder 400 wamegawanyika humo humo kuna Wahasibu, Marketing Officer, IT, Wanashera, Wapishi na kadhalika yaani wamekamilika.

Ulaya kipindi Viwanda tunavyo viona leo hii vya madawa na vyakula na kadhalila ni ya Ushirika walianza, walianza kama ushirika na baadae wakatanua na kufungua Makampuni ambazo ziko hadi leo hii.

Tumeona Wasomali wana Umoja sana, wanachangishana Pesa na kufungua kampuni na kweli kampuni husimama, Waarabu hivyo hivyo, Wahindi hivyo hivyo.

Wakenya pia na Waganda nimeona, Binafisi nina rafiki zangu Wakenya wako Tanzania wanafanya mambo ya IT jamaaa walijichanga wako watatu, wakajichanga na kufungua kampuni ya IT, pia wapo ambao nawajua wamejichanga, ingawa kule kwao hii ni kawaida sana, Waganda pia.

Njoo Sasa kwetu Watanzania, yaani hata ndugu tumbo moja pacha ukiwaeleza swala la kuunganisha nguvu hawakuelewi kabisa, yaani hata Kijana kuunganisha nguvu na Baba yake mzazi au Mama yake mzazi bado haiwezekani. Tumekuwa na sababu nyingi sana kubwa kuliko yote ni UMANIFU hii ndo ngao yetu kuu ya kuto kuunganisha mitaji.Lakini mbona kwenye starehe tunaaminiana sana na kuchangishana?

Ni kawaida Tanzania kukuta ndugu wawili Familia Moja wana Biashara za ku compete, mfano ndugu familia moja wote wana Mabasi na yana compete, Wana maduka yana Compete, na kadhalika, hawa ukiwaambia waunganishe mitaji hawakuelewi kabisa.

Investors wengi wanao kuja Tanzania kama hawajakopa basi unakuta wamejichanga, hata Wazungu, unakuta wa mejichanga wanne au watatu na kufungua kampuni Tanzania.Hatutaweza kushindana na wawekezajinwa nje kama hii vita tutaipigana kila mtu kivyake. Niambie kuna Kampuni ipi ya ujenzi inaweza shindana na zile za Wachina au Wajapani? Ipo? Tuna utitiri wa kampuni za ujenzi ila kamwe hazifikirii kuungana na kuwa na kampuni moja strong ya kushindana.

Sisi unakuta kila mtu anataka afuge kuku angalau 500 wa nyama au mayai, Ila je tutaweza kusindana na wawekezaji wanao kuja Tanzania wanafungua Shamba la kuku na kwa siku wana chinja kuku 100, 000? Wanakusanya trei 5000 za mayai kwa siku? Tutawaweza?Kule Tanga naambiwa kuna mchina anafuga Broiler akupeleka sokoni ni kwanza mzigo wake uishe nyie wengine ndo muanze kuuza na unakuta hapo sisi mtu ana kuku 49 ndo anapeleka sokoni.

Sisi Gradute na pesa zetu za Boom tumejibana tutaweza toboa bi a kuungana?

Tunaweza fanya nini?

Nadhani ifike wakati tuache hizi sababu kwamba hatuaminiani, tutazungukana na kadhalila. Kama ndo hivyo basi tunaweza fanya haya;

- Kuweka mikataba yote kwenye maandishi, n kujenga kiwango cha juu kabisa cha uwazi, ni kweli tunapenda janja janja lakini, tunaweza fanya kitu, tunaweza weka misingi ya juu kabisa ya uwazi, shida pia ni uwazi, uwazi tunakuwa hatuna wa kutosha.

- Tuachane na Tamaaa, hizi ndo chanzo kikuu cha watu kusingizia uaminifu uaminifu kumbe ni tamaa tupu.

- Tuachane na kushindana kutaka kuwafurahisha ndugu, jamaa na marafiki, moja ya sababu ni kwamba kila mmoja anataka aonekane mbele ya jamii kwamba anamiliki biashara ya pekeee yake, ana basi lake, ana Daladala lake mwenyewe, ana duka lake mwenyewe, ana kampuni yake mwenyewe ya ujenzi.

- Tuajiri Managment, kama tunaona shida basi tunaunganusha mitaji na kuweka menejiment na sisi tunakaa pembeni kabisa Managemnet ndo inafanya kazi, hii ni nzuri sana ila ni ni kwa wenye mitaji mikubwa tu. Wenye mitaji wanaweza weka Management na ikawa inafanya kila kitu wao wakawa wanapelekewe report tu.

-Tukae tuwaze competition tunazo pata na pia zijazo, na tukisha ziwaza tuache kuwaza hasi, na tuunganishe mitaji.

Ndugu zangu ukweli ni kwamba hatutaweza compete na wageni kama kila mtu ataenda kivyake vitani, hatutaweza na hii vita hatutashindwa, tutashindwa hii vita, wanakuja Wawekezaji kama Wachina wana mitaji mikunwa sana na wameungana wanafungua Biashara na bidhaa zao na huduma ni cheap, sisi hatutaweza.Tusipo acha hii kasumba ya kwamba ohoo Watanzania hawaaminiani, mara wezi, mara sijui nini hatutaweza vita ya Biashara.

Lazima tuache neno hatuaminiani, inakuwaje ni sisi tu? Wakenya, Waganda, wote hao wanaamininiana isipo kuwa sisi? Whay?

"Nzi akiacha mambo ya ajabu anaweza tengeneza asali, na sisi siku tukiacha mambo ya ajabu ya visingizio tunaweza watoa jasho wachina"

Karibuni.
 
BLACK MOVEMENT ni idea nzuri sana ila sasa ni mpaka upate watu ambao kabla ya kuunganisha idea muwe pia mnashare interest na pia mna maono sawia .Nakupa mfano

Miaka ile nikiwa chuo tuliungana wale watu tuliokuwa tunapiga wote discussions alafu tukawa tunachanga elfu hamsini(50000/=) ili ikikua basi tuanze kukopesha wanafunzi wenzetu kipindi cha hali ngumi

Hiyo hela ilikuwa inachangwa soon baada y boom ila kwa wale ambao hatukuwa na boom basi tulikuwa tunatoa siku karibia na boom pia

Mwisho hela ilikuwa nzuri tukaanza kukopesha ila finally biashara ilikuja kubuma sababu ya kutokuwa na ushirikiano katika kudai na katika kuwa na real interest mwisho tukapigwa na wajanja wa chuo , hapo ndiyo mwanzo wa magomvi mengi kiasi cha kila mtu kumuona kila mtu ndiye chanzo.

Ndugu hayo yanawezekana ila ni process kuwapata watu wa hivyo sio kukurupuka utalia sana
 
Una mawazo mazuri sana,sasa kwa kumpata huyo wa kushare interest kibiashara ndio inshu,from no where huwezi kumfuata mtu nataka tuwe share kwenye biashara,kwa upande wangu natamani sana kumpata mtu wa kushare nae biashara
 
Tatizo limefahamika, na chanzo kimejulikana KUTOAMINIANA

Kimsingi inabidi tuwekeze kwenye mifumo imara, mfano tukiungana tukaandikishana mikataba ikitokea mtu kazingua tukifikishana kwenye vyombo vya usalama tuwe na uhakika wa kupata haki.

Hata hivyo nimkazi sana kuamini mfumo mzima ikiwa mtu mmojammoja tu hajiamini, haamini na haaminiki!!

Tungetumia hofu kujenga imani na nidhamu mfano, uchawi, waganga na mizimu na laana tatizo waganga wenyewe hawaaminiki!. Labda tustaarabike saana tutumie kuaminiana kwa upendo na dini ya kweli kutoka moyoni.

Anyway kuendelea kutowaamini wenzio ni matokeo ya ukoloni, na kuhusudu hiyo hali au kuishadadia ni kujipiga mapingu sisi wenyewe.
 
Tanzania Ni rahisi sana kutengeneza misukule na kuipiga kuliko kushirikiana kwa kukuza mitaji.
 
Yan mkuu kati ya kitu kinachotesa ni hiki an
Mwaka huu mwishon nitakuwa na 3M ila naona haitoshi kufanya chochote hivo najaribu kutafuta wa kuunga nae mtaji tupige kazi ila watu hawapatikan
Kila mmoja anataka chake tu an

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada umezungumza vizuri sana, kiukweli hakuna mahali tutafika kama kila mtu ataendelea kupigana kivyake, kuna wakati hua nafikiri wenzetu wa shule hebu watusaidie bas hata kuwafundisha watoto wetu nna ya kufanya kazi kwny timu I mean 'teamwork' sabab dunia ya Leo huwezi ku accomplish big things km kufanya kazi ndani ya timu kunakushinda tutake tusitake hili jambo lazima kuli develop..!
 
Una mawazo mazuri sana,sasa kwa kumpata huyo wa kushare interest kibiashara ndio inshu,from no where huwezi kumfuata mtu nataka tuwe share kwenye biashara,kwa upande wangu natamani sana kumpata mtu wa kushare nae biashara
Mkuu lete wazo lako tuone kama tunaweza kwenda pamoja,mimi siogopi kuthubutu,maadamu liwe jema.
 
Ubinafsi umechukua nafasi kubwa za watu.
Tukumbuke kuna wengi wenye mawazo mazuri lakini kumpa mwrnzake apige hatua inakuwa ngumu.
Na ndo maana kila mmoja analialia shida hakuna wa kumvusha mwenzake
 
Mbongo ukiwa nae share kwanza lazima kampuni itakufa au mtakuwa mnakopa ili kuongeza mtaji maana wote mnaiibia kampuni
Hakuna kuwaza ikue la bali kila mmoja anachukua chake mapema

Hata mkifanikiwa kwa mfano kununua assets mtaishia kuuza tu
 
Ni wazo zuri sana kuungana km wote mtakua na same interest , na pia muwe na attitude zinazofanana ..sio ile mmoja anataka kuwa juu ya mwenzake ...Tatizo kubwa kwa wabongo ni Selfishness, Lack of trust na EGO
 
Back
Top Bottom