Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 30,715
- 39,796
Inashangaza unajisifia Internet wkt nusu nzima ya watu wetu hawana chakula, Elimu, Maji safi ya kunywa, afya, I mean naweza kujuza kurasa hapa kuorodhesha matatizo ambayo yalipaswa yawe yamekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa kama tungewekeza muda wetu kufanya yale muhimu na yaliyo ndani ya uwezo wetu!
angalia sasa internet ilivyokua nuksi,
Elimu- kupitia internet unajifunza kwa walimu best, haijalishi unasoma shule ya kata au umesoma feza, kupitia internet unaweza ukajifunza kwa mwalimu best na ukawa na elimu bora kushinda mtu aliesoma shule ya mamilioni.
Afya- Hospitali nzuri kumuona tu daktari na kupewa ushauri unaweza ukaambiwa gharama zake ni mshahara wa mwalimu. ila kupitia internet napata ushauri wa ki Afya toka kwa madaktari nguli duniani, nchi zote kubwa marekani, uingereza, australia wana website za Taifa za afya ambazo zinaelekeza kutibu magonjwa mbali mbali na kutoa ushauri wa ki Afya kwa wananchi wao. Huduma anayopata mmarekani anapata mtanzania hiyo hiyo asante iende kwa internet.
chakula na maji - kupitia hio hio internet unajifunza mbegu bora za kulimia, watu wanaagiza mbegu na vifaa online na kulima kisasa kwa maelekezo ya online hii inasaidia kuongeza productivity na kusaidia kupunguza hio njaa, ukiwa serious unaweza ukalima sawa na mkulima wa marekani. same kwenye maji, kuna tips kibao online za kuyasafisha, jinsi ya kuyachimba kiurahisi etc
nenda mbele rudi nyuma internet itabakoa kuwa muhimu kwenye maendeleo.