Kama Simba mfalme wa mwitu

Musa Meizon

Member
Aug 3, 2021
13
53
Habari yako ndugu msomaji, kwa Mara nyingine tena nawasilisha kwako mada niliyo iandaa ili kukufanya uwe bora zaidi. Ni imani yangu umejipanga kuboresha maisha yako huku Mungu akiwa tegemeo lako.

Katika pita pita zangu nilikutana na kipindi kwenye runinga juu ya mfalme wa mwitu, yaani SIMBA! Nilijifunza mengi kumuhusu mnyama huyu na wengine pia lakini kama muandishi ilinibidi kujaribu kugeuza kile nilicho jifunza na kukiweka katika mtazamo wa kibinadamu zaidi.

Katika sifa nzuri nyingi nilizo ziona, zifuatazo ni sifa mbili za simba ambazo ukizijua unaweza jifunza mambo mengi makubwa;

1. SIMBA ANAJITAMBUA KUWA NI MFALME: Hakika nimeliona hili na nikastaajabu mno! Ni pale nilipomuona simba dume akienda kunywa maji mtoni ghafla mamba akajaribu kumuwinda kama vile anavyowawinda nyumbu wakinywa maji. Ni wazi kwamba mamba anauwezo mkubwa wa kumuua simba endapo angefanikiwa kumvuta Nani ya maji lakini simba huyu hakukimbia pale mamba alipo panua mdomo wake kujaribu kumdaka baadala yake alikwepa kisha akaanza kuunguruma, haikuchukuwa muda mamba akajirudisha kwenye maji taratiibu na kumuacha simba Yule akinywa maji kwa raha zake. Naamini mamba aligundua simba na nyumbu ni tofauti pale pale.

Rafiki; kujitambua ni nguzo ya ubora wako, kuna mambo huwa yanaonekana magumu kwetu kwasababu hatujajitambua sisi ni kina nani.

2. SIMBA JIKE HUMPIMA DUME KABLA HAJAKUBALI AMPANDIE: Hili litawalenga wanawake hasa japo hata mwanaume unaweza jifunza. Ili simba jike akubali kupandwa na dume basi hupitisha takribani wiki 2 akilichunguza dume hili kama je, lina nguvu? linajua kujilinda? na linaweza kumlinda? Sababu ni kwamba dume mmoja hutawala eneo kubwa la pori pamoja na majike hadi zaidi ya sita. Simba dume huweka alama kuzunguka imaya yake kwa kutumia mikojo, dume mwingine haruhusiwi kuingia katika eneo hilo alilowekea alama na akiingia maana yake anataka kupindua ufalme wake kwa kupigana na kumuua au kumfukuza.

Endapo dume mwenye imaya atapigwa na kunusurika kuuawa basi hukimbia na kwenda kutafuta falme nyingine na dume jipya huakikisha limefuta uzao wa dume lililo nyang'anywa falme kwa kuua vitoto vyote vitakavyo kuwepo hapo. Hii ndiyo sababu majike huwa makini kuchagua dume la kuwapanda kwani huumizwa sana pale vitoto vyao vinapo uawa na dume geni.

Rafiki; kila uamuzi unaouchukuwa Leo unaathari kubwa baadaye, hivyo ni muhimu kuwamakini.

Usifanye jambo kwa sababu tu unauwezo Bali lifanye kwa sababu unataka kulifanya!.

Do not do it just because you can, but do it because you want to!

Vijana wengi Leo hii tunaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwasababu tu tunaweza kufanya hivyo lakini sio kwasababu tunataka. Na huwezi kukitaka kitu ambacho hujakijua wala kukichunguza kama kinamchango hasi au chanya kwako vinginevyo uwe mpuuzi!

Leo nitakomea hapo na muda mwingine nitakuja na sifa nyingine za simba ambazo zinamafunzo kwetu japo ni binadamu sio wanyama. Ahsante!


IMG_20210804_195756_004.JPG
 
Duh aisee sikubali unifananishe na mnyama Simba bila wengine Bora unipe na sifa za eagle dume Kisha nichague na za nyangumi dume
 
Pamoja na yote lakini kiboko ya simba ni Nyani hasa wakiwa wengi akikuona binadamu anakukimbilia hakufanyi kitu umuokoe maana anajua Nyani wanamwogopa binadamu
 
Simba mchumba tu mbele ya Tiger kuanzia kwa akili za uwindaji na upambanaji, ukubwa, ukatili na uzito. Yani ni bora ukutane na Simba watano unaweza kunusurika kulikoni kukutana na Tiger mmoja ujue uhai wako umekwisha.
 
Ungeniambia kwanza sifa za Tiger (Chui mwenye milia), Leopard (Chui), Cheetah (Duma), Eagle, Rhino, Buffalo, Elephant (Tembo) halafu nilinganishe na Simba tujue yupi ni mfalme halisi.
 
Nataka kujua hz jamii,Simba ni jamii ya Paka na ndio paka mkubwa na yule Dubu( Bear) mwenye sura km ya Mbwa je huyu ni jamii ya Mbwa yani ndio Mbwa mkubwa??
 
Back
Top Bottom