Kwanini Slaa hashiriki katika vipindi mbalimbali vya TV?

Kwanini Slaa hashiriki katika vipindi mbalimbali vya TV?

Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali vya mijadala katika tv zetu, katika vipindi hivyo wamekuwa wakiwaalika watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, mfano Profesa Lipumba, Jamesi mbatia, juliuas mtatiro na hata Maalim seif, lakini ni ngumu sana kumuona dk Slaa au Mbowe wakialikwa kwenye vipindi hivyo je ni uoga wa vituo hivyo kuwaalika watu hawa? Mfano kuna kipindi cha dakika 45 cha itv pili je tutafika cha chanel teni, tatu malumbano ya hoja, nne tuongee asubuhi cha star tv, kipima joto nk.
Je kwa nini hawashiriki!

angalia na uzikilize nini hao unaowSema wanazungumza halafu linganisha na hawa akina Dr na mwenyekiti kwamba wanazungumzia nini na hat ivo kumbuka kuwa hata mafisadi wanazungumza sana kwenye vyombo vya habari
 
Mbona husemi Kikwete kutokea ktk vipindi mbalimbali? Kwann ufikirie Dr. Slaa & Mbowe? Wanakazi ya kukijenga chama, matawi mangapi yamefunguliwa, chaguzi mbalimbali kushiriki kikamilifu, kusimamisha madiwani nchi zima, s/mtaa na wabunge, mbona nchi inaongozwa na Cdm kwani huna habari? Kina mbatia, Lipumba hawana dira na mikakati ya kuingia Ikulu, watibuaji na matawi ya magamba, inamaana siasa za Tz huzijui.

Kamanda Mgelukila, umenena vyema mkuu. Mwanzoni maswali yalikuwa kwa nini hatuwaoni vijijini na mitaani...
 
Jaman kuweni wazi ni ukweli kwamba wakiitwa na kuhojiwa kuhusu jambo lolote wataanza kuongelea ufisad
 
Wengi hawana maswali sahihi, na mengi yake yanamfaa sana mtu kama JK , mengine wayawekayo Mnyika huwa anatosha sana.

Kumweka CDM na CCM bila control ya hali ya juu ni kuwadhalilisha CCM na kuwapaisha CDM. (magamba wataburuzwa sana hadi waanze ongelea general ili na conclude kuwa tunahitaji jenga nchi kwa pamoja)
 
Sasa hivi huyu jamaa was Dakika 45,alisoma wapi?,mwanzoni alia za vizuri,alisema atawaita mawaziri kuzungumzia mambo mbalimbali yahusuyo mustakabari wa nchi,baadaye akawavamia wastaafu sasa sijui walimnunua au ni vipi?,baadaye amegeuza kuwa kipindi cha kujibu hoja za wapinzani,sasa huyu bwana mdogo tumshauri tu ajitahidi kubalance,ili watanzania tuelewe majibu ya hoja pande mbili,alafu pia hasiruhusu mambo yasio na Tija kwa taifa kwenye kipindi choke.
 
Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali vya mijadala katika tv zetu, katika vipindi hivyo wamekuwa wakiwaalika watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, mfano Profesa Lipumba, Jamesi mbatia, juliuas mtatiro na hata Maalim seif, lakini ni ngumu sana kumuona dk Slaa au Mbowe wakialikwa kwenye vipindi hivyo je ni uoga wa vituo hivyo kuwaalika watu hawa? Mfano kuna kipindi cha dakika 45 cha itv pili je tutafika cha chanel teni, tatu malumbano ya hoja, nne tuongee asubuhi cha star tv, kipima joto nk.
Je kwa nini hawashiriki!
Jery Slaa na dakika 45 ?
Ushaona pakacha likibebewa maji?
 
Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali vya mijadala katika tv zetu, katika vipindi hivyo wamekuwa wakiwaalika watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, mfano Profesa Lipumba, Jamesi mbatia, juliuas mtatiro na hata Maalim seif, lakini ni ngumu sana kumuona dk Slaa au Mbowe wakialikwa kwenye vipindi hivyo je ni uoga wa vituo hivyo kuwaalika watu hawa? Mfano kuna kipindi cha dakika 45 cha itv pili je tutafika cha chanel teni, tatu malumbano ya hoja, nne tuongee asubuhi cha star tv, kipima joto nk.
Je kwa nini hawashiriki!
Labda ni kwa sababu sio waandishi wa habari wa vituo hivyo.
 
Kwanza kwa hali ilivyo TV za nchi hii ili kumpa airtime Slaa au Mbowe lazima hata Ikulu ihusishwe maana kitakacho tokea hapo wenyewe wanajua. Na kwa taarifa yako ukitangaza mapema kuwa wakati fulani kutakuwa na mahojiano na Dr Slaa nina hakika Tv zingine zote zitakosa watazamaji muda huo ila tumeshashuhudia mkulu anatoa hotuba ya mwezi na watu wanaangalia Tamthilia,hapo ndio ujue thamani yao ni ipi hao watu kwa nchi hii. Huo ndio ukweli.
 
uchambuz fresh sanaaaaaaa
 
Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali vya mijadala katika tv zetu, katika vipindi hivyo wamekuwa wakiwaalika watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, mfano Profesa Lipumba, Jamesi mbatia, juliuas mtatiro na hata Maalim seif, lakini ni ngumu sana kumuona dk Slaa au Mbowe wakialikwa kwenye vipindi hivyo je ni uoga wa vituo hivyo kuwaalika watu hawa? Mfano kuna kipindi cha dakika 45 cha itv pili je tutafika cha chanel teni, tatu malumbano ya hoja, nne tuongee asubuhi cha star tv, kipima joto nk.
Je kwa nini hawashiriki!

Wataongea nini zaidi ya majungu na ufataani.
 
Kwanza nikubaliane na mchangiaji mmoja kuwa ili hawa watu waalikwe ni lazima hata ikulu ya JK nayo iwe na taarifa kwa sababu always hawa ni watu wasio wanafiki kwani nyeusi wataiita nyeusi na nyeupe ni nyeupe tu!!.Hapa maana yake ni moja kuwa hawa ni watu wasioinea haya serikali kwani huikosoa moja kwa moja pasipo kulemba!!..Mfano,ukimwalika ktk kipindi cha Selemani Semunyu cha DKK 45 (ITV) na ukamuuliza swali mfano Dr Slaa la uchumi na umasikini wa nchi yetu, usitegemee akamung'unya maneno hapo kwa kutosema kuwa hii yote inatokana na sera mbovu za CCM na udhaifu wa serikali ya JK na JK mwenyewe.Na milele hatasita kutaja sera ya kulindana inayopelekea kushamiri kwa ufisadi/rushwa iliyozaa kashfa kama za EPA, Richmond,madawa ya kulevya nk na ktk hayo yote JK atachanwachanwa na milele hawezi kuchwa salama.Nani anataka kuona haya ktk serikali na CCM ambao ndo wanadhiti mfumo mzima wa habari?Kituo gani cha TV/Redio kitakuwa na ujasiri wa kumwalika mtu wa sampuli hii katika mfumo huu wa uendeshaji mambo yetu tulionao?

Hata hivyo kuna ya ziada hasa kwa huyu (Dr W. P. Slaa) kwa sababu huyu mzee binafsi nilibahatika kumwona kwa karibu na kusikiliza hoja zake ktk moja ya hotuba yake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 na mara moja baada ya uchaguzi huo ktk kipindi fulani ktk TV (sikumkuki ni kipindi gani), nilijifunza haya yafutayo toka kwake;
  1. Ni kiongozi asiyependa mizaha ktk mambo ya msingi ya kitaifa hata ukitazama macho yake,sura yake utasoma mpaka kilicho ndani ya moyo wake kwani (ukichemka atakupasha hapohapo hata kama wewe ni mtangazaji wa redio au Tv hiyo unamuhoji.Nadhani udaktari wake ni wa philosophy/psychology
  2. Ni mzee mmoja mwenye ufahamu na uelewa wa hali ya juu sana wa mambo. Na hii maana yake ni kuwa anasoma na kujifunza kila kuchao bila kuchoka kama alivyokuwa tu baba wa taifa Julius K. Nyerere kitu ambacho ni tofauti sana kwa viongozi wetu wengi wa sasa wazee wa dizaini ya JK au Ndugai au Anna Makinda na wengine wengi tulionao.Na hii ni kwa sababu moja au mbili tu UVIVU na KULEWA MADARAKA na kutotambua kuwa cheo ni dhamana na ni utumishi kwa umma.Ni watangazaji majasiri pekee wa dizaini ya Jenerali Ulimwengu ((Channel Ten Tv) au Rainfred Masako (ITV) wanaoweza kukabiliana na mtu wa namna hii.....Na si watu kama Ivona Kamuntu wa STARTV au Semunyu wa kile cha DKK 45 cha ITV!!

Mwisho kabisa ni mfumo wa habari ktk nchi yetu kwani kwa sehemu kubwa uko controlled na serikali yenyewe iliyo chini ya CCM kwa sasa ambao kwa sasa adui yao mkuu ni Dr Slaa/Mbowe na CDM (huu ni mtazamo wao na wanaamini hivyo). Chunguza vipindi vingi vya Tv (TBC,STARTV,CHANNEL 10,ITV nk) na Redio mbalimbali vinavyojadili mambo mbalimbali ya kitaifa....Vingi ya vipindi hivi pamoja na watangazaji wake vipo/wapo kimkakati zaidi in favour of the government in power under CCM, yaani vingi havipo fair na DR SLAA au MBOWE na yeyote asiyependa masihara na ujinga hawezi kukubaliana na vipindi hivi ambavyo ni ONE SIDED!!...Angalia mfano kipindi cha DKK 45 anakuja Steven Wassira ataponda Chadema weee...... au Dr Slaa mpaka baasiii!!!....,Na kusifia serikali yake na CCM balaa mpaka mtazamaji/msikilizaji unakosa radha ya kipindi!!!..Na hata siku moja huyo aliyesemwa hapati nafasi ya kujibu hoja!..Sasa ktk hali kama hii tusitegemee kuwaona watu wa mrengo wa Dr Slaa kuitwa ktk forum kama hii na ikitokea tu na TV au Redio hiyo ikatangaza kuwa siku fulani watakuwa na mahojiano na DR SLAA kuna mchangiaji mmoja kasema kuwa kila mtu siku hiyo ataangalia kipindi hicho na kusahau kipindi vingine vyoooote.....na hakika ndivyo ilivyo!!
 
Dr.Slaa si muuza sura kama walivyo viongozi wengi wa CCM alias Bi kizee cha Lumumba.Labda sana sana atafanya mahojiano na jamaa wa BBC kwenye kipindi cha 'Hard Talk' huko ndo kunaibuliwa hoja zenye mashiko.
 
Kwanza kwa hali ilivyo TV za nchi hii ili kumpa airtime Slaa au Mbowe lazima hata Ikulu ihusishwe maana kitakacho tokea hapo wenyewe wanajua. Na kwa taarifa yako ukitangaza mapema kuwa wakati fulani kutakuwa na mahojiano na Dr Slaa nina hakika Tv zingine zote zitakosa watazamaji muda huo ila tumeshashuhudia mkulu anatoa hotuba ya mwezi na watu wanaangalia Tamthilia,hapo ndio ujue thamani yao ni ipi hao watu kwa nchi hii. Huo ndio ukweli.
Wengine tunakuwa hatujui kabisa kama kuna hotuba ya rais inatolewa muda fulan. Na hiyo ni kutokana na kukosa mvuto kwa wananchi. Mikutano ya CDM huwa matangazo yanakuwa kidogo au muda mfupi lakini wanjaza nyomi.
 
Back
Top Bottom