Kwanini simba mfalme wa nyika hawezi kumdhuru fisi?

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Wengi tunafahamu simba ni mfalme wa nyika na anapo unguruma wanyama wengi hukimbia mbali nae.

Kwanini simba huyu mwenye nguvu na spidi hawezi kufua dafu kwa fisi mnyama mdogo kiumbo?

Wataalamu Embu mtupe elimu kama ni kisayansi au kwa namna yoyote tujifunze.
 
Mtoa hoja umeongea kwa codes nini?,kama sio hoja yako ni ya uongo mkubwa,simba na Fisi wote ni predators, kwa hiyo ni maadui na elewa simba/Fisi ni wanyama wenye vipande vyao vya kuishi, vita yao ni nani mwenye numbers kubwa, fisi wakiwa wengi wana uwezo wa kuchukua chakula kutoka kwa simba, hivyo hivyo kwa simba,ILA male lion 🦁 ndio kings, hata fisi wanamkimbia hata wakiwa 10
 
Nimeuliza kujua💁🏻‍♂️
Mkuu hiyo midoli una mtoto wakike nini?🤣
Fisi ana sauti kali na fisi anaweza kusogea karibu kabisa na simba anapokula tofauti na wanyama wengine. Simba dume akija wanasogea mbali au kuondoka fisi ni mchawi ujue tu
 
Na mimi nilidhani hivyo kuwa ni codes 😄 🤣
 
Mkuu hiyo midoli una mtoto wakike nini?🤣
Fisi ana sauti kali na fisi anaweza kusogea karibu kabisa na simba anapokula tofauti na wanyama wengine. Simba dume akija wanasogea mbali au kuondoka fisi ni mchawi ujue tu
Wala si wakike mkuu.

Kipindi Mke wangu ana mimba nilikuwa nikimwambia huyu anayekuja ni mwanamke mwenzako, yeye akasema huyu Nina Hakika dume.

Nilikuwa nanunua magari na midoli incase ikitokea popote.
 
Wakuu habari za uzima?

Wengi tunafahamu simba ni mfalme wa nyika na anapo unguruma wanyama wengi hukimbia mbali nae.

Kwanini simba huyu mwenye nguvu na spidi hawezi kufua dafu kwa fisi mnyama mdogo kiumbo?

Wataalamu Embu mtupe elimu kama ni kisayansi au kwa namna yoyote tujifunze.
Wewe humjui simba. mara nyingi ukiona simba katimka mbio, jua pale kuna fisi sio chini ya 10, ila ukiona wawili watatu wanne, simba huwa anahakikisha kaua sio chini ya mmoja. simba akiua mnyama, fisi akitokea huwa anaacha hadi msosi anamfukuza fisi hadi amuue ndio arudi kula. mnyama pekee mwenye uwezo wa kumshinda simba, wa kwanza ni binadamu, na wa pili ni Tiger. na tiger ni kwasababu umbile lake ni kubwa kuliko simba na anajua sana kupigana kuliko hata simba. wengine woote hata tembo, simba huwa analala usingizi mzito anajua hakuna mjinga yeyote atamsogelea. pia, msikie simba kwenye tv tu, ukiwa karibu naye, anatisha kuliko unavyoweza kuongea. ni hatari hasa umkute yule umri mkubwa ni hatari hadi hali ya hewa inabadilika.
 
Mtoa hoja umeongea kwa codes nini?,kama sio hoja yako ni ya uongo mkubwa,simba na Fisi wote ni predators, kwa hiyo ni maadui na elewa simba/Fisi ni wanyama wenye vipande vyao vya kuishi, vita yao ni nani mwenye numbers kubwa, fisi wakiwa wengi wana uwezo wa kuchukua chakula kutoka kwa simba, hivyo hivyo kwa simba,ILA male lion 🦁 ndio kings, hata fisi wanamkimbia hata wakiwa 10
Hakika mekuelewa mkuu.
 
Simba (Panthera leo) anamuua vizuri Fisi (Crocuta crocuta) akiingia kwenye kumi na nane zake, japo akimuua hawezi kula nyama yake maana ina harufu fulani ambayo inamkereta Simba...

Hivyo, akishamuua fisi atamuacha na scavengers wengine watamula bila kumuonea huruma...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom