Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,053
Reaction score
15,515
Wakuu habarini.
Naomba kujua kwanini iPhones zina specifications ndogo ukilinganisha na simu nyingine zote hata ambazo zinachipukia.

Sijaona iPhone inayozidi hivi vigezo:
- Maximum RAM 3gb
- Maximum Camera 12 Mega Pixels
- Maximum Battery size </ = 3000 mAh

Hawa jamaa innovation yao ipo katika mlengo upi?.

Hizi simu sijawahi kuzitumia na nahisi sizipendi japo nina pesa ya kununua iPhone niitakayo. Lakini naona simu kama ya waganga wa kienyeji. Maana masharti ni mengi kuliko enjoyments.

Yaani kumiliki hizi simu ni kama Mkinga mfanya biashara anayelala chooni ilihali ana majumba ya kifahari

1. No interaction with PC without Itunes
2. No Bluetooth compatibility with other devices except its generic siblings
3. Kupata apps za local developers ni msala
4. No downloading on websites and blogs
5. Poor documents perusing and management
6. No memory extension.
7. Finger print zinakufa hovyo kuliko simu zozote
8. Poorness of IOS Ecosystem
9. No access of payable services in some many regions (Especially Africa)
10. Poor navigation of (Back) Button. Sijui watu wenye iPhone huwa mnaenjoy nini kwenye simu zenu.
11. No dual SIM
12. No File Management App
13. Safari as a default Browser no way ndugu yangu

Naomba ushirikiano
 
Hazchem plate,

Nimewahi Tumia Samsung S3, then note 4. Baadae Nikatest Huawei na Tecno. Lengo lilikuwa kujua hasa ladha na uzuri hususani baada ya kuona watu wanaongea ongea sana. Kila simu hapo juu, niliitumia kwa kipindi kirefu cha kuweza kujua uzuri na ubaya wa kila moja.

Baada ya kupita kote huko, nikajilipua nikanunua iPhone 8 Plus. Ukweli ni kwamba, sijajutia hela yangu maana simu ina ladha asikwambie mtu.

As well kuna vionjo fulani hivi ambavyo simu zangu zote za nyuma hazijuwa na huo uwezo. Apple Devices for sure are in another level. Comment yangu hii imebase from practical experience. Sina utaalamu sana wa kuchambua jinsi iPhone hii ilivyo but kuna tofauti kubwa sana na hizo Samsung, Huawei na Tecno ambazo nilishawahi kutumia.
 
Simu za Android zina garbage nyingi hivyo huitaj specification kubwa Iphone hazina garbage haziitaji specification kubwa ukitaka kuhakikisha chukua Android yenye RAM na processor kubwa na iPhone yenye spefication ya chini kidogo jaribu kucheza game utaona zinaenda sawa. Au jaribu kuwasha na kuzima.
 
Nimewahi Tumia Samsung S3, then note 4. Baadae Nikatest Huawei na Tecno. Lengo lilikuwa kujua hasa ladha na uzuri hususani baada ya kuona watu wanaongea ongea sana. Kila simu hapo juu, niliitumia kwa kipindi kirefu cha kuweza kujua uzuri na ubaya wa kila moja.

Baada ya kupita kote huko, nikajilipua nikanunua iPhone 8 Plus. Ukweli ni kwamba, sijajutia hela yangu maana simu ina ladha asikwambie mtu.

As well kuna vionjo fulani hivi ambavyo simu zangu zote za nyuma hazijuwa na huo uwezo. Apple Devices for sure are in another level. Comment yangu hii imebase from practical experience. Sina utaalamu sana wa kuchambua jinsi iPhone hii ilivyo but kuna tofauti kubwa sana na hizo Samsung, Huawei na Tecno ambazo nilishawahi kutumia.
So umekubali aliyoyaandika mtoa mada ni ya kweli?
 
iPhones RAM ndogo ila processing speed ni kubwa kuzidi simu za Android zenye RAM kubwa zaidi.iPhones kama ilivyo kwa brand nyingine naye ananunua camera toka kwa Sony, cha kushangaza picha zake zinatoka clear zaidi hata ya Sony wenyewe.

Kifupi hadi leo iPhones haziapata mbadala kwenye high end phones.
 
Mtoa maada umechambua vyema Sana upo sahihi.ila Mimi simu ya ndoto zangu SI Ni iphone kwa kweli yaani nikipata tu hela lazima ninunue iPhone nijionee mwenyewe.sijawahi hata kushika iPhone wenye nazo wachoyo kweli
Haahaa mkuu wanakunyima Hata kushika,pole sana
 
Nimewahi Tumia Samsung S3, then note 4. Baadae Nikatest Huawei na Tecno. Lengo lilikuwa kujua hasa ladha na uzuri hususani baada ya kuona watu wanaongea ongea sana. Kila simu hapo juu, niliitumia kwa kipindi kirefu cha kuweza kujua uzuri na ubaya wa kila moja.

Baada ya kupita kote huko, nikajilipua nikanunua iPhone 8 Plus. Ukweli ni kwamba, sijajutia hela yangu maana simu ina ladha asikwambie mtu.

As well kuna vionjo fulani hivi ambavyo simu zangu zote za nyuma hazijuwa na huo uwezo. Apple Devices for sure are in another level. Comment yangu hii imebase from practical experience. Sina utaalamu sana wa kuchambua jinsi iPhone hii ilivyo but kuna tofauti kubwa sana na hizo Samsung, Huawei na Tecno ambazo nilishawahi kutumia.

Nina rafiki yangu alikua anapenda sana Tecno na Samsung. Jamaa ni conservative fulani hivi yaani akiwa na msimamo wake ndio huo huo. Ikafka time Tecno yake iliharibika nikamshauri anunue iPhone kwa sababu kwamba znadumu maana mimi nlikua natumia iPhone 6 kipindi hcho yeye alinunua tecno ikaja kuharbika mimi bado iPhone ipo.

Akajaribu akaagiza iPhone 6 Plus ambayo alikaa nayo almost miezi 4 akaibiwa.

Baada ya hapo amekuwa Apple addict maana akaja akanunua 7 Plus akakaa nayo akaiuza now anatumia iPhone X na amenunua Apple Macbook Pro version ya 2017 kabisa yaani ashatekwa na ukimuuliza vipi kuhusu Tecno anakuambia labda siku nifilisike nitarudi kwenye hizo brand zingne yaani ni uozo tu.
 
Watu wengi hawafahamu kuwa apple ni kampuni yenye nguvu sana kwenye soko lakin haimaanishi ndio simu bora kuliko zote zipo simu hata kwenye soko la kwetu huku hazijafika sababu kwanza zina bei na bora zaid ya Iphone ila wana nguvu ya soko ingia mtandaoni utafute simu zenye ubora na bei kibwa kuliko iphone utaikuta imetupwa mbali tu nyingi zinaishia America na Ulaya
 
Hapo kwenye megapixels, mimi sio mtaalamu sana wa camera lakini katika simu usiangalie megapixels peke yake, angalia kitu kinaitwa aperture.

Mfano sasa hivi simu nyingi zina 12mp lakini tofauti inakuja kwenye aperture. Ukitaka kuijua aperture, kwenye sites mbalimbali zinazoweka specifications za simu utaona kwenye camera wanaandika 13mp, f/1.8 sasa hiyo f/1.8 ndo kitu cha kuangalia zaidi.

The less it is in figures, the higher the quality of the pic.

Hivyo hata kwenye iPhones ni kweli hawana zile mbwembwe za 16mp, ila aperture is what matters.
 
Utupe maelezo sasa,hiyo apecha pecha lololo,ipi kubwa na ipi ndogo,
 
Hazchem plate, Nilikuwa nawatamani wanaotumia iPhone kiasi kwamba niliamua kuchukua i6+. Hakika sikumaliza nayo wiki. Inaboa sana.

Nimerudi Samsung kwakweli.

Kimtazamo huku kwetu ni kwamba mtu anayetumia iPhone, anaonekana ni mwenye hadhi. Nimesema kimtazamo tena kwa watu tuliokosa elimu na kukaa na watu wengi tukajua dunia ilivyo.

Kwa upande wangu, iPhone haina lolote kwakweli kumzidi Samsung
 
Back
Top Bottom