Kwanini Serikali isiige mfumo wa elimu kama IST?

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Hii shule ni Moja kati ya shule bora katika kuaanda watoto level ya primary.

A full Graduate wa shule hii humlinganishi na katoto ka shule yeyote ile hapa Tanzania katika communication skills.

Nimefikiria na kujiuliza hivi kwanini serikali isijaribu walau kuiga mfumo wa shule walau katika shule chache ndani ya Tanzania katika kanda tofauti.

Maana walimu wa shule hizi wapo pia Watanzania wenzetu na tena wamesoma katika vyuo hivi hivi vyetu na hata hao volunteers watakuja kwa wingi watasaidia pia katika hizo shule chache zitakazo chaguliaa.
 
IST wanatumia NECTA?
Usiwe mgumu kuelewa vitu vyepesi ndugu , ndani ya iyo mtaala wa nacte wana weza waka transfer techniques, toka izo shule kama IST zika fit ktk ma shule yetu ya kata mwisho wa siku tukatokomeze ili tabaka la elimu bora na bora elimu walau lipungue kwa level flan.
 
Walimu wengi wa IST ni Wakenya, wako na mishahara 'minono' and btw, uko tayari kulipa 50m ya ada?
Mkuu sio 50M ni above 84+ Mkuu.

Ingawa jamaa ana hoja yake kuwa tukopi mfumo wao full mwanzo mwisho.

Vijana wakisoma wanakuja kuwafundisha wenzao Hao Hao. Yaani hata tuanze upya mfano kuanzia 2025 sheria hiyo ianze kutumika pia. Mbona 2023 sheria mpya ya FAO inaanza kutumika ama kisa haina manufaa kwao.

Kuna mdau mmoja amedai kuwa watamtawala nani mana wanasiasa hawapendi watu wawe wajanja sana. Kuna mdau kachangia ivyo hapo juu.

Pia nadhani huu mfumo hauna kwao manufaa kwao ni kama kuna mdau mmoja amesema kuwa bora rule nyasi ila tuchimbe chuma mana tutakitumia wenyewe kwa sgr construction sema ndo ivyo jamaa hawana nacho manufaa mana huwezi kuweka ki pande cha chuma kwenye begi ukatoka nalo so hawaiipigii chapuo.
 
Walimu wengi wa IST ni wakenya, wako na mishahara 'minono' and btw, uko tayari kulipa 50m ya ada?
Hapa ndipo shida yetu, mwalimu awe mkenya awe mtanzania akipita katika mtaala wa shule husika na akawa anakaguliwa regularly kupima uwezo wake wa kudeliver always anatoa matokeo mazuri.

Sisi katika kuiga huko tunaweza kuiga vichache vizuri hasa TEACHING activities e.g lessons, strategies vitu kama ivi.
 
Hebu mjumbe tuwekee mtaala wanaofuata or even syllabi ili tuone sisi tunapwaya wapi. Kama shida ni syllabus, uwezo wa walimu wetu, au vitendea kazi
 
Kwanini tusisaidiane na serikali katika kutatua kwanza changamoto za msingi kama upatikanaji wa madawati na vyumba vya kutosha vya madarasa kisha hayo mengine yakafuata?

Au mnasemaje ndugu zangu?
 
Ingawa jamaa ana hoja yake kuwa tukopi mfumo wao full mwanzo mwisho.
kukopi mfumo wao ni useless, kama hakutakua na miundombinu mizuri ( vifaa vya practical vya kutosha) huko labs

darasa lenye watoto 300 ( wote wanakaa chini ) badala ya 10 ,

leo hii mtoto za Azania anaenda kufanya praktiko Pugu :cool::cool:
 
Kwanini tusisaidiane na serikali katika kutatua kwanza changamoto za msingi kama upatikanaji wa madawati na vyumba vya kutosha vya madarasa kisha hayo mengine yakafuata?

Au mnasemaje ndugu zangu?

Subiri kwanza tumalize kulipa kodi kwny harusi, birthday, send-off then tutachangia madawati.
 
Mtaala wao siyo wa Tanzania
Nafikiri bado haujaelewa. Hatuchukui mtaala wao. Tunachukua vichache vinavyowafanya watoto wao wawe bora then tuna vihuiwisha ktk mtaala wetu wa shule za jamii chache kwa kuanzia. Sasa vitu vya ku transfer sio limfumo lote ni baadhi mfano TEACHING startegies/techniques, maada za kujifunza n.k
 
Hii shule ni Moja kati ya shule bora ktk kuaanda watoto level ya primary.

A full Graduate wa shule hii humlinganishi na katoto ka shule yeyote ile hapa Tz ktk communication skills...
Nia ya wanasiasa wetu ni kutaka kuona kuwa the majority ya Watanzania wanapotelea kwenye ujinga ndio maana wanawapa bora elimu na si elimu bora.

Na hii inafanywa makusudi ndio maana watoto wao wanasoma nje au kwenye shule nzuri zilipo nchini.
Hawasomi hizi shule za Tamisemi
 
Nafikiri bado haujaelewa. Hatuchukui mtaala wao. Tunachukua vichache vinavyowafanya watoto wao wawe bora then tuna vihuiwisha ktk mtaala wetu wa shule za jamii chache kwa kuanzia. Sasa vitu vya ku transfer sio limfumo lote ni baadhi mfano TEACHING startegies/techniques, maada za kujifunza n.k
Ni vizuri lakini pesa pia inachangia, walimu na wafanyakazi wanalipwa vizuri sana, hivyo wanafanya kazi bila mawazo, watoto mazingira wanayosomea wana kila kitu, serikali kama shule zake madarasa hayatoshi watoto hawana madawati, walimu wengine wanafundisha tu kwakuwa wapate pesa unadhani itawezekana mkuu?
 
Usiwe mgumu kuelewa vitu vyepesi ndugu , ndani ya iyo mtaala wa nacte wana weza waka transfer techniques, toka izo shule kama IST zika fit ktk ma shule yetu ya kata mwisho wa siku tukatokomeze ili tabaka la elimu bora na bora elimu walau lipungue kwa level flan.
Ili iweje?

Mfumo wa elimu uliopo unawanyima nini watawala mpaka waubadilishe?
 
Back
Top Bottom