Kwanini Serukamba hakutolewa bungeni?!

Kwanini Serukamba hakutolewa bungeni?!

Kaka ungesoma bandiko la makaripio makali ya M.M kwa CDM, na majibu ya DR. Slaa basi ungepata majawabu tosha - kwa kifupi ni kwamba CCM tayari ime-PANIC.
 
mie nilishasema kuwa,watu makini hawawezi kutumia muda wa bunge kutukana ,watatamani hata wapewe masaa 3 ili waseme kwa kina matatizo ya wapiga kura wao.

Nadhani uongozi wa bunge nao kingereza tatizo,kwani matusi wanayoyaelewa wao ni yale ya kiswahili tu.PILI,serukamba naye naona naye ni kihiyo,nguvu aliyotumia kumshambulia mbunge mwenzie ni kubwa unadhani alishambuliwa au bunge ni mali yake binafsi.Nguvu ile ingetumika kutaka mikataba mibovu na mafisadi wachukuliwe hatua ingekuwa dili
 
kp19042013.jpg
-PAXP-deijE.gif
-PAXP-deijE.gif
 
Walishazoea kutukanana .............matusi ni sehemu ya maisha jadi yao. Huoni kwenye kampeni zao za ndani? Kama walifikia kulishana sumu ndo wataona matusi ni kitu? Wakiwafukuza watafukuza wangapi? Wanafikiri Tanzania ya leo ni Tanzania ya NDIO MZEE!
wanafikiri kutukana kwa kimombo ndo Wananchi hawataelewa? Ndo maana wanahakikisha watoto wa walalahoi wanamaliza form IV "with empty minds". Filamu za kinigeria zimewafunza wengi kimombo walahu cha kusikia tusi kama alilotoa Serukamba.
 
...Huwezi Jua...Labda Mheshimiwa Naibu haelewi maana ya 'F**k You', maana lilipotolewa hakuonekana hata kushituka angalau kwa kumuangalia tu Mropokaji!

Huyu nae mbona aliharibu lakini hakutolewa nje?
WASSIRA.jpg
 
PIMA UZITO WA MAMBO HAYA

1.KUTUKANA NDANI YA BUNGE
2.KUSEMA MAMBO BINAFSI YA WATU KM VILE MTOTO ANA WIKI 2,MIMBA
3. KUSINZIA BUNGENI
4.UTORO ULIOKITHIRI BUNGENI NA kuomba mwongozo mara nyingi nani mkosefu na alitakiwa kutolewa nje hapa?
 
Nyerere: "waswahili wana mambo ya ajabu. mambo ya kijinga jinga yakisemwa kwa kiingereza, wanashangilia kana kwamba ni mambo mema"

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema baba wa taifa Mwl Julius K. Nyerere katika moja ya hotuba zake.
Tusi alilolitoa Serukamba ndio tusi kubwa kuliko yote yaliyowahi kutolewa bungeni mpaka sasa. Tofauti na mengine yeye lake amelitoa kwa kiingereza kiasi kwamba naibu spika ameliona ni jema hivyo kutomchukulia hatua yoyote.

Hata majadiliano yanayoendelea sasa miongoni mwa wananchi na viongozi ni kuhusu "utovu wa nidhamu" wa Tundu Lissu wa kuomba miongozo na taarifa kila mara hivyo kutimuliwa bungeni na wenzake waliokuwa wakipinga kitendo cha naibu spika kumtoa nje. Hili la Serukamba halizungumzwi kama ni tusi kuu bungeni.

Tatizo ni kama alivyosema Nyerere, katukana kwa kiingereza hivyo spika na naibu wake hawaoni kuwa ni tusi. Waziri mkuu haoni kuwa ni tusi. Aibu!

Huyu peter serukamba ni mtu mdogo sana . Hafai kujadiliwa hapa. Elimu yenyewe ya ku-unga unga. Amemaliza MBA hapo ESAMI!!! Amekimbia kusoma MBA mlimani au Mzumbe.
 
Watanzania ni wapole sana.ndio maana hawana reaction yoyote kwa upuuzi unaotokea bungeni!ngoja na mimi niwatukane tu humu,....nyie ni ......kabisa!yaangalie sura zao yanavyochungulia humu jf!Serukamba endelea kuporomosha baba!wenyewe hawana noma bhana!
 
Mheshimiwa J.ndugai aliona kama LISSU ni mkosaji kwa kuomba miongozo mara nyingi na kuamua kumtimua bungeni.
SWALI:
1.kama wabunge wa ccm ndiyo wanaoongoza kisinzia bungeni,miongozo hiyo wangeomba saa ngapi wakati wanasinzia?
2.kama wabunge wa ccm ndiyo wanaongoza kwa utoro bungeni,muda wakuomba miongozo wataupata wapi?
3.kama wabunge wa ccm walichojaliwa ni matusi,je watakumbuka miongozo ya bunge?
4.kama wabunge wa ccm wanaongoza kwa kukaa nje ya majimbo yao,isipokuwa Pr.Majimarefu,wataomba miongozo kwa hoja gani wakati hoja walizo kwenda nazo bungeni hazikutokana na wapigakura wao?
5.kama wabunge wa ccm wanaongoza kwa rushwa km vile kina badwell,wataomba miongozo wamhhoji nani na nini?
6.kama wabunge wa ccm ni vinara kwa kututumia muda wa bunge kupongezana na kwasifia wake zao hadi wajukuu wao,watapata wapi muda wakutafakari ya kuombea miongozo?
7.kama wabunge wa ccm ndiyo wanaongoza kwa kusifia kila hoja ,wataomba miongozo ya nini?
8.kama wabunge wa ccm wanaona kwamba kila mbunge wao kama vile Deo filikunjombe anaikosoa serikali anaambiwa huyu atakuwa ni wa chadema,wataomba miongozo ili wakosoe nini?
9.kama wabunge wa ccm wanaona kazi yao pale ni kujipendekeza kwa rais hata kama maswala hayo yanataka kuboresha maslahi ya taifa,miongozo itatoka wapi?
10.kama spika na naibu spika wa ccm hayajui matusi yatolewayo kwa kiingereza na kuona hatua haitakiwi kuchukuliwa kwa mbunge aliyetukana kwa kiingereza,miongozo itaombwa kwa kazi gani?
11.kama wabunge wa ccm wanaona kazi iliyowapeleka bungeni ni kuwadhiti chadema tu ,wataomba miongozo ya nini?
 
Ukosefu wa busara wa hali ya juu kabisa,watu wazima wenye heshima zao maneno ya hovyo hovyo tu yanawatoka pasipo ata na staha.

Nashauri vipindi vya bunge vinavyorushwa kwenye tv viwe rated "R" ili watoto wasiangalie
 
Jamani mimi kidogo kiingereza kinanipiga chenga, sasa naomba mnisaidie tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma

1. FAKI YU
2. IMPOTENTI

Nawasilisha
Ukitoa tu tafsiri ya hayo maneno mawili, hasa hasa hilo la kwanza, ni kama vile utakuwa unawaomba kwa hiari yako mwenyewe, mods wakuitie polisi, ili wakutoe kwenye ukumbi huu wa JF na kukufungia siyo siku 5 kama kule mjengoni, ww waweza pata ban ya 5 years!!
 
Impotent government (WENJE) vs (SERUKAMBA)f**k you
 
Tusi 'original' katika historia ya bunge ndio hilo la serukamba. Lakini kwa vile katukana kizungu na tena yeye ni mccm hata kukemewa bado wakati wacdm wanafukuzwa kwa kudai mwongozo
 
Nilichojadili sio sifa ya kuwa Mbunge. Mjadala ni busara ya mtu. Kama Naibu Spika busara yake ilimtuma kutokereka na neno F*#@ YOU lililo nje ya kanuni ambalo alilisikia vizuri tu wala asishituke, badala yake akakereka dhidi ya mtu anayeomba mwongozo kwa mujibu wa kanuni, nadhani busara yake inaweza kuonekana kirahisi.
Halafu unayemsema aliomba radhi kwa kusema F*#@ YOU, alifanya hivyo lini?
By the way, Ukiomba radhi ndio unakuwa hukusema F*#@ YOU?
Kikao cha jioni saa 11 mara tu kilipoanza Serukamba alipewa dakika za kuongea na akaomba radhi kuwa kipindi cha asubuhi kuna neno lilimfyatuka ambalo sio zuri masikioni hivyo anaomba radhi na Bunge likamkubalia lakini aliyefuata aliomba Muongozo wa Neno hilohilo (Tusi la F*#@ YOU) akajibiwa kuwa limeshaombewa
Ndugai alisema kupitia Star TV kuwa Bungeni kuna matusi mengi ambayo hayasikiki wanayoyatamka Wabunge. Hivi unekuwa wewe (badili ya Serukamba) unatoa Hoja zako akatokea mwingine kukubeza au kukutukania wakati hana Mic na hasikkii lazima ungemjibu kutokana na Neno lake
 
Kama Ccm ndo serayao matusi atafukuzwaje Ccm hoyeeeee
 
Back
Top Bottom