Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
- Thread starter
- #141
Ni upuuzi mtakatifu kusema ili tuendelee inatubidi kupitia hatua walizopita walioendelea.
Hii hatua tunayopitia sasa wenzetu hawakuipitia. Wamarekani na waingereza walitegemea misaada ya nje kwenye bajeti zao?
Kwa kila shilingi moja ya msaada na mkopo tunayochukua tunalipa shilingi 2 kwenye riba, fedha chafu (money laundering) na ukwepaji kodi wa makampuni ya nje. Chukulia tu kodi wanayodaiwa Acacia kwa miaka 10, je haizidi misaada ya nchi tuliyopokea kwa miaka kumi?
Ndio maana namkubali sana Magufuli!
Hakuna mahali niliposema kwamba tunahitaji msaada ili tuendelee, na kwanza hiyo misaada iko kwa ajili hiyo kutupumbaza ili tuendelee kuamini hatuwezi kujisimamia bila ya Muzungu, bali nimesema kuna hatua ni lazima tuzipitie kama jamii bila ya hivyo hakuna mahli tutaenda, na kuna kila ushahidi wa hilo unaonekana kila mahali!