Kwanini Serikali ya Tanzania inamuogopa sana kijana mdogo Twaha Mwaipaya?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,664
218,152
Wakuu natanguliza salamu, baada ya salamu hizi naingia moja kwa moja kwenye mada.

Tulishasema humu mara kadhaa na labda turudie tena kwa wale ambao hawakuelewa , CCM BILA POLISI NI WEPESI KULIKO PAMBA, na hili sasa limedhihirika kwa awamu zote za serikali ya chama hicho.

Twaha Mwaipaya ni kiongozi wa Bavicha anayepitia misukosuko mingi mno , huyu kijana alishakamatwa mara kadhaa na kurundikwa kwenye selo mbalimbali , mara zote Polisi wameshindwa kuthibitisha makosa yake , huwa anaachiwa tu katika mazingira tata, mara ya mwisho alitolewa gerezani usiku na mwenzake Nusrat Hanje , ambaye baadaye alipewa Ubunge na Job Ndugai.

Bado haijafahamika sababu hasa ya Serikali zote za CCM kumuogopa kijana huyu, kiasi cha kuwatumia Polisi kumkamata kila uchao.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kuwakanya wanaccm wenzake kuhusu madhara ya kuitegemea Polisi .

FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Polisi siku zote wanafanya kazi kwa maslahi ya CCM, hapo sioni la kushangaza.

Mimi nashangaa kwanini licha ya mazungumzo ya maridhiano yanayoendelea kwa zaidi ya mwezi sasa, lakini bado matukio kama haya yanatokea?

Hata kama Twaha amekosea, kwanini hafikishwi mahakamani siku zote hizo? Mbowe anasemaje kwenye hili? Lissu where are you? Lema...Sugu...
 
Kuna taarifa kwamba kipo kikundi ambacho hakitaki mazungumzo ya mwafaka
 
Mimi nashangaa kwanini licha ya mazungumzo ya maridhiano yanayoendelea kwa zaidi ya mwezi sasa, lakini bado matukio kama haya yanatokea?
Mazungumzo feki haya. CCM wanataka kuyatumia kuwapumbaza chadema.

Time will tell the truth
 
Wakuu natanguliza salamu, baada ya salamu hizi naingia moja kwa moja kwenye mada.

Tulishasema humu mara kadhaa na labda turudie tena kwa wale ambao hawakuelewa , CCM BILA POLISI NI WEPESI KULIKO PAMBA, na hili sasa limedhihirika kwa awamu zote za serikali ya chama hicho.

Twaha Mwaipaya ni kiongozi wa Bavicha anayepitia misukosuko mingi mno , huyu kijana alishakamatwa mara kadhaa na kurundikwa kwenye selo mbalimbali , mara zote Polisi wameshindwa kuthibitisha makosa yake , huwa anaachiwa tu katika mazingira tata, mara ya mwisho alitolewa gerezani usiku na mwenzake Nusrat Hanje , ambaye baadaye alipewa Ubunge na Job Ndugai.

Bado haijafahamika sababu hasa ya Serikali zote za CCM kumuogopa kijana huyu, kiasi cha kuwatumia Polisi kumkamata kila uchao.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kuwakanya wanaccm wenzake kuhusu madhara ya kuitegemea Polisi .

View attachment 2280000
Ukoo wa Panya buku!!
Acha unoko wewe na buku Zako.
 
Back
Top Bottom