Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,628
- 218,059
Taarifa za Uhakika kutoka kwenye Jopo la Wanasheria wa Chadema, zinaonyesha kwamba mmoja wa mashahidi Muhimu watakaohitajika kutoa ushahidi Kwenye kesi inayokikabili chama hicho dhidi ya Wabunge wasaliti Waliofurushwa na wanaolindwa kwa udi na uvumba na Serikali ya Tanzania, ni ndugu Twaha Mwaipaya ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa Taasisi bora kabisa ya Vijana Duniani (Bavicha) .
Inadaiwa Mwaipaya anayo Majina ya viongozi wa NEC, Bunge na maofisa wa vitengo vingine wanaotajwa kuwezesha mchakato wa Kuwatoa Jela Usiku mwingi ili Mfungwa Nusrat Hanje akaapishwe bungeni.
Tayari kitengo chetu kinayo majina ya maofisa hao, bali hatutawataja hapa kwa vile Sheria za Tanzania zinakataza mambo yaliyo Mahakamani kujadiliwa mitaani au mitandaoni.
Iko haja kwa angalau miezi hii michache Mwaipaya akaongezewa ulinzi kwa ajili ya Masilahi mapana ya Demokrasia na Haki .
Mungu Ibariki Chadema .