Kwanini Serikali imesamehe Shilingi Trilioni 424?

Tunakunaliana na Lissu ....
mtetezi wa Acacia...
JPM amefanya maamuzi ya kijinga sana.
hatuna sababu ya kushukuru kulipwa kidogo.
hatuna sababu ya kushukuru hisa kupanda.

Wafuasi wa Lissu tuna akili sana
hisa 16% na wao 84%

Yaani unamaanisha tumenunua hivyo vi hisa kiduchu kwa Trilion zetu 424?. Pesa ambayo thamani yake ni bajeti ya nchi yetu kwa miaka zaidi ya 10 bila kuhitaji kusaidiwa na wahisani
 
Duh aiseee Dunia sio fear kabisa yaani halmashauri yangu imegoma kabisa kunisamehe kodi ambayo hata sikuitumikia kibiashara ambayo haizidi hata milioni ila wanaenda kuwasamehe mabeberu pesa yote hiyo!!!
 
Mkuu JokaKuu!

Yaani hili zoezi lilivyokuwa linaendeshwa huwa najisikia hadi aibu! Cha ajabu watu tulikuwa tunasema humu kwamba hao wote ni wamoja na wanachofanya ni drama... lakini watu wakaendelea kupiga vigelegele! Yaani kabisa wakawa wanaamini mwenye 34% Shares anaweza kumvimbia mwenye 66% shares!

Inaumiza sana kufanywa matahira! Yaani pale Magufuli Administration mbele ya Barrick inaonekana wazi kwamba ni hamna kitu!
 
Wewe uliamini ile rubbish report toka kwa wale rubbish professors? Hivi ni wapi uliwahi kuona chuma kinasafirishwa kwenye makonteina?

Ile report kwa yeyote mwenye uelewa wa sekta ya madini, anajua ilikuwa na uwendawazimu.
 
Again umejionyesha una IQ ya kiwango gani,jibu hoja yangu kwa hoja bora zaidi,ujibuji wako tayari unajionyesha ni mwana JF wa jinsi gani,huu ni mjadala ni vema tukajadiliana hatuwezi wote tukawa na msimamo mmoja ila FACTS zibakie hivyo,na elewa tuna haki ya kutofautiana .
 
Me nauliza jamani, hivi trillion zikiwa 1000 ni sawa na pesa ngapi(Nataka jina la pamoja)
 

..nilichoka walivyoita WASANII ambao waliimba kabla ripoti haijawasilishwa.

..sijaona popote ripoti za uchunguzi , za kitaalamu , zikiwasilishwa baada ya wasanii kitumbuiza.

..ripoti zile ziliwasilishwa kwa USHABIKI mkubwa, na serikali na JPM, kwa maoni yangu, wali-OVERPROMISE lakini kwa matokeo haya wame-UNDERDELIVER. Wametuangusha.

NB.

..na hapa bado hatujaangalia kilichomo kwenye makinikia.

..Jpm alidai mwenye yale makonteina kuna dhahabu inayojaa lumbesa kwenye lori saba za tipper, na landrover moja.

..Je, madai hayo ni ya kweli?
 
[Hapa na mimi huwa nakonda kiakili kila nitafutapo maelezo ya suala hili, hususani hiyo tofauti ya mihela QUOTE="Missile of the Nation, post: 33259409, member: 490108"]
Dola milion 300 ni sawa na shilingi 0.67 Trilion

Sisi tunawadai Trilion 424

wanachoturudishia hakifiki hata Trilion 1, Si uwendawazimu huo?
[/QUOTE]
 
Me nauliza jamani, hivi trillion zikiwa 1000 ni sawa na pesa ngapi(Nataka jina la pamoja)
Quadrillion ambayo inakuwa na ziro 15 yaani 1,000,000,000,000,000.
Million: 1,000,000
Billion: 1,000,000,000
Trillion: 1,000,000,000,000
Quadrillion: 1,000,000,000,000,000
Quintrillion: Hii ina ziro 18.
 
Quadrillion ambayo inakuwa na ziro 15 yaani 1,000,000,000,000,000.
Million: 1,000,000
Billion: 1,000,000,000
Trillion: 1,000,000,000,000
Quadrillion: 1,000,000,000,000,000
Quintrillion: Hii ina ziro 18.
Duuuh, mkuuu...!!!! Sasa hii Quintillion 1 tu si inaweza kuwa bajeti ya Dunia nzima kwa mwaka...!!!
Ila thanks kwa kunitoa huu ujinga
 
[emoji23][emoji23][emoji23] kwamba tipa na landlovr
 
JokaKuu

Report za Barrick zipo wazi kwa sababu kampuni hii ipo listed na LSE ambapo kwa mwaka matokeo ya operations zao zote duniani zipo wazi. Hiyo ni pamoja na ACACIA faida iliyopatikana wakati wakifanya uchimbaji Tanzania. Hizo figures za 191 billion zipo juu sana na waliweka what they get yearly worldwide, na hiyo ndio ilipelekea maridhiano.
 
Kwa hivyo ripoti za maprofesa wetu zilikuwa ni "pishi" tu? Kutoka trilioni 420+ mpaka bilioni 700! Na Lissu aliziita "professorial rubbish".

Kuna nyakati nachukia sana tunavyowaita hawa wazungu "mabeberu", huwa najiuliza ina maana sisi ni "mbuzi jike"? But kwa vitu kama hivi, pengine ni halali tu tuendelee kuwaita mabebereru!
 
"Wanaume " wasingekubali kulipa madai yaliojengwa juu ya ripoti ambazo ni "professorial rubbish". Hivi nani amewahi kuyasoma hayo makitu? Au ndiyo tulipigwa sound tu. From $190B to $300M hiyo ndiyo kazi ya "mwanaume".
 
kama wameshakuja na terms mpya za uendeshaji na tumekubaliana bado mnatumia technic ya MEGA kututisha?[emoji16][emoji16]
na tutambue kuwa hii kesi in a long term tutaathirika mno,maana wawekezaji wa madini wame I RED FLAG nchi yetu na tumo namba 2 kutoka chini kwa nchi ambazo ni HIGH RISK KUWEKEZA KWENYE NYANJA HII YA MADINI.
 
Lissu aliita hiyo report Professorial rubbish. Alikuwa Sawa. Kama migodi mitatu ingekuwa inatoa faida hivyo basi nchi kama Botswana au Namibia Wangekuwa wanaishi peponi kwa madini waliyonayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…