Kwanini serikali inakuwa mshindi tuu kwenye kila kesi ya migomo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini serikali inakuwa mshindi tuu kwenye kila kesi ya migomo?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Wild fauna, Aug 3, 2012.

 1. Wild fauna

  Wild fauna JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 427
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Salam jf
  inakuwa ni vp kila serikali inapokimbilia mahakamani yenyewe ndio inakuwa mshindi? Does it mean kuwa yenyewe iko perfect wakati wote?
  Mathalani tazama migomo ya madaktari pamoja na walimu,hivi ni kweli haya makundi yalikurupuka na hayakuwa na hoja za msingi?
  Ni kwa vp mahakama imetuaminisha kuwa ni chombo cha haki?
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Serikali hata siku moja haiwezi kua mshindi. Wagonjwa kufa bila sababu na wanafunzi kutosomeshwa huo ushindi wanautoa wapi. Mahakama sio chombo huru hata jaji augustino ramadhani alishawahi kusema mahakama inaingiliwa sana na serikali kwenye maamuzi yake. Ingekua ni chombo huru wasingesema hiyo migomo ni batili.
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...mahakama ni kichaka cha watawala.
   
 4. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  hakimu kachaguliwa na raisi, walimu wanaigomea serikali ya raisi uyo uyo, ah bana kesi ya ngedere akiamua tumbili wadhani tumbili atashindwa?? Chukua hatua
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Hilo liko wazi, serikali inaziamuru mahakama kutoa hukumu in its favour! Lakini tunakoelekea siko,wananchi tayari wameshapoteza imani na mahakama,kuna wakati mahakama zitatoa amri hazitosikilizwa na zitabezwa na huo ndo utakuwa MWANZO WA MWISHO
   
 6. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Halafu ikija kwenye kesi kama za Dowans lazima ishindwe. Je unaelewaje? Tafakari na chukua hatua.
   
 7. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Mahakama inaingiliwa sana sasa hivi,haziko huru tena,yani imefikia mahali ukiwa una dai haki yako halafu serikali inakuambia nenda mahakamani unajua ndio kwisha hivyo.
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Mahakama ni Chombo cha kuisaidia serikali,kudhurumu,kuiba na kunyanyasa wanyonge,mimi binafsi sina imani na mahakama hata kidogo.
   
 9. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Na kweli kama mwendo wa mahakama ndio huo, kuna siku watu watakataa kutii amri za mahakama maana si za haki. hawa majaji wa EPE ndio tatizo lao. Amewajaza bila sifa hata kidogo.
   
Loading...